↧
MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO
↧
"BIASHARA NI KAMA VITA"–(1)
NA MARKUS MPANGALA
NOVEMBA 8 mwaka huu Bunge la Jamhuri ya Muungano lilikataa kusaini mkataba wa Ushiriakiano na Jumuiya ya Ulaya (EPA) ambao mchakato wake ulianza mwaka 2001. Mwanazuoni Yash Tandon ni ameeleza kwa kina ubaya na hatari ya mkataba wa EPA kupitia kitabu chake cha “Trade Is War; The West’s War Against the World,’ chenye jumla ya kurasa 196. Kitabu hichi kimechapwa mwaka 2016 na Kampuni ya Mkuki na Nyota na kikapewa nambari 978-9987-75-342.
Tandon anasema Afrika inatakiwa kuwa makini kwenye mikataba ya aina hiyo. Anaelezea jinsi Marekani, Ulaya na Japana zinavyolitumia Shirika la kibiashara duniani (WTO) kwa madhumuni ya kuchota rasilimali za mataifa madogo. EPA (European Partnership Agreement) ni mojawapo ya silaha kubwa iliyopangwa kuchota rasilimali na kuua soko Afrika mashariki. EPA inataka asilimia 80 ya masoko ya ndani yaachwe wazi na kuruhusu kuingizwa bidhaa za Ulaya.
Tandon anasema Afrika inatakiwa kuwa makini kwenye mikataba ya aina hiyo. Anaelezea jinsi Marekani, Ulaya na Japana zinavyolitumia Shirika la kibiashara duniani (WTO) kwa madhumuni ya kuchota rasilimali za mataifa madogo. EPA (European Partnership Agreement) ni mojawapo ya silaha kubwa iliyopangwa kuchota rasilimali na kuua soko Afrika mashariki. EPA inataka asilimia 80 ya masoko ya ndani yaachwe wazi na kuruhusu kuingizwa bidhaa za Ulaya.
Anasema mabadiliko ya kiuchumi yamezua vichekesho kwa uchumi wa kimataifa na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla, ingawa China imeleta taswira mpya. Mataifa hayo yamevumbua mbinu mpya ya kibiashara na kuunda kundi la G20 lililolazimika kuziingiza nchi hizo kuleta uwiano. Kuanzishwa BRICS (Brazil, Russia, india, China na South Africa) kumechochea mabadiliko ya kibiashara na uchumi.
China ilianzisha Benki ya Miundombinu (Chinese Infrastructure Bank) ambayo ilikuwa mahususi kushughulikia miradi ya ujenzi wa miundombuni na mikopo kwa kampuni za uhandisi ili kuchochea mapinduzi ya sekta hiyo. Mwaka 1995 nchi zinazoendelea kiuchumi zilisafirisha bidhaa kwa asilimia 42. Mwaka 2103 nchi hizo zimesafirisha bidhaa kwa asilimia 57, ambapo nusu yake zilikwenda China. Asilimia 60 ya biashara za nchi hizo zilikwenda India na Brazil. Kuanzia mwaka 2001-2011 biashara kati ya Mataifa ya Afrika na BRICS ilikuwa kutoka dola bilioni 22.9 hadi dola bilioni 267.9.
Licha ya umuhimu wa ushirikiano kati ya Afrika, Ulaya, Marekani kwa pamoja na Brazil, India na China, bado hakuna usawa wa biashara baina ya mataifa makubwa na madogo. China ndiyo mdau mkuu wa biashara na Afrika kwa dola bilioni 198.5 wakati Marekani na Afrika ni dola bilioni 99.8 kwa mwaka 2013. Uwekezaji wa China barani Afrika hadi mwaka 2014 ulikuwa dola bilioni 40. India imepenya soko la Afrika kupitia kampuni za Bharti, Essar na Tata.
Tandon anafichua mikataba inayosababisha kikwazo cha maendeleo ya kiuchumi katika nchi za Afrika, ACP (Africa Caribbean na Pacific), makoloni ya zamani kubanwa na mikataba ya Lome Convention I,II&III na Cotonou.
Vibano walivyovipata kwenye mikataba hiyo ni vidogo kuliko vile vya mkataba wa EPA kama ungesainiwa. Anaeleza mpambano mkali wa vikao uliokuwapo jijini Dar es salaam kati ya timu ya ushawishi wa mikataba ya EU dhidi ya Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC).
Kwamba Shirika la biashara duniani (WTO) linafanya kampeni kuzifukarisha nchi ndogo kupitia taratibu na sheria zake.
BIASHARA NI VITA
Tandon anakuja kufafanua kwanini kitabu hiki amesema biashara ni vita. Toka zamani biashara ni silaha kubwa katika vita vya maslahi kati ya mataifa tajiri na masikini. Matokeo yake vita hivyo ni wimbi la watu wanaoitwa wahamiaji kukimbia umasikini na ufukara katika mataifa machanga na kwenda mataifa tajiri.
Vita vya kibiashara vilisababisha kesi ya wakulima wadogo wa Kenya (Kenya Small Scale Farmers) dhidi ya serikali iliyokuwa ikishinikizwa isisaini mkataba wa EPA. Anasema biashata ilichangia ukoloni na ukoloni mambo leo huko India, kuanguka kwa ufalme wa Ottoman, umasikini wa Mexico na mataifa mengine ya Amerika kusini.
Anaonyesha namna mataifa ya Afrika yanavyoweza kufanya vizuri kwa kuimarisha ushirikiano wa ndani; COMESA, SADC, na EAC. Anatolea mfano hoja za waziri wa biashara wa Rwanda Monique Nsanzabaganwa alivyoweza kuwashawishi mawaziri wa biashara katika mkutano wao uliofanyika Kigali (Uk.17-18).
Anaeleza kuwa mbali ya mikataba hiyo mara nyingi hutumiwa MFN yaani kwa kimombo ‘Most Favoured Nation’ ili kuingia kirahisi soko la ndani kwa manufaa yao. Vikwazzo vya kibiashara hutumika kama nyenzo ya kuhakikisha ufukara na dhiki vinaielemea nchi husika, hivyo kuilazimu kupiga magoti kwa WTO (Uk.21-23).
Changamoto kwa mataifa ya Afrika kubaini utapeli wa kibiashara unaokuja kwa lugha tamu tamu. Anasema hakuna usawa katika shirika la biashara duniani. Anatoa mfano mikataba ya Singapore, Doha, Seattle na Canncun ambayo inasisitiza ‘Fair Trade For Africa’ kwamba ni ulaghai kwani imesababisha ajira za mamilioni ya watu kupotea pamoja na ufukara kuongezeka (Uk.24-26)
Itaendelea
KUPATA KITABU HIKI, PIGA SIMU NAMBA 0718144517/0685115758.
↧
↧
PROFESA KITILA MKUMBO ANG'ATUKA UANACHAMA ACT-WAZALENDO
↧
MTAHINI ANAPOKUWA MTAHINIWA.
NA KIZITO MPANGALA
Nchini Nigeria zaidi ya walimu 20,000 kufutwa kazi kutokana na "hat trick" iliyofanywa na serikali ya nchi hiyo kwa kuwatahini walimu mitihani ile ile ambayo huwa wanawatungia wanafunzi wao.
Walimu zaidi 20,000 wamafeli mtihani huo hali ilinayofikirisha wengi kuwa inakuwaje mtahini ashindwe utahiniwa? Hivyo, uamuzi wa serikali ya Nigeria ni kiwafuta kazi wale wote ambao wamefeli mtihani huo.
Hilo linanikumbusha mwaka 2011 ambapo mwalimu mmoja wa Seminari ya Likonde nchini Tanzania alitoa simulizi fupi kuhusu mchakato na manyanyaso waliyokuwa wakipata msimu wa kusahihisha mitihani ya kitaifa ambao ulikuwa ukifanyika jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa wizara ya Elimu pamoja na wale wa baraza la mitihani wakati huo walikuwa wakiwataka walimu wanaokuja lusahihisha mitihani hiyo watahiniwe kwanza ndipo wajue nani anafaa kusahihisha.
Walimu wote kwa ujumla walitoa pendekezo kwamba wao waanzr kuwatahini viongozi wote wa wizara ya elimu na baraza la mitihani mtihani uleule uliofanywa na wanafunzi wao ndipo wajue kama wanafaa kusimamia Elimu nchino. Hapa hapakitosha kabisa! Hakuna aliyetaka kuaibika!
Hivyo basi, Nigeria wameua lufanya hivyo na wamewanasa waliowataka. Taifa la Nigeria lina watu wengi sana barani Afrika hivyo utoaji Elimu una changamoto kubwa. Hali hii imeilazimu serikali kuruhusu shule nyingi binafsi kianzishwa kwa ada elekezi.
RAI:
Lengo siyo kuwaaibisha walimu, lengo ni kujua nani ni nani katika nini. Hilo siyo mbafala wa vyeti feki. Hivyo, ingawa kuna maswali Mengi ya kuuliza kuhusu jambo hilo, ni vema walimu wawe na utamaduni wa kuperuzi vitabi mbalimbali kulingana na somo husika analofundisha ili kujiimarisha katika ufahamu na kuweza kiwapa wanafunzi kinachostahili.
Pia serikali iongeze ubora vitabu na kuchapisha vingi na ikibidi hata vitabu vya ziada viruhusiwe kwa kuwa vipo vingo vizuri na bora. Na jambo la mwisho ni kuwajali walimu. Si tu yule anayeitwa profesa ndiye anastahili kujaliwa, bali yeyote aliye mwalimu anastahili hilo. Na walimu wenyewe wajielewe kuwa wao ni walimu.
©Kizito Mpangala
↧
CATALUNYA IMENIKUMBUSHA WIMBO WA TAIFA WA HISPANIA.
NA HONORIUS MPANGALA, 0628994409
ILIKUWA katika mechi ya kombe la dunia mwaka 2002,Korea kusini na Japan ndiko nilipohitimisha majibu ya maneno ya kusimuliwa. Kaka yangu alikuwa mtu aliyependa kunisimulia kuhusu vibweka vya kwenye soka tangu zamani na hajaacha hadi Leo. Naweza kusema ndiye aliyefanya nikawa napenda soka na kulichambua.
![]() |
Wachezaji wa Hispania wakishangilia moja ya mabao waliyofunga. |
Mechi ilimalizika kwa magoli ya 3-2 lakini ikiwa na upinzani mkali. Hapo unaizungumzia Bafana Bafana ya Lucas Radebe na Ben McCarthy. Na Hispania ya Raul Gonzalez na Gaizka Mendieta.
Alianza Raul Gonzalez dakika ya nne, bao lake likasawazishwa na Ben McCarthy dakika ya thethini na moja. Gaizka Mendieta akafunga dakika ya arobainina tano lakini walipotoka mapumziko dakika ya hamsini na tatu Radebe akasawazisha. Bao hilo halikudumu muda mrefu dakika tatu baadae Raul tena akawainua wa Hispania.
Sasa moja ya vile vibweka kabla ya mechi ndo nikichokiona katika timu kuimba myimbo za taifa. Wakiwa katika mstari niliwasikia Vijana wa Thabo mbeki wakati huo wakiachama midomo yao huku wakiimba ule wimbo pendwa wa 'Nkosi Sikelel'i Africa' yaani Mungu ibariki Afrika uliotungwa na Mwalimu Enock Sontonga. Wimbo huo ndio uliochukuliwa ubeti wa kwanza na taifa letu la Tanzania na kuongeza maneno katika ubeti wa pili na tukautumia hadi Leo.
Zamu ya wahispania ilipofika nilishangaa kuona vinywa vya wachezaji wa Hispania havinyanyuki na kuimba chochote. Maneno ya kaka yangu nikahitimisha pale kwani aliwahi niambia juu ya hilo nilisubili kuhakikisha. Licha ya kuwa na Ala nzuri ya mziki katika wimbo wao wa taifa ambao unaoitwa 'La Marcha Real' lakini hawakuwa na neno la kutamka.
Nilipotazama nyuso za kina Fernando Morientes zilikuwa zikionyesha heshima kwa taifa kwa kusimama kwa utulivu kama ilivyo kawaida ya nyimbo za taifa lakini ndani ya sekunde 56 za 'La Marcha Real' hakukutoka neno lolote.
La Marcha Real ni wimbo uliotungwa ala yake ya muziki na mmoja wa makamanda wa jeshi la Hispania aliyeitwa Fransisco Gau Vegara. Kutokana na kushiriki katika kikundi cha muziki jeshini ndipo alipotunga wimbo ambao kutokana na mvutano ilikuja kubakishwa ala pekee bila maneno.
Hispania ni miongoni mwa mataifa manne ambayo hayana maneno katika wimbo wa taifa.Nchi kama Bosnia & Herzegovina,Kosovo na San Marino ni miongoni mwa mataifa ambayo yanatumia ala pekee bila maneno.
Ziko sababu zilizopelekea haya kuwepo katika mataifa haya kutokuwa na maneno katika wimbo wa taifa. Kwa nchi ya Hispania Tangu zama utawala wa mfalme Alfonso XIII ilishindikana kupatikana maamuzi ya lugha ya kutumia katika wimbo wa taifa.
Kutokupatikana kunatokana na mvutano uliotoka katika jamii zilizoonyesha kuwa na msimamo kwa kutaka lugha yao itumike na wengine wakikataa kutumia lugha wenzao katika wimbo huo. Licha ya kuwepo kwa lugha ya kihispania lakini jamii hizi zilionyesha kutaka kupata mamlaka katika wimbo kutumia lugha yao.
Jamii ya watu Basque ambako ndiko unakopatikana mji wa Bilbao walikuwa na msimamo wao. Na ni kati ya majimbo yanayosemekana kuwa na ubaguzi mkubwa nchini Hispania. Pia watu wa Katalunya iliko Barcelona nao walivutia ngozi kwao.
![]() |
Kocha mkuu wa Timu ya taifa ya Hispania, Julem Lopetegui |
Katika lugha nyepesi unaweza kusema Hispania kuna ubaguzi wa kila jamii kujiona bora kuliko nyingine. Na imekuwa ni mambo ambayo yametoka Tangu zama za viongozo wao kama Dikteta Fransisco Franco hadi Leo.
'Umimi'walioupanda Tangu utawala wa viongozi hao umeendelea kuwatafuna hadi sasa.Ni rahisi kwa Ander Herrera kukubali kiwepesi kwenda kucheza katika klabu ya Athletic Bilbao na ukamshangaa akitosa kwenda Real Madrid au Bercelona. Hii yote kutokana na ubaguzi waliokua nao Tangu wangali wadogo kule Basque.
Wakati wa kampeni za majiji kuandaa mashindano ya olimpiki mwaka 2016, Rais wa kamati ya olimpiki nchini Hispania alichagua kutumika maneno ya wimbo wa klabu ya Liverpool. 'You will never walk alone ndo maneno ambayo kamati hiyo kupitia rais wake walitaka yaweze kufasiliwa na kutambwa katika ala ya 'La Marcha Real'.
Hali hiyo ilitokana na jamii hizo za watu wa Basque, Katalunya,Galician na mengine kuandaa maneno kwa lugha zao. Na nafasi ya kuandaa mashindano hayo ikadondokea Rio de Jeneiro nchini Brazil.
Kinachoendelea sasa katika jimbo la Katalunya waweza kusema ni mwendelezo. Mwendelezo huu ni ule uliofanya kama waHispania kushindwa kuwa na maneno katika wimbo wa taifa. Ubaguzi ni zambi inayowatafuna Tangu zamani.
Sitashangaa kuona watu wa Basque nao siku moja wakiamua kufanya harakati za kujitenga.Siasa na masuala ya utawala yamefanya taifa hilo kuweza kuingiza ubaguzi wao hadi katika soka. Ni rahisi kwa nyota wa Bilbao akacheze nje ya Hispania kama ilivyokuwa kwa Javier Martinez kucheza Bayern munich kuliko Barcelona.
Wakati Pep Guardiola akiwa kocha wa Barcelona alimhitaji katika vipindi tofauti mchezaji yule lakini ikashindikana. Lakini ilikuwa ni biashara inayoweza kufanyika kwa Bayern Munich kuliko kwenda Katalunya.
Ligi ya Hispania ilianzishwa na klabu tatu ambazo zinatoka katika maeneo tofauti yenye mvutano wa kiitikadi ya kiutawala wa kisiasa yaani klabu ya Bilbao toka Basque, klabu ya Real Madrid toka katikati ya nchi kwa jamii ya wacastile na Barcelona kutoka kwa wakatalunya.
Katika mataifa mengi ulaya yana ubaguzi wa kikanda au kijamii kama ilivyo kwa baadhi ya nchi hapa Afrika.Lakini wamekuwa watu wenye kuuficha ukweli na mwisho hutokea aibu kama hizi za kutaka kujitenga kwenye sababu za kibaguzi.
Vuta picha eti wimbo wa taifa letu usingekuwa na na maneno ya kuimba sijui mataifa ya ulaya Wangeongeleaje hilo. Kufanikiwa kwa Wakatalunya kujitenga ni ngumu kutokana na Hispania kutotaka kuaiachia Katalunya yenye kuchangia mapato ya nchi asilimia 20.
Watu wa Ulaya wana mengi ambayo ukichunguza unabaini ni kama vile wao wanavyozisema nchi za afrika kutokuwa na umoja.Wanaongea hayo mbele ya kamera lakini moyoni wakiwa na majibu kuwa aheli wawe kama walivyo kuliko kuungana kama ilivyokuwa malengo ya Muamary Gaddafi.
Tukio la Hispania katika jimbo la katalunya litakuwa na sura ya tofuati katika kuiweka hali sawa ya ligi yao ya BBVA. Maana ni kama siasa na ubaguzi umekolezwa miongoni mwa nyoyo za mashabiki na wachezaji.Ndo maana haikushangaza kuona mlinzi wa Barcelona Gerrard Pique akiwa anapiga kura huku Sergio Ramos akashikilia bendera ya taifa lao na kuonyesha uzalendo.
↧
↧
SOMO LA LEO
“Mheshimiwa Kakunda (Joseph –Naibu Waziri Tamisemi) nakuagiza kuanzia leo maana wewe ndiyo nimekukabidhi jukumu la elimu, nataka mtihani wa 2019 shule za vipaji zote 22 ziongoze mtihani wa Taifa na shule binafsi ziwe nyuma, lakini tuongoze kwa halali si ubabaishaji hapo ndipo shule binafsi za makanjanja zitajifuta zenyewe,”
-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo.
↧
TAARIFA KWA WANAHABARI
CHAMA cha ACT Wazalendo leo Oktoba 11/2017, kimewasilisha Mahakamani kesi ya kupinga uteuzi wa Katibu wa bunge uliokiuka Katiba na sheria za nchi. Taarifa zaidi juu ya suala hilo zitatolewa kesho baada ya taratibu za kimahakama kukamilika.
Abdallah Khamis
Afisa Habari ACT-Wazalendo
↧
TUACHANE NA DUNIA YA MICHONGO NA MADILI.
NA KIZITO MPANGALA
PICHANI ni duka la dawa za binadamu. Unaona limefungwa. Limefungwa kwa sababu maalumu kisheria. Tazama jinsi lilivyo, kwa nje hata utambulisho ya kwamba hili ndilo duka mojawapo miongoni mwa maduka ya dawa za binadamu lifahamikalo katika mtaa husika.
Hatupo kwa ajili ya kuharibiana wasifu. Hatupo kwa ajili ya kubaniana michongo na madili. Hatupo kwa ajili ya kukatishana tamaa. Wakati ule nilipokuwa Mseminari tulikuwa tukifimdishwa kitu kinachoitwa "DHAMIRA". Tuwe na dhamira zenye kujali uwepo wa wengine.
Duka hili lililofungwa liwe funzo kwa wengine ambao bado hamkuguswa kwa maana unyoya bado unapepea na utakuja kukuguseni popote mlipo. Ninaheshimu wasifu wenu nyote, ila uwe wasifu wenye nia nkema na kuachana na dunia ya michongo na madili.
Aliyekuwa anasimamia duka hili na ambaye ndiye mhusika mkuu wa umiliki wa bidhaa zilizokuwemo dukani humu HANA UJUZI WOWOTE UNAOHUSU FAMASIA. Hivyo, alikuwa akiuza dawa na kuandika maelekezo ya matumizi ya dawa kwa mgonjwa kwa kutumia UJANJA. Alikuwa ANABASHIRI tu. Ukihitaji Magnesium (Mg) anakutazama kwa makini na kukuambia POLE SANA, UNA MINYOO. Huu ni mchongo wa kibedui kabisa! Duka limefungwa.
Ifahamike kuwa dawa ya minyoo nfani yake lazima ihusishe chembe za dutu Silver (Ag), hivyo ni niambata vya "pergertives" Duka limefungwa.
Wale wenye maduka ya dawa za binadamu hata mifugo kuweni makini. Kuuza dawa iliyokwisha muda wake ni kosa na ni uharamia dhini ya uhai wa binadamu na mifugo. Faida ya fedha haikatazwi lakini tazama yule anayekuletea faida mjengee uwezo ili akufae kwa faida wakati mwingine tena. Duka limefungwa!
Siyo maduka ya dawa tu, yako maduka ua namna mbalimbali. Hata wauzaji wa simu wapo wanaouza simu zilizotumika mida mrefu lakini huvikwa vifaa vipya ili zionekane murua. Duka limefungwa!
Leo tumakinike na masuala ya dawa kwanza. Maana inawezekana mtu akakuambia anauza "Morphine" tena kwa bei kubwa lakini huenda ikawa imekwusha muda. Kama anadai kuitengeneza yeye mwenyewe huenda akawa amezidisha viambatanisho au ameweka pungufu. Ni biashara safi, lakini CHEZA KARATA YAKO VIZURI. Duka limefungwa!
© Kizito Mpangala
↧
WATALII TOKA ULAYA WATEMBELEA HIFADHI YA LUHIRA
SONGEA, RUVUMA
Watalii toka nje ya nchi wameanza kutembelea hifadhi ya Asili ya Luhira iliyopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Takwimu za mwaka 2016/ 2017 zinaonesha kuwa hifadhi hiyo imepokea watalii toka nchi za Ujerumani,Afrika ya Kusini,India,Ufaransa,Italia, Uholanzi na wageni toka mikoa mbalimbali nchini ambao pia wanafanya utalii wa kuchunguza aina ya mimea na ndege katika hifadhi hiyo.
Msimamizi wa Hifadhi hiyo Msonda Simwanza anasema wanajiandaa kuweka mazingira ambayo yatawezesha wanyama kama tembo,simba na wanyama wengine adimu kuishi katika hifadhi hiyo bila kuleta athari kwa wanyama na binadamu.
Simwanza anasema hivi karibuni Hifadhi hiyo imetumia zaidi ya sh. Milioni 15 kuleta wanyama aina ya swalapala watano na pongo wawili toka Hifadhi ya Arusha.
Moja ya vivutio vikubwa vya utalii katika mkoa wa Ruvuma ni hifadhi ndogo ya asili ya wanyama inayoitwa Ruhila Natural Game Reserve yenye ukubwa wa hekta 600 ambayo ilianzishwa mwaka 1973,ipo umbali wa kilometa saba kutoka mjini Songea.
Ndani ya Hifadhi hiyo kuna aina mbalimbali za wanyama wakiwemo pundamilia, fisimaji, nyani,pongo tumbili, kakakuona,swalapala na kobe,pia bustani hiyo ni makazi ya reptilia na ndege wa aina mbalimbali. Mtalii anaweza kufanya utalii wa kutembea kwa miguu,kupiga picha,kuangalia wanyama na ndege,utalii wa kuweka kambi(camping) na kufanya mapumziko ya mchana(picnic) hufanyika ndani ya eneo maalum.
©Albano Midelo
↧
↧
WATU WASIOJULIKANA WATAIKIMBIZA AFCON U-17 2019
NA HONORIUS MPANGALA
MWANDISHI maafuru wa fasihi kutoka Nigeria,marehemu Chinua Achebe katika kitabu cha 'Things Fall Apart' alisema kukimbia matatizo sio njia sahihi ya kutatua hayo matatizo. Wakati msomaji wa fasihi hiyo akiona kama burudani kusoma vibweka vya Okonkwo lakini kuna mafundisho katika kitabu kile. Nyakati zote huwezi kuona ugumu wa jambo kama halijakutokea.
Chinua ananifanya nihusianishe matukio ya watu wasiojulikana na hatima ya Nchi katika nafasi ya kuandaa fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Ukimya wetu katika kuchukulia kila jambo ni kitu kinachofanyika na tukashindwa kutambua tatizo au kuwabaini wahusika linaweza kutuondolea mwonekano wetu nje ya mipaka ya nchi.
Matatizo yanatakiwa kutatuliwa kwa kufahamu chanzo na kuchukua hatua ya kuyamaliza. Sisi kama Taifa tuna hamu kubwa na kuona tukifanikisha Michezo inafanyika vyema hapa nchini kwa kuhusisha sekta zote kushiriki vyema.
Labda nikumbushe jambo moja baada ya Afrika kusini kutangazwa kama waandaaji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2010.
Moja ya mataifa ambayo yalikuwa na kampeni za kuifanya Afrika kusini kama sio sehemu makini kwa fainali zile ilikuwa ni Hispania. Naweza kusema wahispania ubaguzi ni jambo ambalo watu wamekua nalo wanapenda kujiona bora kuliko wengine.
Hispania walieleza mengi yaliyohusu Usalama. Na Hayati Mzee Nelson Mandela aliihakikishia FIFA atahakikisha na waafrika kusini watakuwa wenye kutambua thamani ya nafasi waliyopewa kuandaa fainali zile. Wasauzi na waafrila kwa ujumla walichukizwa na maneno yaliyokuws yakitamkwa na Hispania na Mataifa mengine yaliyokuwa nyuma yao.
Walipoenda kucheza Mashindano ya mabara juni 2009,Hispania waliduwazwa na hali ya kiusalama kwa wasauzi maana walionyesha jinsi walivyojipanga. Licha ya kuona hali ile baada ya mashindano yale Hispania waliweza kuja na hoja nyingine mfu kuwa FIFA wakataze Mashabiki kutumia vuvuzela viwanjani kwani inaondoa usikivu kwa wachezaji. Hali hii ilikuja baada ya kuona majukwaa ya Viwanja vya Peter Mokabha,Ellis Park, na vinginevyo kama Royal Bafokeng kule Rosenberg kushambulia sana vuvuzela.
Hoja ya Hispania haikuweza kufanikiwa kwa FIFA na Wasauzi wakaweza kuishuhudia Woza kwa mizuka ileile.Hapo ndipo utakapojua mafanikio yako wako ambao wanaweza kuyatolea macho na kutamani wewe upate matatizo nao wachukue faida ya kufanya ushawishi kwa vyombo husika na kuchukua nafasi.
Watu wasiojulikana Mimi nachukulia kama matatizo yaliyoibuka nchini. Watu hao wamekuwa matatizo kwasababu hadi sasa hawajaweza kufahamika,ni ngumu na kuhatarisha maisha ya watu kwa kuishi na watu wasiojulikana nchi moja. Lolote linaweza kutokea wakati wowote kwasababu vyombo vyetu vya usalama wame tuhakikisha kuwa hawawajui hao manguli wa matukio.
Katika hali hiyohiyo ambayo sisi tulioko ndani tunaweza kuiona kama ni kawaida lakini atatokea mmoja toka kusikojulikana na kuichokonoa CAF juu ya hali ya Usalama wa raia hapa. Inatokea nchi inachukua matatizo yetu ambayo tuashindwa kuyatatua kwa kuyakimbiakimbia na kuona kama hali yeti kiusalama ni ndogo hivi hata Wageni watakao kuja kushiriki AFCON ya U 17 kutilia shaka Usalama wao wawapo nchini.
Yako mataifa ambayo yaweza kuchukua mapungufu yetu na kutaka kujinufaisha.Nani alitegema Leo hii Mashinadano ya Chan yakahamishiwa Morocco badala ya Kenya aliyekuwa mwenyeji wa kuandaa fainali hizo? Umewahi kujiuliza kwanini Caf wamehamisha fainali hizo toka Kenya hadi Morocco?
Huwezi kutumia akili kubwa kutambua sababu kuu na ya msingi. Tatizo lililojitokeza katika uchaguzi wa Kenya umefanya Chan itoweke Kenya. Hii ndo hoja kuu kwasababu historia ya Kenya katika masuala ya uchaguzi imekuwa imekuwa yenye kurejesha kumbukumbu kubwa kwa wadau wa soka.
Ikiwa uchaguzi wa Kenya ukihairiahwa na kupangwa tena. Caf wanajaribu kufikiria matokeo ya pili yatachukuliwaje kwa wakenya kwa ujumla. Je utulivu wa wakenya utakuwepo kweli ambao unaweza kufanya kusitokee na changamoto yoyote baada ya uchaguzi.
Hili lililomkuta Kenya ndilo lililomkuta Libya aliyetakiwa kuandaa AFCON mwaka 2015 lakini hali ya kiusalama ikafanya kuwe na changamoto na Caf wakaamua kupeleka mashindano Morocco ambako baada ya mlipuko wa maambukizi ya Ebola wakaamua kujiweka pembeni.Ndipo Guinea ya Ikweta ikaamua kuchukua jukumu kuokoa jahazi ikiwa imetoka kuandaa kwa kushirikiana na Gabon miaka mitatu iliyopita yaani 2012.
Tanzania mwaka 2019 itaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Na kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini watu watatumia nafasi hiyo kuelezea hali ya nchi ilivyo wakiwa na mihemko tofauti tofauti. Mara ifikapo tu 2018 tayari kila mwenye matarajio atakuwa anajipanga ili kuweza kulikabili jukwaa la siasa mwaka 2019.
Kama kamata kamata inaendelea kwa haya yanayoendela katika majukwaa ya siasa kinachojengwa katika mioyo ya watu ni chuki na watu watafikia hatua kuwa vibaraka wa Caf na kuharibu Mipango ya sisi kama nchi kuandaa AFCON U17 2019.
Matatizo ambayo yamewapata wakenya imekuwa manufaa kwa Wamorocco. Jambo pekee ambalo linaweza kufanya nchi yetu kwa kutumia watu wenye mamlaka kuweka sawa hali
ya kimifumo ya utawala na kuvutia wengi kuja.
Kama tunategemea kupata wageni watakao leta fursa ya nyongeza ya pato la taifa tunapaswa kujidhatiti na usalama. Hoja ya kutoa majibu ya kusema watu hawajulikani inafanya watu kuweka akiba ya kauli hizi na kuzitumia katika kupora nafasi yetu.
Kama waziri alitolewa bastola na Leo aliyefanya hilo tukio hajulikani inafanya tuonekane tusio makini. Kuondolewa kwa umakini wetu ndiko kutasababisha wengine kuchukua faida na kuhitaji kupora uenyeji wetu.
Tanzania hatujawahi kuandaa mashindano yaliyochini ya CAF badala yke tumefanya hayo kwa ngazi ya Cecafa. Mashindano makubwa kwa umri wa miaka nchini 17 kutahitaji 'support' ya serikali katika kufanikiwa uaandaaji wake.
Usalama wa raia ndio unaotoa ujumbe wa maisha wanayoishi watu katika nchi yao. Sio jambo dogo kuona nchi inafanikisha uaandaji wa mashindano kwani hali ya utulivu na kushiriki kwa serikali ndio mafanikio ya maandalizi hayo.
Tutumie majukwa yetu vyema ili tusitengeneze vinyongo kwa ambavyo vitatufikisha 2018 na kutokuwa na uhakika wakuandaa U17 kwa mwaka 2019. Wasiojulikana inabidi wafuatiliwe na kujulikana ili kuweka mambo sawa.
Matatizo hayakimbiwi bali watu hukaa chini na kufanya uchunguzi hatimaye kubaini Yale yenye kuonyesha uvunjifu wa amani. Kuyafumbia matukio ambayo yanahusu kuondoa usalama wa raia utatoa faida kwa mataifa mengine.Faida ninayoijadili hapa ni uenyeji wa fainali za vijana chini ya miaka 17.
Tuna ya kujifunza kwa kilichotokea Kenya kupokonywa uenyeji wa michuano ya Chan mwaka 2018. Tusijivike gunia na kujifanya hatuoni tunachotakiwa kuwajibika nacho ili kulifanya taifa liwe kama sehemu ambayo wageni hufurahia kuwepo.
Michuano hiyo ni sehemu kutangaza Utalii na vivutio vya vilivyoko katika taifa letu.Utulivu wa miji kama Arusha na ukafanikiwa kuliweka kundi mojawapo la timu kutumia uwanja wa Shikh Amri Abeid unaweza kufanya ongezeko la hamu ya wageni kutamani kuja katika nchi yetu. Lakini ili kufanikiwa hilo tunahitaji utulivu na kukoma kwa matukio yanayoibuka na kukosa ufumbuzi wa vyombo vya usalama.
Www.lundunyasablogspot.Com
0628994409
MWANDISHI maafuru wa fasihi kutoka Nigeria,marehemu Chinua Achebe katika kitabu cha 'Things Fall Apart' alisema kukimbia matatizo sio njia sahihi ya kutatua hayo matatizo. Wakati msomaji wa fasihi hiyo akiona kama burudani kusoma vibweka vya Okonkwo lakini kuna mafundisho katika kitabu kile. Nyakati zote huwezi kuona ugumu wa jambo kama halijakutokea.
Chinua ananifanya nihusianishe matukio ya watu wasiojulikana na hatima ya Nchi katika nafasi ya kuandaa fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
![]() |
Serengeti Boys wakifurahia katika moja ya mabao waliyofunga katika mechi za kimataifa |
Matatizo yanatakiwa kutatuliwa kwa kufahamu chanzo na kuchukua hatua ya kuyamaliza. Sisi kama Taifa tuna hamu kubwa na kuona tukifanikisha Michezo inafanyika vyema hapa nchini kwa kuhusisha sekta zote kushiriki vyema.
Labda nikumbushe jambo moja baada ya Afrika kusini kutangazwa kama waandaaji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2010.
Moja ya mataifa ambayo yalikuwa na kampeni za kuifanya Afrika kusini kama sio sehemu makini kwa fainali zile ilikuwa ni Hispania. Naweza kusema wahispania ubaguzi ni jambo ambalo watu wamekua nalo wanapenda kujiona bora kuliko wengine.
![]() |
Kikosi cha Serengeti Boys |
Walipoenda kucheza Mashindano ya mabara juni 2009,Hispania waliduwazwa na hali ya kiusalama kwa wasauzi maana walionyesha jinsi walivyojipanga. Licha ya kuona hali ile baada ya mashindano yale Hispania waliweza kuja na hoja nyingine mfu kuwa FIFA wakataze Mashabiki kutumia vuvuzela viwanjani kwani inaondoa usikivu kwa wachezaji. Hali hii ilikuja baada ya kuona majukwaa ya Viwanja vya Peter Mokabha,Ellis Park, na vinginevyo kama Royal Bafokeng kule Rosenberg kushambulia sana vuvuzela.
![]() |
Kocha wa timu za Vijana nchini, Kim Poulsen |
Hoja ya Hispania haikuweza kufanikiwa kwa FIFA na Wasauzi wakaweza kuishuhudia Woza kwa mizuka ileile.Hapo ndipo utakapojua mafanikio yako wako ambao wanaweza kuyatolea macho na kutamani wewe upate matatizo nao wachukue faida ya kufanya ushawishi kwa vyombo husika na kuchukua nafasi.
Watu wasiojulikana Mimi nachukulia kama matatizo yaliyoibuka nchini. Watu hao wamekuwa matatizo kwasababu hadi sasa hawajaweza kufahamika,ni ngumu na kuhatarisha maisha ya watu kwa kuishi na watu wasiojulikana nchi moja. Lolote linaweza kutokea wakati wowote kwasababu vyombo vyetu vya usalama wame tuhakikisha kuwa hawawajui hao manguli wa matukio.
Katika hali hiyohiyo ambayo sisi tulioko ndani tunaweza kuiona kama ni kawaida lakini atatokea mmoja toka kusikojulikana na kuichokonoa CAF juu ya hali ya Usalama wa raia hapa. Inatokea nchi inachukua matatizo yetu ambayo tuashindwa kuyatatua kwa kuyakimbiakimbia na kuona kama hali yeti kiusalama ni ndogo hivi hata Wageni watakao kuja kushiriki AFCON ya U 17 kutilia shaka Usalama wao wawapo nchini.
Yako mataifa ambayo yaweza kuchukua mapungufu yetu na kutaka kujinufaisha.Nani alitegema Leo hii Mashinadano ya Chan yakahamishiwa Morocco badala ya Kenya aliyekuwa mwenyeji wa kuandaa fainali hizo? Umewahi kujiuliza kwanini Caf wamehamisha fainali hizo toka Kenya hadi Morocco?
Huwezi kutumia akili kubwa kutambua sababu kuu na ya msingi. Tatizo lililojitokeza katika uchaguzi wa Kenya umefanya Chan itoweke Kenya. Hii ndo hoja kuu kwasababu historia ya Kenya katika masuala ya uchaguzi imekuwa imekuwa yenye kurejesha kumbukumbu kubwa kwa wadau wa soka.
Ikiwa uchaguzi wa Kenya ukihairiahwa na kupangwa tena. Caf wanajaribu kufikiria matokeo ya pili yatachukuliwaje kwa wakenya kwa ujumla. Je utulivu wa wakenya utakuwepo kweli ambao unaweza kufanya kusitokee na changamoto yoyote baada ya uchaguzi.
Hili lililomkuta Kenya ndilo lililomkuta Libya aliyetakiwa kuandaa AFCON mwaka 2015 lakini hali ya kiusalama ikafanya kuwe na changamoto na Caf wakaamua kupeleka mashindano Morocco ambako baada ya mlipuko wa maambukizi ya Ebola wakaamua kujiweka pembeni.Ndipo Guinea ya Ikweta ikaamua kuchukua jukumu kuokoa jahazi ikiwa imetoka kuandaa kwa kushirikiana na Gabon miaka mitatu iliyopita yaani 2012.
Tanzania mwaka 2019 itaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Na kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini watu watatumia nafasi hiyo kuelezea hali ya nchi ilivyo wakiwa na mihemko tofauti tofauti. Mara ifikapo tu 2018 tayari kila mwenye matarajio atakuwa anajipanga ili kuweza kulikabili jukwaa la siasa mwaka 2019.
Kama kamata kamata inaendelea kwa haya yanayoendela katika majukwaa ya siasa kinachojengwa katika mioyo ya watu ni chuki na watu watafikia hatua kuwa vibaraka wa Caf na kuharibu Mipango ya sisi kama nchi kuandaa AFCON U17 2019.
Matatizo ambayo yamewapata wakenya imekuwa manufaa kwa Wamorocco. Jambo pekee ambalo linaweza kufanya nchi yetu kwa kutumia watu wenye mamlaka kuweka sawa hali
ya kimifumo ya utawala na kuvutia wengi kuja.
Kama tunategemea kupata wageni watakao leta fursa ya nyongeza ya pato la taifa tunapaswa kujidhatiti na usalama. Hoja ya kutoa majibu ya kusema watu hawajulikani inafanya watu kuweka akiba ya kauli hizi na kuzitumia katika kupora nafasi yetu.
Kama waziri alitolewa bastola na Leo aliyefanya hilo tukio hajulikani inafanya tuonekane tusio makini. Kuondolewa kwa umakini wetu ndiko kutasababisha wengine kuchukua faida na kuhitaji kupora uenyeji wetu.
Tanzania hatujawahi kuandaa mashindano yaliyochini ya CAF badala yke tumefanya hayo kwa ngazi ya Cecafa. Mashindano makubwa kwa umri wa miaka nchini 17 kutahitaji 'support' ya serikali katika kufanikiwa uaandaaji wake.
Usalama wa raia ndio unaotoa ujumbe wa maisha wanayoishi watu katika nchi yao. Sio jambo dogo kuona nchi inafanikisha uaandaji wa mashindano kwani hali ya utulivu na kushiriki kwa serikali ndio mafanikio ya maandalizi hayo.
Tutumie majukwa yetu vyema ili tusitengeneze vinyongo kwa ambavyo vitatufikisha 2018 na kutokuwa na uhakika wakuandaa U17 kwa mwaka 2019. Wasiojulikana inabidi wafuatiliwe na kujulikana ili kuweka mambo sawa.
Matatizo hayakimbiwi bali watu hukaa chini na kufanya uchunguzi hatimaye kubaini Yale yenye kuonyesha uvunjifu wa amani. Kuyafumbia matukio ambayo yanahusu kuondoa usalama wa raia utatoa faida kwa mataifa mengine.Faida ninayoijadili hapa ni uenyeji wa fainali za vijana chini ya miaka 17.
Tuna ya kujifunza kwa kilichotokea Kenya kupokonywa uenyeji wa michuano ya Chan mwaka 2018. Tusijivike gunia na kujifanya hatuoni tunachotakiwa kuwajibika nacho ili kulifanya taifa liwe kama sehemu ambayo wageni hufurahia kuwepo.
Michuano hiyo ni sehemu kutangaza Utalii na vivutio vya vilivyoko katika taifa letu.Utulivu wa miji kama Arusha na ukafanikiwa kuliweka kundi mojawapo la timu kutumia uwanja wa Shikh Amri Abeid unaweza kufanya ongezeko la hamu ya wageni kutamani kuja katika nchi yetu. Lakini ili kufanikiwa hilo tunahitaji utulivu na kukoma kwa matukio yanayoibuka na kukosa ufumbuzi wa vyombo vya usalama.
Www.lundunyasablogspot.Com
0628994409
↧
KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Pichani ni Nyumba ya Mwalimu Nyerere iliyopo eneo la Magomeni ambayo kwa sasa ni makumbusho ya Taifa.
Mwaka 1957 Mwalimu akiwa anafundisha shule ya Sekondari Pugu alikusanya mafao yake ya ualimu na akamwomba rafiki yake Mustafa Songambele amtafutie kiwanja katika maeneo hayo, naye akamtafutia kiwanja hicho kilichopo Magomeni, Mtaa wa Ifunda.
Enzi hizo Magomeni ndiyo ilikuwa kama Masaki ya sasa na Mwalimu alitaka kukaa mahali penye mazingira salama na ulinzi ili kuendelea na harakati za kulikomboa Taifa kutoka kwa Mkoloni wa Kiingereza.
Lakini baadae Mwalimu kwa Moyo wa ajabu akaitoa nyumba yake mwenyewe aliyoijenga kwa jasho lake na mafao yake na kuikabidhi kwa Serikali ya Tanzania ili iwe Makumbusho ya Taifa kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo vikumbuke ni wapi tulipotoka na wapi tunaelekea.
Mwalimu wakati wa Uhai wake katika Ngazi ya Familia alikuwa Baba na Babu pia, angeweza kujilimbikizia yeye na familia yake Mali zote za Taifa lakini kwake Tanzania na Afrika nzima ilikuwa Zaidi ya Maisha yake binafsi na Familia.
↧
HAKUNA WA KUFANANA NA MWALIMU NYERERE
NA MWANDISHI WETU
"Nchi yetu inaongozwa kwa sheria. Hatuwezi kuchagua kiongozi asiyeheshimu sheria akawa anaongoza nchi kwa kushauriwa na mkewe, maana hamjui kesho akiamka atamshauri nini" Mwl. J.K. Nyerere
"Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe." Mwl. J.K. Nyerere.
"Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana"- Mwl. J.K. Nyerere
"Tatizo la paka kwa panya lingeisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: tabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo."- Mwl. J.K. Nyerere
"Mtu aliyejiandikisha kupiga kura, halafu siku ya Uchaguzi haendi kupiga kura, Huyo ni Mpumbavu'' Mwl. J.K. Nyerere
"Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana, sawa na kula nyama ya mtu,dhambi ya ubaguzi haiishi inaendelea tu, leo utabagua kwa kusema sisi ni Wazanzibari hawa ni Watanganyika ,kesho utasema sisi ni Wanzanzibari hawa ni Wazanzibara. Lazima utaendelea, utaona kuna mpemba na Muunguja. Utaendelea tu haiishi sawa na kula nyama ya mtu" Mwl. J.K. Nyerere
"Ukiona mtu anakwambia jambo la kipumbavu na yeye mwenyewe anajua kuwa unajua ni la kipumbavu..ukilikubali ujue amekudharau" Mwl. J.K. Nyerere
"Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza si kwamba rushwa haikuwepo, ilikuwepo lakini tulikuwa wakali sana.. Ikithibitika mahakamani kuwa mtu ametoa au kupokea rushwa hatukumuachia hakimu nafasi ya kutoa hukumu peke yake. Tukasema atakwenda ndani kwa miaka miwili na viboko ishirini nanne, kumi na viwili siku anaingia kumi na viwili siku anatoka akamuonyeshe na mkewe" Mwl. J.K. Nyerere
"Mnaingia karne ya 21 mmepanda basi la ukabila, mnaona sifa kuulizana makabila. Mnataka kutambika?!" Mwl. J.K. Nyerere
"Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?" Mwl. J.K. Nyerere
"Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii." Mwl. J.K. Nyerere
"Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?" Mwl. J.K. Nyerere
"Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga." Mwl. J.K. Nyerere
"Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili." Mwl. J.K. Nyerere
Siku chama kilipokuwa kinamuaga mzee Kawawa (Alipostaafu rasmi siasa za majukwaani) Katika hotuba ya shukrani alisema, pamoja na mambo mengine: ‘ "Naahidi nitakufa nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM"
Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘
"Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM?! Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi nami naachana nayo kwasababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine" Mwl. J.K. Nyerere
"Njia pekee ya kumsaidia masikini ni kumwelimisha mtoto wake". Mwl. J.K. Nyerere
"Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika" - Mwl. J.K. Nyerere (Januari, 1966)
Nukuu nyingi kati ya hizi zimo katika kitabu kinachoitwa : Reflections on leadership in Africa: forty years after independence : essays in honour of Mwalimu Julius K. Nyerere, on the occasion of his 75th birthday ' , by Haroub Othman, VUB University Press, 01 Jul 2000.
↧
“RAIS ANA MIAKA 31”
![]() |
Sebastian Kurz |
James Masters alikuwa anamzungumzia Sebastian Kurz ambaye amewahi kuwa waziri wa Ushirikiano wa Kimataigfa tangu mwaka 2013 akiwa na miaka 27. Sebastian Kurz ambaye amekuwa Kansela wa Austria mwenye umri mdogo zaidi kwani sasa hivi ana miaka 31 tu.
Ni mwenyekiti wa chama cha OVP. Sebastian kuanzia jana jumapili aanaongoza serikali ya Austria ( kama vile Rais hapa kwetu) baada ya chama chake kushinda viti vingi vya bunge.
Hitimisho la James Masters lilipa somo, anasema kwa Austria wanamwona Sebastian kama kujibu mapigo ya Ufaransa wanaoongozwa na kijana Emmanuel Macron mwenye miaka 39. Pia ni kujibu mapigo ya Canada wanaoongozwa na Justin Trudeau, mwenye umri wa miaka 45.
Nami nionavyo, katika ulimwengu wetu huu mabadiliko ya uongozi yanazidi kuchukua nafasi kubwa zaidi. Kwahiyo suala la msingi ni uwezo wa uongozi si umri wa akina 'Sebastian Kurz". Afrika tuko dunia hii, hatutokwepa hayo.
©Andunje wa Fikra
↧
↧
CHUO CHAANZISHA SHAHADA YA WADUDU
NAIROBI, KENYA
KITUO cha Elimu na Utafiti kinachofadhiliwa na Benki ya Dunia kimeasisiwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogo Oginga Odinga na kinasubiri ruhusa ya kuanzishwa kwa programu za Uzamifu na Uzamili kuhusu wadudu wanaoweza kuliwa.
Taasisi hiyo inapania kubuni njia za kuzalisha wadudu hao kwa wingi bila ya kuharibu mazingira ili kukidhi utashi mara baada ya wazo hilo likifanywa kuwa biashara.Wadudu wanaoliwa sana maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ambao wana wingi wa madini ya protini na Zinki watafanywa kuwa biashara ili kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, na kuondoa dhana mbaya katika kula wadudu.
“Kwa muda mrefu, Senene, kumbikumbi na panzi wamekuwa wakiliwa sana Magharibi mwa Kenya na wana madini mengi ya protini na zinc. Lakini imani potofu kuwahusu umuhimu wao, imefanya ulaji wa wadudu hawa kupungua na ndio maana kituo hiki ni muhimu sana,” alisema Naibu Mkuu wa Chuo Hicho Stephen Agong. Wadudu watakaoshughulikiwa mno ni pamoja na Senene, kumbikumbi na panzi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa chakula kutoka kwa wadudu, mpango huo unatazamiwa kuanza kufanyiwa kazi katika kipindi cha miezi michache ijayo na taasisi hiyo itakuwa na uwezo wa kuwapa mafunzo wanafunzi 20 wa Uzamivu (PHD) na 60 wa Uzamili ambao 35% watatoka Kenya.
↧
MANDHARI YA KIGOMA
↧
UTAMU WA WIMBO WA TAIFA UKO KOMBE LA DUNIA.
NA. HONORIUS MPANGALA
0628994409
ILIKUWA miaka Sita ya Ubabe wa soka barani Afrika kuanzia mwaka 2006 hadi 2012. Kila mpenzi wa soka alimfahamu Hassan Shehata,kila mpenzi wa soka alimfahamu Waile Gomaa. Ilikuwa nyakati za Misri kunyanyasa mataifa mengine ndani ya bara la Afrika. Ilimchukua Kameruni miaka tisa kulipiza manyanyaso aliyopata toka kwa Misri ya kiumeni mwaka 2008 pale Ghana.
Ni Misri ambayo iliipa hasara CAF kuunda kombe lingine la Afcon baada ya kulibeba lile awali Mara nne Mfululizo. Mwaka 2006 fainali zilizoandaliwa na Misri wakikutana na Ivory coast ya Didier Drogba.
![]() |
KIKOSI CHA MISRI |
Fainali ile iliisha kwa matuta na wenyeji kutwa taji. Licha ya kuwa na kikosi ambacho kilikuwa na vijana taklibani Saba wakitoka kikosi cha Al Ahly ambayo ilikuwa moto wa kuotea mbali. Hapa nawazungumzia Mohammed Barakat,Saeed Moward,Essam El Hadary,Ahmed Hassan,Hossam Hassan,Mohammad Mido,Mohammed Aboutrika na wengineo. Ilikuwa ni kikosi kilichojaa vipaji kikiwa na hamasa kubwa kutoka kwa kocha mzawa Hassan Shehata kiliwafanya wapinzani wafikirie Mara mbili zaidi.
Ukuta ulioongozwa na Waile Gomaa ilikuwa kama unakutana na Rio Ferdinand wa nyakati za Vodafone na Manchester Utd yake. Beki mmoja chuma halafu bedui anacheza kibabe kiasi kwamba hupati nafasi ya hata kumiliki mpira kama mshambuliaji. Kwa lugha za sasa za mtaani unaweza kusema 'ana kuvugaa' kama ulivyo.
Si mnakumbuka Zengwe la Hassan Shehata na Mido katika Nusu fainali ya afcon iliyowalutanisha Misri na Senegal 2006. Ilikuwa Senegal ya vipaji haswa. Kuna nyakati unaweza kukaa na kutoa majibu kuwa soka la kipaji limeondoka miguuni mwa wachezaji tunao watazama sasa.
Lile zengwe ilikuwa baada ya Kufanyika mabadiliko yaliyomuingiza uwanjani Amri Zaki na kumtoa Mido. Mwarabu yule hakufurahishwa aligombana kwa maneno na kocha wake. Ajabu ya mwenyezi Mungu Zaki akafunga bao lililowapeleka fainali na kumwacha Mido akishindwa kushangilia huku Shehata akimwonyeshea kidole katika kichwa chake akimaanisha akili.
Licha matukio matamu yenye kusisimua kwa nyakati za zote za Ubabe wa Misri jambo pakee ilikuwa kizazi hicho hakikufanikiwa kufuzau kombe la dunia. Asikudanganye mtu hakuna raha kama kuimbiwa wimbo wa Taifa katika mashindano ya kombe la dunia.Misri walijaribu kuitafuta raha hiyo lakini wakaishia kuipata wanapocheza Afcon.
Mara ya mwisho kwa Misri kushiriki ko be la dunia ilikuwa mwaka 1990. Katika fainali zilizofanyika nchini Italia ikawa mwisho wao hadi sasa ambapo Mohammed Sarah anawapeleka Urusi mwakani. Ilikuwa nyakati za utawala wa Hosney Mubarak ndipo waMisri walipoimba kwa pamoja na wachezaji wao wimbo wa taifa pale Italia.
![]() |
MOHAMMED SALAH |
Wakiwa na nahodha na golikipa mkongwe Essam El Hadary Misri wanafuzu huku akiwa na wadogo zake ambao wametengeneza kikosi kilichoandika historia ya Misri tena. Matumaini ya kurudi katika Ubabe wa soka la Afrika yalianza kuonyesha matumaini katika michuano ya Afcon ya mwaka huu pale Gabon. Ukikitazama kikosi chao kina majina maarufu mawili yaani Mohammed Sarah na Mohammed Elneny katika dimba huku kaka yao El Hadary akihakikisha hakuna mpira unaompita na kutinga wavuni.
Juni 8 ilikuwa ya kihistoria kwao baada ya kufanikiwa kutinga faninali za kombe la dunia la mwakani. Magoli ya mawili ya Salah dhidi ya moja la Congo Brazzaville yaliwapaisha na kuwafikisha Urusi.
Jambo pekee katika Mchezo huo ni goli la dakika ya 90+3 lililofungwa kwa mkwaju wa penati na Salah ndilo lililofanya Misri yote ilindime kwa Shangwe vifijo na ndelemo. Ilikuwa zaidi ya sherehe kila mmoja alijikuta akifurahia matokeo ya Timu ya taifa licha ya tofauti za kisiasa zinazolitafuna taifa hilo kwa maandamano na mapigano ya wanajeshi wa serikali na Waasi.
Ukitaka kujua raha ya kuimbiwa wimbo wa taifa kombe la dunia muulize Serey Die nahodha wa sasa Ivory Coast. Alitoa mchozi wakati wimbo wa taifa unaendelea pale Brazil katika Mechi iliyowakitanisha Ivory Coast dhidi ya Japan. Mchezo ambao wapenzi wengi wa soka ilibidi wasubili hadi kumi za usiku kwa masaa ya Afrika mashariki kumwona Die akiangua kilio.
![]() |
WAEL GOMAA |
Nawaona wamisri wakiangua kilio zaidi ya kile walichoangua pale Misri baada yachezo dhidi ya Congo Brazzaville. Ilikuwa kama ndoto kwa mkongwe El Hadary kutimiza ndoto za kuisaidia Misri kufuzu kombe la dunia. Vilio vya uchungu walivyolia Wamisri pale Sudan mwaka 2009 vimegeuka vilio vya furaha kwa mwaka 2017. Kuna wakati mnaweza kupitia mitihani mikubwa lakini kumbe Mungu anakuwa na maksudi nanyi.
Ubabe wa Afcon kwa wamisri haukuwapeleka kombe la dunia lakini unyonge wao wa wakati huu unawafanya watimize ndoto na kwenda kuimba wimbo wao wa 'My country' katika ardhi ya Urusi. Utamu wa wimbo wa taifa mchezaji auimbe akiwa kombe la dunia.
Hakuna hoja yoyote ambayo inaweza kumfanya mtanzania akaona kama ni ya kujifunza Kwa kufuzu Kwa misri. Kama kufuzu Kwa Serengeti watanzania walichangiani je kwa Taifa Stars? Unajisikiaje Rais wa Misri kamwaga pesa Kwa vijana wake au unasikia Rais wa Panama kaamua siku moja kufanyika mpumziko ili kuwapongeza vijana wake.
Misri mmepata mlichokitafuta kwa miaka takribani ishirini na sita. Nendeni Urusi mkawakilishe Wafrika ambao watakuwa wanawachukulia kama timua yao.
0628994409
↧
TAKWIMU MUHIMU ZA WILAYA YA NYASA HADI OKTOBA 2017

2. Total Number of Households for Nyasa dc = 31,146
3. Total Female Population for Nyasa dc = 74,768.
4.Total Male Population for Nyasa dc = 71,392.
5. Total Population for Nyasa dc = 146,160.
6. Total Number of Secondary school = 14
7. Total Number of Primary School = 106
Total Number of Villages = 84
8. Total Number of Ward = 20
9. Total Number of Division = 3
CHANZO: Nyasa dc statistics
↧
↧
MAONI YA MHARIRI: KWA WILAYA YA NYASA DUNIA HAIJABADILIKA?
Majuzi nimeona picha ya mwanadada mashuhuri katika mtandao wa Instagram, Mange Kimambi akionyesha majengo ya hospitali ya Lumeme wilayani Nyasa ikiwa na mazingira mabaya ya kufanyia kazi na ukosefu wa huduma muhumu. Pamoja na jengo lenyewe kutokamilika, lakini limekuwa likitumika hivyo hivyo.
Kwangu mimi ile ilikuwa habari kubwa sana kwa wilaya yetu ya Nyasa. Kama mwanahabari naamini kuripotiwa matukio au masuala yasiyofaa ndani ya jamii ambayo haitoi habari za kutosha ni njia mojawapo kubwa ya kubadili mwenendo.
Je waanzilishi wa blogu ya JIMBO walikusudia tamasha au nini? BONYEZA HAPA KUTAZAMA. Kimsingi habari za Jimbo la Nyasa ni lazima zitolewe wala kwa wananchi. Pili inadhihirisha "kuamini" kuwa NYASA ni ileile ambayo inaishi pasipo kuwa na habari zozote. Mtazamo huo si sahihi ndio maana wahusika wanaona "bora liende tu" huku wakisahau na kushindwa "KUMUUZA" mbunge.
Kwangu mimi ile ilikuwa habari kubwa sana kwa wilaya yetu ya Nyasa. Kama mwanahabari naamini kuripotiwa matukio au masuala yasiyofaa ndani ya jamii ambayo haitoi habari za kutosha ni njia mojawapo kubwa ya kubadili mwenendo.
HAPA CHINI kuna Blogu ya JIMBO LA NYASA. Lakini habari za Jimbo husika ziliwekwa mara ya mwisho Januari mwaka huu. Nimejiuliza wasaidizi wa Mbunge wanafanya nini kama hawawezi kutoa taarifa za ofisi ya mbunge? Najiuliza hivi hatuoni umuhimu wa habari zetu zikiwa hadharani bila kujali mbaya au nzuri?
Je waanzilishi wa blogu ya JIMBO walikusudia tamasha au nini? BONYEZA HAPA KUTAZAMA. Kimsingi habari za Jimbo la Nyasa ni lazima zitolewe wala kwa wananchi. Pili inadhihirisha "kuamini" kuwa NYASA ni ileile ambayo inaishi pasipo kuwa na habari zozote. Mtazamo huo si sahihi ndio maana wahusika wanaona "bora liende tu" huku wakisahau na kushindwa "KUMUUZA" mbunge.
Nimejiuliza hadi leo hata kutengeneza ukurasa wa habari za mbunge kwenye mitandao hatuwezi kweli? Hivi mahusiano ya mbunge na wapigakura wake yana maana gani? Naandika hapa kwasababu naamini wapo wahusika wanaofikisha ujumbe. Ningependa kuwakumbusheni kuwa "kutomuuza mbunge" katika ulimwengu wa kidigitali ni uzembe. Labda tunaweza kutembelea wananchi kila kona ya jimbo, lakini tunapawa kuelewa kuwa taarifa za huko ziwekwe sehemu maalumu kutunza kumbukumbu sio mambo ya "MASJALA" tena (hizo ni zama za kale mawe).
Kwa heshima nawakumbusha wasaidizi wa mbunge, kutoitendea haki blogu, kutozungumzia hata utalii ambao ni chachu ya kukuza mzunguko wa fedha wilayani kwetu ni UDHAIFU unaopaswa kurekebishwa.
Ninawatakieni majukumu mema.
HABARI NI BIASHARA. HABARI NI UCHUMI.
MARKUS MPANGALA,
Oktoba 17/ 2017
Dar es salaam
MARKUS MPANGALA,
Oktoba 17/ 2017
Dar es salaam
↧
Article 1
KITABU: DOUDOU NA MAMA WAKWE ZAKE
MWANDISHI: WANG LIPING
MCHAMBUZI: KIZITO MPANGALA
Doudou Na Mama Wakwe Zake ni hadithi iliyoandikwa kwa lugha ya Kichina na mwandishi Wang Liping na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na wakalimani Chen Lianying na Han Mei. Kitabu hiki kina jumla ya kurasa 261 na kimegawanyika katika sehemu 24 za masimulizi yenye mtiririko mzuri ambapo sehemu inayofuata inategemea mhimili kutoka sehemu iliyopita. Kimechachapishwa na Zhenjiang Literature and Art Publishing House kikiwa katika lugha ya kichina na baada ya kutafsiriwa kwa Kiswahili kimechapishwa na Mkuki Na Nyota jijini Dar es Salaam Tanzania na kupewa namba za usajili (ISBN) 978 – 9987 – 08 – 284 – 1. Shukrani kubwa ziende kwa wakalimani Chen Lianying na Han Mei kwa kutangaza lugha ya Kiswahili.
Ni hadithi inayofahamisha maisha ya kawaida ya Wachina lakini mafundisho yake yanafaa kwa kila mmoja wetu duniani. Hadithi hii kwa mara ya kwanza iliingia nchini Tanzania ikiwa kama mlolongo wa tamthiliya ambapo ilikuwa imefanyiwa marekebisho ambayo yalifanya mazungumzo ya wahusika yasikike kwa Kiswahili. Ilikuwa ikionyeshwa na shirika la habari la taifa (TBC) mwaka 2011.
Msichana Mao Doudou alikumbwa na mkasa wa kuachwa na mpenzi wake ambaye alikuwa mpenda pesa kuliko upendo kwa mwenzi wake. Katika hali kama hii maishani ni wazi kuwa ndoa ya aina hii haiwezi kusonga mbele endapo itatanguliza pesa mbele kuliko upendo unaostahili miongoni mwao. Miaka ya sasa ndoa nyingi zinakumbwa na tatizo hili ambalo huanza mwanzoni tu mwa mahusiano. Na mtu anayejitutumua kujionyesha ana pesa sana mbele ya mpenzi wake hakika huyo ni masikini wa fikra!
Tafuta mpenzi anayekufaa lakini usitume watu wakutafutie kisha wewe ukubaliane naye bila hata kuelewana kwa kina. Jambo hili ndilo liliomgharimu kijana Mao Feng na kupelekea kuachana na mpenzi huyo siku mbili tu baada ya harusi kufanyika. Mchakato wa kutafuta mchumba nchini China unafanywa na makampuni rasmi ambayo hukutafutia mchumba kwa kuilipa kampuni hiyo na kisha kujaza fomu maalumu. hiyo ni biashara ya kipekee sana ambayo huifaidisha serikali kwa kodi. Hivyo basi, mchumba tafuta mwenyewe, usijiiunize kwenye matatizo yasiyo ya lazima.
Tafuta mpenzi anayekufaa lakini usitume watu wakutafutie kisha wewe ukubaliane naye bila hata kuelewana kwa kina. Jambo hili ndilo liliomgharimu kijana Mao Feng na kupelekea kuachana na mpenzi huyo siku mbili tu baada ya harusi kufanyika. Mchakato wa kutafuta mchumba nchini China unafanywa na makampuni rasmi ambayo hukutafutia mchumba kwa kuilipa kampuni hiyo na kisha kujaza fomu maalumu. hiyo ni biashara ya kipekee sana ambayo huifaidisha serikali kwa kodi. Hivyo basi, mchumba tafuta mwenyewe, usijiiunize kwenye matatizo yasiyo ya lazima.
Katika jamii zetu tumeona au tumefikwa na hali ya kuishi na mzazi wa kambo, hii ni kutokana na sababu mbalimbali ambazo zinakuwa nje ya uwezo wetu kuzitatua. Mao Doudou baadae anapata mume ambaye ni Yu Wei na kuishi pamoja kwa misukosuko kutoka kwa mama wakwe zake. Lakini je, kwa nini MAMA WAKWE NA SIYO MAMA MKWE? Imezoeleka kuwa mama mkwe ni mmoja tu. Lakini hilo ni mtihani mkubwa sana endapo baba na mama wakaachana na kisha kuoa au kuolewa tena, kwa hali hii itakuwa ni MAMA WAKWE na siyo MAMA MKWE tena, vile vile ni BABA WAKWE na siyo BABA MKWE tena!
Katika hao mama wakwe, yupo mama mzazi wa kijana wa kiume ambaye anaishi na baba wa kambo pia yupo mama wa kambo wa kijana wa kiumbe ambaye anaishi na baba yako mzazi, hapo ndipo ugomvi unajitokeza kila mmoja anadai umpelekee mkwe. Ugomvi wa ndoa wa wazazi hakika mtoto usiuingilie, kwani Wahenga wa Kiswahili husema “wagombanao ndio wapatanao”. Ni vitendo vya aibu kugombana ovyo katika familia ambayo imekuwa na msingi thabiti tangu awali. Lakini kwa uvumilivu na busara kama alizozionyesha msichana Mao Doudou ushindi unapatikana kwa kishindo! Msichana Mao Doudou ni mfano wa kuigwa katika hadithi ya kitabu hiki.
Mapenzi ni matamu sana ikiwa huna ujeuri kwa mwenzako na yeye hana ujeuri kwako wewe! Kwa mahabuba yenye raha na amani mmoja wenu anaweza akakuambia ametembea duaniani kote kutafuta mpenzi lakini hajaona mpenzi mzuri kama wewe hapo mlipo! Safi kabisa. Hapa tumkumbuke nguli wa fasihi ya Kimombo bwana William Shakespeare katika mashairi yake aliposema kuwa kwenye mapenzi kunahitajika aina fualni ya uwongo ili umuweke mpenzi wako kwenye mstari ulionyoka na asitoke! Vitendo vya kudanganyana kiholela katika mapenzi ni ujinga. Hilo lilimkumba Mao Feng ambaye ni mtaalamu wa kuwabwaga wasichana hao akishakamilisha dhamira yake. Lakini wakati ulipofika wa kuachwa yeye aliona dunia ipo kichwani mwake ameibeba! Kwa hiyo, tujifunze na tuwe wa kweli. Hapa namkumbuka afande Issa Mnyongo alipotuasa kwa kusema “vijana kuweni wa kweli”
Umaarufu ni jambo la kujivunia kwa wapenda umaarufu na kujihisi kuwa ulimwengu mzima unawatazama. Mtu yeyote aliye maarufu kwa jambo lolote, tafadhali chunga sana umaarufu wako kwa kuwa kuna wakati umaarufu huo unaweza kuwa UMMA-HARUFU. Kijana Mao Feng kwa umaarufu wake aliweza kuwahadaa wanawake na kuwa mlevi kupindikia jambo liliomfanya aingie kwenye ndoa na mtu aliyemzidi umri kwa kiasi kikubwa na ndoa ikayeyuka siku mbili tu baada ya harusi. Makinika na fundisho linalotoka hapa.
Yeyote anayeitwa mama mkwe basi azingatie kwa nini anaitwa mama mkwe. Mama mkwe ni kiongozi, ni mzazi, ni mlezi, ni mshauri, ni mwalimu na kadhalika. Mama mkwe anayefikiri kwamba fedha ndio msingi wa upendo kwa watoto wake kuingia kwenye ndoa basi huyo hana sifa hizi zilizotajwa isipokuwa tu yeye takuwa ni mlanguzi, tapeli, mfitini, mchonganishi, mchochezi, mjanja, mwongo, mwenye chuki na kadhalika. Mao Doudou ni binti anayempinga mama yake hadharani kwamba fedha siyo msingi wa upendo kwa mume wake, Mao Doudou anasema (akiwa amekasirika); “mama sipendi useme hivyo! Ni kwa nini kina mama wengi wako hivyo, wao wanachoangalia ni pesa tu” Uk. 36. Makinika na fundisho linalopatikana hapa.
Mama mkwe mwenye nia njema na watoto wake walioingia katika maisha ya ndoa ni mfariji, ni mwalimu, ni kiongozi, ni mlezi, ni mzazi, ni mshauri, ni mwenye amani ya nafsi na kadhalika. Pongezi hizi apate mama yake mzazi Mao Doudou baada ya kukosolewa na binti yake huyo kuhusu mawazo yake katika fedha. Mama anabadili msimamo na kumfariji binti yake kwa moyo wenye faraja kwamba wanaweza kuishi kwa kuvumiliana bila hata fedha ingawa kuna wakati watahityaji fedha kwa matumizi mbalimbali. Mama anasema; “Haya, kama unaweza kuvumilia maisha ya kawaida yasiyo na fedha nyingi mimi siwezi kupinga”. Hapa mama amejitambua kwa kiasi kikubwa sana, anapaswa kumfariji mtoto na siyo kumjaza falsafa za maisha ya ndoa bila fedha hayaendi, hii si kweli.
Kila mmoja anapenda kupendwa na mtu wa jinsia tofauti kwa namna ya pekee yenye ukaribu wa pekee na kwa hali pekee. Hilo ni juio la kila binadamu ingawa wapo binadamu wenye umri mdogo ambao wanakua na baadae watatambua hilo. Hata mimi nahitaji kupendwa na mtu wa jinsia tofauti kwa namna ya pekee! Ndio ubinadamu huo. Tuwape pole wale wote waliopoteza wenzi wao kwa namna mbalimbali. Hali hii inaweza kukufanya uchanganyikiwe kwa wakati fulani. Dada Yu Hao katika kitabu hiki alipoteza mume wake katika ajali ya gari siku mbili tu baada ya harusi, hali hii imemsababishia aishi kwa mfadhaiko kwa muda mrefu na hivyo kupata matatizo ya akili. Poleni nyote mliokumbwa na matatizo kama hayo. Jamani mapenzi matamu!
Kijana wa kiume, kwa kuwa name ni wa kiume kama wewe wa kiume usomaye hapa, basi makinika na funzo hili alilolionyesha kijana Yu Wei kwa kujitambua kwa umakini mkubwa. Yu Wei alijiweka wazi kwa mpenzi wake Mao Doudou aliyempenda maishani. Hakumuahidi magari, fedha, majumba na kadhalika. Hii ilimfanya akubalike zaidi na familia ya Mao Doudou kwa uwazi wake. Hivyo basi, kijana mwenzangu wa kiume makinika na fundisho hili. Kuwa muwazi. Tabia ya kudanganya kwamba una magari, fedha nyingi, maduka makubwa, majumba makubwa na kadhalika itatupeleka pabaya katika maisha yetu. Uchunguzi ukifanyika utaona kwamba anayeahidi au kutamba hivyo hata mkokoteni wa kuvuta na punda hana! Kama kweli unavyo vitu hivyo, basi usivipe kipaumbele kwa mpenzi wako!
Kusema kweli kuishi pamoja na mama mkwe mtukutu ni taabu zaidi kuliko kufanya kazi nyingine, mbali na kuwa mtiifu na mvumilivu wakati wa kukosolewa na mama mkwe wa aina hii, ni lazima kuwa na uwezo mwingine wa kukabiliana naye! Mama mkwe wa namna hii ni hatari zaidi kwa wanawe. Mama mkwe sikiliza kwa makini, hata kama mkweo amekosea jambo au kama humpendi jitahidi kuwa naye karibu kwa amani na ujitathmini kwa nini humpendi. Katika kitabu hiki tunaona jinsi Cao Xinmei anavyomchukia Mao Doudou lakini Mao Doudou anajitahidi kumvumilia. Kwa hiyo, fundisho lake ni kwamba mama mkwe unapaswa kuwa mstahimilivu na mwenye busara unapokuwa na mkweo. Mkweo ni binadamu kama wewe na ukumbuke kuwa na wewe ulikuwa mkwe kwa wazazi wa mume wako. Kama ulitendewa jambo baya huko basi jitahidi sana usihamishie kisasi chake kwa mkwe uliyenaye hapo!
Wakati wa dhiki udhati ndio huonekana kwa kiasi kikubwa sana. Kumpenda ndugu, jamaa, au rafiki yako kwa dhati kusionekane wakati wa dhiki tu bali ni wakati wote. Ikiwa kama mwadhani ya kwamba kumpenda ndugu, jamaa, na rafiki zenu kunahitaji fedha za kigeni basi jueni ya kwamba mnakosea. Msijivike mavazi yanayosimulia fedha ili kuonyesha upendo kwa ndugu, jamaa, au rafiki zenu. Upendo siyo fedha na fedha siyo upendo! Makinika na falsafa hii ndogo yenye manufaa makubwa.
Wifi ni mtu mzuri sana katika familia na anao umuhimu wake kwa mkeo wewe kijana wa kiume. Wifi anaweza kumchombeza mke wako ili amakinike zaidi kwa mahabuba mazito kwako, anaweza kumchombeza mkeo ili ajihisi kuwa bila wewe mambo yake yote yanaharibika, anaweza kumchombeza ili ajisikie kuwa yupo kwenye ghala salama lisilo na wadudu wanaoharibu nafaka, anaweza kumchombeza ili ajihisi kuwa wewe ni jemedari wa majukumu yanayokupasa kwake bila kuchenga na ajihisi kuwa hakuja kwako kula na kunywa bali alifuata mapenzi ili kulainisha moyo wake! Haya ni matunda ya wifi bora. Lakini endapo wifi anakuwa kinyume na chombezo kama hizo basi kila kukicha anamsimanga mkeo, anamkejeli, anamtukana, anampa kila neno la kumkatihsa tama. Kwa hakika wifi kama huyu ni bomu kubwa sana. Hivyo basi, ninyi mawifi kaeni na mawifi zenu vizuri ili muishi kwa amani na furaha.
Pan Meili ni msichana anayetambua thamani ya kuonekana kwa asili na siyo kujiweka nakshi mbalimbali za urembo mpaka kujiondolea asili yake. Hivyo basi kina dada mnapaswa kujali asili ya mionekano yenu ili mjiepushe na magonjwa ya ngozi yanayotokana na matumizi yasiyo ya lazima ya vipodozi vikali au vilivyokwisha muda wake wa kutumiwa.
Mafunzo yanayopatikana katika kitabu hiki yanafaa sana katika maisha yetu. Akina dada igeni mfano wa dada Mao Doudou katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ya ndoa. Msidanganyike kusema kuwa maisha ya ndoa bila fedha nyingi hayaendi. Nanyi mama wakwe popote mlipo msiwatendee wakwe zenu vibaya, kama ni kuwaonya basi muwaonye kwa nidhamu na heshima ili muishi kwa amani na furaha daima.
Ushauri wangu kwa waandaaji wa tamthiliya ya SIRI ZA FAMILIA ambayo hurushwa na Clouds Media, ni kwamba wanaweza kuiweka tamthiliya hiyo katika kitabu itakapomalizika ili kutunza kumbukumbu kwa miaka ijayo kama mwandishi Wang Liping alivyofanikisha hilo katika maonyesho ya MAO DOUDOU NA MAMA WAKWE ZAKE.
© Kizito Mpangala
0692 555 874, 0743 369 108
↧
SABUNI ZA MAWESE MWANGA, KIGOMA
↧