Quantcast
Channel: KARIBUNI NYASA
Viewing all 535 articles
Browse latest View live

STEPHEN HAWKING: MWANAFIZIKIA MGONJWA WA MUDA MREFU.

$
0
0
NA KIZITO MPANGALA

STEPHEN HAWKING alizaliwa mwaka 1942 jijini Oxford nchini Uingereza kwa wazazi Frank Hawking na Isobel Hawking. Japokuwa familia yake ilikuwa na mtikisiko kifedha lakini wazazi wake walijitahidi kujiendeleza kielimu katika chuo kikuu cha Oxford. Baba yake alisoma udakitari wa dawa na mama yake alisoma Falsafa, Sayansi ya Siasa, na Uchumi katika chuo hicho.

Baba yake na mama yake walikutana kwa mara ya kwanza muda mfupi tu bada ya kuanza kwa vita ya pili ya dunia katika Taasisi ya Utafiti wa Dawa ambapo baba yake alikuwa mtafiti  na mama yake alikuwa katibu wa taasisi hiyo. Ndipo mapenzi yao yalipoanza na walibahatika kupata mtoto wa kiume ambaye ni Stephen Hawking.

Familiya ya Hawking ilisifika kwa kuwa na kiwango kizuri cha upeo wa akili tangu wazazi hadi watoto wao. Muda mwingi walipokuwa nyumbani kulikuwa na ukimya ikidhaniwa kuwa wanasafiri mara kwa mara lakini sivyo! Ukimya uliotawala ndani ya familia hiyo ulitokana na wazazi kuwazoesha watoto kujisomea vitabu jambp ambalo walilipenda na ndipo Stephen Hawking alipodhihirisha kiwango chake katika upeo wa akili. Walikuwa wakiishi kwenye nyumba kuu kuu iliyokuwa na maktaba ya familia ndani.

Stephen Hawking alianza shule katika shule ya Byron mtaa wa Highgate jijini London. Baadae alilalamikia shule hiyo kutokana na mfumo wake uliokuwa ukitumika kufundishia, jambo ambalo lilinampa ugumu katika kujifunza zaidi. Wazazi wake walipohamia katika mji wa Mt. Albans, Stephen alijiunga na shule ya upili ya wasichana ya Mt. Albans mjini hapo kwa muda mfupi na baadae akahamishiwa katika shule ya Radlett katika mji mdogo wa Hertfordshire.

Wazazi wake waliipa elimu kipaumbele kwa kiasi kikubwa na kuwahimiza wajisomee vitabu vilivyokuwepo katika maktaba ya familia ndani ya nyumba yao.  Baba yake alitamani Stephen akasome katika shule binafsi ya Westminster lakini kwa bahati mbaya siku ya kufanya mtihani wa kujiunga na shule hiyo Stephen alishikwa na homa kali lakini pia wazazi wake hawakuweza kulipa ada katika shule hiyo iliyokuwa ikitoza kiasi kikubwa cha fedha wakati huo, hivyo Stephen alibaki katika shule aliyokuwepo.


Stephen Hawking alijizolea marafiki wengi katika shule aliyokuwepo kutokana na kiwango chake cha upeo wa akili katika masomo, hivyo hata yeye mwenyewe alifurani kuwa na marafiki na kucheza nao pamoja. Wakiwa shuleni walifundishwa stadi za kazi na mambo mengine yahusuyo maisha kwa ujumla. Walijifunza kutengeneza maboti na vielelezo mbalimbali vya ndege.

Mwaka 1958wakisaidiana na mwalimu wao wa Hisabati bwana Dikran Tahta walitengeneza kompyuta  wakitumia vifaa vya saa kubwa ya kielektroniki iliyokuwa mbovu, pia walitengeneza simu za mezani kwa kutumia vifaa vya vyombo vibovu vya kielektroniki.

Stephen Hawking alipewa jina la utani shuleni ambapo alikuwa akiitwa “Einstein”, pia alikuwa na udhaifu katika maendeleo yake kitaaluma lakini alijitathmini kwa msaada wa mwalimu wake wa Hisabati bwana Dikran Tahta na kuamua kujikita katika masomo ya sayansi, akawa anaimarika kitaaluma. Aliweka bidii zaidi katika Hisabati na alipofika chuo kikuu alisoma Hisabati zaidi.

Baba yake alimhimiza asome udakitari wa dawa (Doctor of Medicine) akimuambia kuwa kuna ajira chache sana ambazo zinahitaji wajuzi wa Hisabati, hivyo alimsihi aachane na Hisabati ili asome udakitari wa dawa. Alimsihi pia ajiunge na chuo kikuu  cha Oxford. Baada ya kujiunga ilitokea kwamba ni ngumu kusoma hisabati wakati ule kutokana na uhaba wa walimu ndipo Stephen akachagua kusoma Fizikia na Kemia. Mkuu wa chuo alimsihi Stephen avute subira hadi mwaka wa masomo utakaofuata kwamba kutakuwa na walimu wa kutosha lakini Stephen alifadhiliwa.

Alianza masomo mwezi wa kumi mwaka 1959 katika chuo kikuu cha Oxford akiwa na miaka 17. Miezi 18 tangu aanze masomo katika chuo hicho alihisi kuchanganyikiwa kitaaluma kutokana na hulka yake ya kujilinganisha na wengine kitaaluma hivyo alijiona yeye si kitu na kwamba hafai lolote kusoma chuo kikuu, lakini mwalimu wake wa Fizikia katika chuo hicho bwana Robert Berman alimtibu kisaikolojia kwa kumuambia “ninapofundisha ninataka kukuonyesha kwamba kuna kitu fulani cha pekee inabidi kifanywe, na usikifanye kwa kuangalia watu wengine walifanyaje au wanafanyaje”. Kutokana na maneno hayo, Stephen alionyesha mabadiliko makubwa kitaaluma alipoanza mwaka wa pili wa masomo na mpaka alipofika mwaka wa tatu. Kadiri ya mwalimu wake huyo alisema kwamba Stephen likuwa kijana mwerevu kati ya waerevu.

Alipenda kujisomea hadithi za kisayansi na kujihusisha na muziki. Pia alikuwa mmoja kati ya washiriki wa masindano ya kuendesha maboti katika mashindano yaliyokuwa yakifanyika chuoni hapo.

Stephen alisema kwamba katika maisha yake ya kitaaluma chuoni Oxford miaka mitatu alitumia masaa 1000 tu kujisomea katika jumla ya miaka hiyo mitatu, hivyo mtihani wa mwisho wa kumaliza mafunzo ulimpa changamoto na akaamua kujibu maswali machache tu ya kipengele kimoja cha Fizikia ya Nadharia (Theoretical Physics) akiwa na lengo la kujiendeleza na masomo ya Cosmolojia katika chuo kikuu cha Cambridge ambapo alihitajika kupata ufaulu wa daraja la kwanza. Kutokana na mfadhaiko, alilala usingizi hafifu sana siku moja kabla ya kufanya mtihani wa mwisho, hivyo akapata alama zilizopungua kidogo kupata daraja la kwanza na kulazimika kufanya mtihani wa marudio uliojulikana kama “Viva” ili kusahihisha matokeo.

Stephen Hawking alijihisi ya kwamba ni mwanafunzi mvivu na mgumu kuelewa masomo kwa ufasaha. Alipoulizwa kuhusu matokeo yake ya awali alijibu hivi “mkinipa daraja la kwanza nitakwenda Cambridge, mkinipa daraja la pili nitabaki hapa Oxford, natumaini mtanipa daraja la kwanza”. Walimu wake walitambua kipawa chake cha upeo wa akili na walikuwa wakimpa uangalizi mkubwa sana bila kumuambia yeye mwenyewe. Baadae akapewa daraja la kwanza.

Alikwenda nchini Iran na rafiki zake kwa ajili ya mapumziko baada ya kumaliza chuo huko Oxford, na aliporudi Uingereza alianza kufanya kazi zilizohusu taaluma yake katika Ukumbi wa Kisayansi wa Trinity mjini Cambridge mnamo mwaka 1962.

Alipoanza masomo ya shahada ya uzamivu alihisi kwamba amekosea njia katika taaluma. Alipata changamoto kubwa  na hivyo kukata tamaa ya kuendelea na masomo ya Cosmolojia. Pia alihisi hataweza kujiendeleza na hisabati tena kutokana na changamoto alizopata. Lakini alihimili changamoto hizo hadi mwisho wa masomo yake.

Muda mfupi baadae alipata homa na hivyo kufanyiwa upasuaji na akabainika kuwa anasumbuliwa na homa iliyoiangamiza “motor nuerone” na kumfanya apooze mwili. Dakitari alimshauri aendelee na masomo japokuwa mwili wake ulikuwa ukiendelea kupooza taratibu, hivyo hakuweza kutembea na akawa anatumia baiskeli mpaka hivi sasa, vilevile alipata ugumu wa kupangilia matamshi yake kwa usahihi kutokana na kupooza kuanzia shingoni na kuathiriwa katika matamshi wakati anapozungumza.

Alirudi masomoni katika hali hiyo na kwa mshangao mkubwa aliboreka zaidi katika taaluma na pia aliweza kuboresha matamshi yake kwa msaada wa kitabibu.

Alpoanza kuwa mkufunzi alikuta mjadala mzito uliokuwa ukijadiliwa na wakufunzi wenzake wa Cosmolojia kuhusu jinsi ulimwengu ulivyotokea. Alikuwa mkufunzi hodari licha ya kuwa maisha yake kuwa katika baiskeli muda mwingi huku shingo ikiwa imekwenda upande kama anavyonekana pichani kutokana na kupooza mwili. Mwka 1965 aliandika insha yake mashuhuri kuhusu mjadala uliokuwa ukijadiliwa kuhusu jinsi ulimwengu ulivyotokea. Aliandika akiwa bado kijana lakini akiketi kwenye baiskeli muda mwingi.

Mwaka 1966 alitunukiwa shahada ya uzamivu katika Hisabati Tumizi (Applied Mathematics) na Fizikia ya Nadharia (Theoretical Physics) na alijikita zaidi katika Cosmolojia (Cosmology). Na baadae kazi yake aliyoandika kutokana na utafiti alioufanya (licha ya kuwa na kilema kama anavyoonekana pichani) ya “Singularities and the Geometry of Space – Time” iliheshimiwa na hivyo akashinda tuzo ya Adams katika sayansi.

Mwaka 1970 aliteuliwa kuwa profesa wa hisabati katika chuo kikuu cha Cambridge. Katika maisha yake kitaaluma amejikita zaidi katika sayansi ya ulimwengu (The science of Universe). Kadiri muda ulivyosonga alizidi kudhoofika na kulazimia kupata matibabu mara kwa mara akiwa nyumbani kwake.

Mwaka 1982 alihudhuria mkutano huko Vatican kuhusu ulimwengu ndipo alipotoa msimamo wake hadharani na kusema “hakuna mwanzo, hakuna mwisho, na hakuna mipaka katika ulimwengu”, tukumbuke kuwa ulimwengu una maana pan asana kisayansi, ulimwengu ni zaidi ya ukubwa wa dunia hii au sayari yoyote kwa kuwa ulimwengu ni jumla ya sayari zote na vyote vilivyomo katika anga. Stephen Hawking ansema kwamba nadharia ya Biblia inayosema kwamba kulikuwa na mwanzo wa ulimwengu siyo ya kweli na haina mashiko, hivyo hakuna mwanzo, mwisho, wala mipaka katika ulimwengu.

Pamoja na kuwa kilema na kuwa na tatizo la kufanya mawasiliano kwa usahihi, Stephen Hawking ni mwanafizikia aliyeweka kando ukilema wake na kujikita katika taaluma yake ya Fizikia. Hali ya kuwa kilema ilimpelekea kuachana na mkewe licha ya kuwa na watoto aliopata na mkewe huyo. Alitumia muda mwingi kufikiri masuala ya sayansi na kuweza kuandika vitabu vingi kuhusu Cosmolojia ambavyo vinatumika katika vyuo mbalimbali duniani.

Stephen Hawking amesafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani kwa shughuli binafsi na kikazi. Stephen Hawking amekuwa gwiji wa  Cosmolojia na kusikika masikioni mwa watu wengi duniani kwa umahiri wake katika fizikia na hisabati licha ya kuwa kilema kwa muda mrefu jambo ambalo lilimpelekea kuwa na baiskeli maalumu iliyounganishwa na kompyuta ambayo inamsaidia katika mazungumzo na mambo mengine katika maisha yake.

Stephen Hawking amejitokeza mara nyingi katika mijadala mingi kuhusu Cosmolojia jambo ambalo alisema ndilo la maisha yake yote. Amekuwa mtu wa kutumainiwa katika vyuo mbalimbali duniani kwa taaluma ya Cosmolojia.
Hakika kilema si ugonjwa! Leo Stephen Hawking ambaye bado anatumia pumzi ya bure aliyojaliwa na Mungu ameshinda nishani zaidi ya 10 kwa muda wote wa maisha yake aliyoyaweka katika sayansi. Hawking ansema kwamba kila mmoja anao uwezo wa kujifunza anachokipenda.

Amekuwa na afya dhaifu kwa muonekano wa kawaida mwilini lakini ana afya imara sana katika ubongo wake. Muda mwingi wakati wa mapumziko hutumia kuzungumza na binti yake Lucy Hawking na ambaye humuwakilisha katika upokeaji wa zawadi kwenye matamasha mbalimbali anayoalikwa. Bega lake la kulia ndilo lililoathirika zaidi pamoja na miguu, lakini kwa hakika Mungu ni mkubwa, ubongo wa Stephen Hawking una afya imara sana ya maarifa na mambo mbalimbali maishani. Hivi sasa vyuo vingi vinafaidi kazi zake kuhusu Cosmolojia ambapo hutumika katika mafunzo ya kupata shahada ya uzamivu katika sayansi ya anga, na maisha yake muda mwingi ni juu ya baiskeli yake maalumu kama anavyoonekana pichani. Yuko hai.

© Kizito Mpangala 
0692 555 874,   0743 369 108.  

FUAMBAI SIA AHMADU: MWANAMKE ANAYETETEA UKEKETAJI AFRIKA.

$
0
0
Na KIZITO MPANGALA

FUNAMBAI SIA AHMADU alizaliwa mwaka 1969 nchini Sierra Leone katika jamii ya kabila la Kono kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Alifanya kazi na UNICEF nchini Gambia. Fuambai Sia Ahmadu alipata shahada ya uzamili katika chuo cha masuala ya Uchumi jijini London Uingereza akiwa kama mataalamu wa Anthropojia. Baadae aliendelea na masomo zaidi katika chuo kikuu cha Chicago na kupata shahada ya uazmivu.

Anafahamika zaidi kwa utetezi wake wa ukeketaji hasa akifikiria zaidi kutoka katika jamii ya kabila la Kono ambapo yeye mwenyewe amekeketwa na anafurahia jambo hilo. Anasema masuala mengi kuhusu ukeketaji hayajaeleweka kwa ufasaha miongoni mwa watu wengi duniani.   

Katika kitabu cha “AFRICAN STUDIES” chenye masuala mbalimbali kuhusu jamii mbalimbali za Afrika lipo swali linalouliza hivi ‘je, ukeketaji ukubaliwe na kuendelezwa kama jambo bora la kimila? Watu kadhaa walitoa majibu kuhusu swali hilo kulingana na mtazamo wao wanavyoona. Fuambai Ahmadu alikubali katika insha yake maarufu ya “Rites And Wrongs” kwa mujibu wa kitabu cha “FEMALE CIRCUMCISION AFRICA: CULTURE, CONTROVERSY AND CHANGE” kilichoandikwa na Lynne Rainer, 2001. 

Kabla ya jibu la Fuambai Ahmadu, mwanadada Liz Creel Et Al alipinga suala la ukeketaji. Jibu la mwanadada huyu ni kwa mujibu wa ripoti ya “ABANDONING FEMALE GENITAL CUTTING: PREVALENCE, ATTITUDES AND EFFORTS TO END THE PRACITCE” iliyoandikwa na taasisi ya Population Reference Bureau, Agosti 2001 Marekani ambapo Liz anasema serikali za Afrika zipitishe sheria kali inayobana wakeketaji.

Bi Fuambai Ahmadu anatetea ukeketaji na kukosoa baadhi ya waandishi hasa wasio wa Afrika na wa Afrika pia wanaohimiza ukeketaji ukomeshwe na kuwataka wanawake na wasichana wa Afrika wawe na muonekano wa Kimagharibi.

Bi Fuanmbai Ahmadu anasema na anaamini kwamba ukeketaji haupaswi kuzuiliwa kwa kuwa unaambatana na mila zingine kulingana na jamii husika inayotekeleza zoezi la ukeketaji ambazo zinampa mkeketwaji kuwa mwanamke anayekubalika zaidi na jamii yake katika mapokeo ya kihistoriaya jamii hiyo. Yeye ni mmojawapo kati ya waliokeketwa katika jamii ya kabila la Kono nchini Sierra Leone. 

Bi Fuambai Ahmadu anasema anachukizwa na wale wanaohubiri ubaya wa ukeketaji kwamba hawajaona na hawajui jema lililomo kwenye shughulihiyona hivyo hulinganisha na maeneo wanayoishi wao ambayo ukeketaji haufanyiki. 

Katika makala yake ndefu ya “RITES AND WRONGS: EXCSION AND POWER AMONG KONO WOMEN OF SIERRA LEONE” amezungumza mengi kuhusu ukeketaji. Katika makala hayo, anazishauri serikali za Afrika siruhusu ukeketaji ufanyike na ziborshe mazingira ya kufanyia ukeketaji yawe ya kitabibu zaidi yaani ukeketaji ufanyike hospitalini badala yakienyeji. Ansema “the issue of female initiation and circumcision is of significant intellectual and personal interest to me” yaani “suala la uhamasishaji na ukeketaji kwa wanawake ni jambo la muhimu la kiakili na matakwa binafsi kwangu”

Bi Fuambai Ahmadu anasema yeye kama mtaalamu wa Anthropolojia kama walivyo Wanaanthroplojia wengine anavutiwa sana na masuala ya kijamii, kidini, kiitikadi, na kimila katika jamii nyingi na zaidi ni katika maeneo anayoyajua zaidi. Andai zaidi kwamba suala ukeketaji liboreshwe mazingirayake na hivyo liwe la kitabibu zaidi ili kuondokana na athari ndogondogo.
Ni Fuambai anasema utafiti mwingi kuhusu ukeketaji unafanywa na wale wasioishi Afrika na pengine hawana asili ya Afrika au wale wanaoishi Afrika na wenye asili ya Afrika lakini hawaishi katika jamii ambazo zinafanya ukeketaji. Ansema wanawake wengi wanaoandika habari kuhusu madhara ua ukeketaji hwajaishi katika jamii zinazoheshimu ukeketaji. Anaongeza kusema kwamba ukeketaji hauna madhara, kinachotakiwa sasa ni kuboresha mazingira ya kufanyia shughuli hiyo.

Bi Fuambai ansema kuwa wanaopinga ukeketaji wameathiriwa na hoja za kizungu na hisia hasi dhidi ya ukeketaji. Anasema wengi wanaokosoa ukeketaji wanajitetea kwa hoja za kimagharibi dhidi ya miili ya wanawake kwa kigezo cha hoja kwamba sehemu inayoondolewa katika shughuli ya ukeketaji ndiyo msingi mkuu msisimko wa hisia za mwanamke katika  tendo la ndoa. Yeye anapinga vigezo hivyo vyote na kusema kwamba hata sehemu hiyo ikiondolewa mwanamke atabaki na msisimko wake kamakawaida.Na vile vile inasaidia kumfanya mwanamke awe mwaminifu zaidi katika ndoa yakena kuepukana na tama ya kunuia kufuata wanaumewengine.

Bi Fuambai Sia Ahmadu kwa sasa ana uraia wa Marekani. Anatoa msisitizo kwamba kutokana na madhara ya muda mfupi baada ya kukeketwa ni vema jambo hilo lifanyike hospitalini ili kuepuka madhara hayo kuwa makubwa.
Msomaji wa makala haya, umepata nyongeza ya maarifa kuhusu ukeketaji na jinsi Bi Fuambai anavyotetea suala hilo kwa nguvu. Huo ndio masimamo wake. Maoni yako ni muhimu sana kuhusiana na suala hili la ukeketaji hasa katika dunia ya leo ya sayansi na teknolojia kama ilivyoasisiwa rasmi mwezi Januari mwka 2000.

0692 555 874, 0743 369 108

MBUNGE WA CHEMBA AONDOA HOJA YA KUONGEZA MUDA WA UBUNGE

$
0
0
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MBUNGE  wa Chemba Juma Nkamia (CCM)amesema ameondoa kwa muda kusudio lake la kutaka kuwasilisha muswada binafsi wa mabadiliko ya Katiba unaohusu kuongeza ukomo wa Bunge. 
JUMA NKAMIA
Nkamia ambaye aliwasilisha kusudio hilo  katikati ya mwezi uliopita mjini Dodoma kwa mujibu wa kanuni ya 81(2) ya kanuni za Bunge toleo la 2016,kupitia barua yake aliyoisaini Septemba 12  iliyokuwa ikipendekeza kuongeza muda wa bunge kutoka miaka mitano hadi saba na kupunguza wa uongozi wa vijiji kutoka miaka mitano hadi minne.

Kupitia ujumbe mfupi aliouandika katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp,alisema ameamua kuondoa kusudio hilo  baada ya mashauriano  na maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

“Ndugu viongozi wenzangu naomba kuwataarifu kuwa baada ya mashauriano na maelekezo  ya viongozi wa juu wa chama(CCM) na hali ya kisiasa  katika nchi kadhaa za Afrika  Mashariki  nimelazimika kuondoa kwa muda hoja yangu binafsi ya ukomo wa Bunge niliyokusudia kuiwasilisha katika bunge lijalo,”aliandika Nkamia.

Mbali na andiko hilo gazeti hili pia lilimtafuta Nkamia kupitia simu yake ya kiganjani ili kumuuliza kama  na sababu nyingine zaidi ya alizozitaja kupitia ujumbe  huo mfupi na lini atakuwa teyari kuwasilisha tena muswada huo alisema.

“Naomba ibaki hivyo hivyo kama ilivyo kwenye meseji  sina cha kuongeza,kuhusu ni lini nitapeleka tena nayo subiri kwa sababu nimesema nimesitisha kwa muda maana yake nitawasilisha tena nitakapokuwa teyari,”alisema Nkamia.

Hoja ya  Nkamia ambayo ilianzia  katika Bunge lililopita ilikuw aikipingwa na wanazuoni pamoja na wanasiasa wakongwe akiwemo Spika Mstaafu wa Bunge Pius Msekwa.

Msekwa ambaye alikuwa akiongea na televisheni ya Azam  mwishoni wa wiki hii alisema  chama cha CCM hakiwezi kukubaliana na maoni au mpango wa kuongeza muda wa kiongozi yeyote kutoka kipindi cha miaka mitano kilichopo kikatiba kwa sasa.

Msekwa alisema kwa uzoefu wake bungeni tayari anaona kuna tafakari nyingi zilizofanywa kabla ya Taifa kuamua kipindi cha utawala kuwa miaka mitano na si vinginevyo.

Alisema hoja hiyo inabidi iangaliwe kwa umakini mkubwa kutokana na ukweli kuwa, iwapo kiongozi atakuwa mbaya, maisha yanaweza kuwa ya mateso kupitia kiongozi huyo na kuongeza kuwa hilo hata Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere aliliona hilo.

“Ni kwamba miaka kumi tu inatosha, ili kama mtu ni mbaya tuvumilie kwa hiyo miaka kumi, na siyo kwamba haikufikiriwa. .na sidhani kama CCM itakuwa na nafasi ya kujadili hilo kwa sasa” alisema Msekwa. Mbali na Msekwa wasomi wakiwemo Dk.Benson Bana nao walimpinga huku akisema kuwa lengo lake lilikuwa ni kujipendekeza kwa Rais Dk. John Magufuli ili ampe uwaziri.

UCHAMBUZI WA KITABU CHA UHAMASISHAJI

$
0
0
KITABU: ISHINDE TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO
MWANDISHI: JOEL NANAUKA
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA


JOEL NANAUKA ni miongoni mwa waandishi wazuri katika vitabu vya uhamasishaji na utambuzi. Kitabu chake cha “Ishinde Tabia ya Kughairisha Mambo” kimechapishwa na kampuni ya Benison Communication &Printing iliyopo Dar es salaam na kupewa nambari za usajili ISBN 978-9987-761-99-9.

Msingi wa kitabu hiki unaanza kupatikana katika utangulizi wake ambapo mwandishi anaandika, “Unakumbuka wakati watu wametangaziwa kujisajili kwaajili ya kupiga kura? Unakumbuka watu walivyotangaziwa kuhusu usajili wa vitambulisho vya utaifa? Ni siku gani watu walijaa zaidi? Bila shaka, utakumbuka ni siku ya mwisho hata kama waliliona tangazo. Kuna watu kila siku wanatuma maombi ya kazi siku ya mwisho hata kama waliliona tangazo hilo miezi miwili kabla. Kuna watu kila wakati watatuma ripoti yao siku ya mwisho, kuna watu kila wakati kazi waliyopewa kufanya wataiwasilisha dakika za mwisho” (uk.2).

Sura ya kwanza ya kitabu hiki inaeleza tabia za baadhi ya watu kupanga mipango fulani na kushindwa kutekeleza. Mathalani mtu anapanga kutekeleza jambo fulani lakini kabla hajaanza au akifika nusu ya jambo lenyewe anaahirisha. Mwandishi anatumia utafiti wa Profesa Joseph Ferrari ambaye aligundua kuwa takribani asilimia 20 ya watu duniani ni waahirishaji wakubwa wa mambo yao. 

Kwa mfano, mtu anataka kununua saruji kwaajili ya kujiandaa kwa ujenzi wa nyumba, pengine inahitajika mifuko 150, lakini yeye ananunua 50, na kuahirisha ujenzi kisha anasema ataanza mwaka mwingine. 

Mwandishi amebainisha taswira halisi katika maeneo ya kazi. Anasema wapo wafanyakazi ambao hawapendi kutekeleza kazi zao kwa wakati badala yake wanasubiri hadi dakika za mwisho ndipo waanze kuhaha huko na huko. Kimsingi tabia hizi zinazozungumzwa zinawagusa watu kila kaliba. Haijalishi umri wala nasaba au jinsia.

“Unaweza ukachukua daftari lako kuandika, ama ripoti yako ama hata kusoma kitabu, ukaamua kuwa unafanya unachotaka kwa nusu saa bila kuyumbishwa na kitu chochote, ghafla baada ya dakika 10 unajikuta nunashika simu na unasema ngoja niangalie meseji, kuja kushtuka unajikuta umeshatumia takribani nusu saa kuperuzi mitandao na hamu ya kuendelea na kazi uliyokuwa unaifanya inapotea kabisa. Ama wakati mwingine unasema ngoja niangalie TV kidogo kisha nitalala ama nitasoma kidogo, kuja kugundua unakuwa umeshafika saa 7 usiku na umeshindwa kuondoka kwneye TV yako. Ni kitu gani kinasababisha uamue jambo moja na kisha ujikute umefanya kitu tofauti,”(uk.9).

Katika muktadha huo mwandishi anakumbusha kuwa wapo watu wanaoishi kwa kuahirisha. Wengine ambao hadi wakumbushwe ndipo hutekeleza jambo fulani. Wapo watu ambao hawezi kujikita kwenye eneo husika. 

Tunaweza kutumia dhana ya “kutanga tanga kimawazo”. Kwamba anayetanga tanga kimawazo anakuwa na vitu vinavyovuruga zaidi utaratibu wa utendaji wa kazi. Hali ya kutanga tanga kimawazo huchochea uvivu na uzembe. 

Mathalani unaweza kuona mtu anajishughulisha kupika jikoni, kwakuwa anajua itachukua dakika takribani 5 au zaidi, anakwenda sebuleni kutazama TV au kukaa mbali na jikoni ili afanye kitu kingine kisichohusika na mapishi. Katika hali kama hiyo unaweza kushuhudia mtu huyo akikurupuka alikokaa na kukimbilia jikoni kutazama anachokipika baada ya kugundua kuwa ameunguza. Mara nyingi vitu vinavyosababisha hayo ni vile tunavyodhani ni vinatupatia raha na kadhalika.

Ili kubaini hilo mwandishi ameeleza tabia za watu mbalimbali na namna wanavyoweza kuahirisha mambo. Wengi wao hukosa nidhamu ya muda, wana mambo mengi yasiyokwisha (sababu ya kutotekeleza kwa wakati na kulimbikiza majukumu), wanatatizo la kulipua mambo, na wanakosa vipaumbele.

Sura ya pili anazungumzia tabia zingine zinazochochea kuahirisha mambo ni kutenda jambo katika dakika za mwisho ambayo huchochea presha kubwa. Pia watu wenye tabia hizo hawafanikiwi kwasababu wanaendeshwa na maoni ya watu. 

Anasema wapo watu ambao wanaogopa kulipia gharama za uamuzi wao hivyo wana tabia ya kuahirisha mambo. Ili kufahamu zaidi yaliyomo katika sura za tatu, nne na tano ni vema msomaji akitafuta kitabu hiki na kujipatia elimu.

Nihitimishe kwa kumkumbusha mwandishi juu ya matumizi sahihi ya maneno ya Kiswahili. Usahihi ni “Kuahirisha” si “kughairisha. Mwandishi wa habari na nguli wa Kiswahili, Amabilis Batamula, anasema “Naomba nisahihishwe kipengele cha lugha kama nakosea, maana na mimi kwa kupenda kuhariri nimeshajishtukia. Hilo neno kughairisha linatumikaje hapo? Ninavyofahamu mimi kuahirisha ndio ‘Procrastination’, kusogeza sogeza, na kughairi ni kubadili mawazo na kuacha kufanya ulichokwisha amua kufanya. Nisahihishwe tafadhali.”.

TABASAMU NA KITABU

$
0
0

Huyu ni rafiki yangu. Anaitwa Ragin Mbaga, ila tuwapo farashani hupendelea kumwita "Mzee wa bustani ya usomaji". 

Kitu kimoja kwetu tunapenda kusoma vitabu. Tunapenda kuandika andika maarifa. Tunapenda kusambaza upendo kupitia usomaji wa vitabu. Tunajua jamii inaweza kupigana dhidi ya ujinga kwa kutumia silaha ya vitabu. Tunapenda kujifunza kwa waliotuzidi na hata tuliowazidi. Madhumuni yetu ni kuhamasisha usomaji wa vitabu kwa wote.  

Kitu kingine zaidi, tuna amani sana mioyoni. Mimi nasoma "Mbio za Jasusi" cha Frowin Kageuka na yeye anasoma "Ishinde tabia ya kughairisha mambo" cha Joel Nanauka. Katika maisha furahia na ukipende kile ufanyacho. Ni tiba maridhawa.

Markus Mpangala,

Morogoro,
Oktoba 10/2017.

UTEUZI WA UBUNGE

PHILIP EMEAGWALI: MWANASAYANSI YA KOMPYUTA ALIYEIPA KASI ZAIDI INTANETI TUNAYOTUMIA SASA.

$
0
0
NA KIZITO MPANGALA

SOTE tunafurahia kutumia mtanadao wa kimataifa “international network” ambapo kwa utaalamu zaidi wa lugha maneno hayo mawili yamefupishwa kwa kuchukua herufi tano za mwanzo za neno INTERnet na haerufi mbili za mwanzo za neno NETwork na kupata neno INTERNET yaani mtandao wa kimataifa, na katika Kiswahili tumetoho na kpata neno INTANETI.

Mtandao huo unatusaidia kwa kiasi kikubwa sana katika shughuli mbalimbali. Wapo waliotumia muda na maarifa yao kwa ajili ya manufaa ya ulimwengu wote. Mtandao huo ulipoanzishwa haukuwa na nguvu kubwa ya “kukata mitaa” ya dunuia yote hii, lakini leo mtandao huu una pilikapilika nyingi na sehemu nyingi duniani na una matumizi makubwa. Ada yako ya kutumia intaneti ni bando tu!

Leo tunaye Mnigeria Philip Emeagwali ambaye amechangia mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nguvu na kasi ya intaneti. Kumbuka kwamba yeye si mvumbuzi wa intaneti lakini kwa kifaa alichokibuni kimesaidia kuboresha na kuipa nguvu na kasi zaidi intaneti tunayofurahia sasa hivi ambapo tunaweza kuwasiliana. Hata hapa usomapo, intaneti imesaidia sana kupata maandiko haya!

Philip Emeagwali alizaliwa mwaka 1954 katika mji wa Akure nchini Nigeria katika jamii ya kabila la Igbo. Mwaka 1967aliacha shule kutokana na vita vya Biafra  na alishiriki vita hivyo kama mpiganaji (askari) kwa lazima alipokuwa na umri wa miaka 14. Vita vilipomalizika alihitimu masomo ya sekondari kwa kufundishwa nyumbani na baba yake. Shule nyingi zilifungwa. Baba yake huyo alikosa fedha za kumlipia ada hivyo akaingia vitani Biafra. Wakati alipokuwa akifundishwa nyumbani na baba yake, alifundishishwa hisabati na kupewa maswali 100 kila siku na aliambiwa awe anayafanya kwa muda wa saa moja tu awe amemaliza! Hakika aliweza jambo hilo!

Katika zoezi hilo maana yake ni kwamba alikuwa anafanya kila swali kwa wastani wa sekunde 36 tu!

Philip anatushirikisha kumbukumbu ya maisha ya familia yake baada ya mapigano ya vita vya Biafra, ansema “tulikuwa tukiishi kama watumwa. Chakula tulikuwa mara moja tu kwa siku na wakati mwingine siku ilipita bila kupata chakula. Nilijitahidi kuwa na fikra ya kufanikiwa kimaisha ndio maana nilijijengea bidii” 


Alikuwa akiishi kwenye nyumba ambayo ni banda tu lililozungushiwa mabaki ya roketi zilizolipuliwa vitani Biafra. Alikuwa akijisomea kuanzia saa 6 mchana hadi usiku saa 4. Ndipo alipofaulu mtihani wa kujinga na chuo kikuu cha Oregon nchini Uingereza kwa udhamini. Alidhaminiwa kutokana na nia yake thabiti ya kupenda kujisomea vitabu na kujifunza zaidi.

Alijiunga na chuo kikuu cha Oregon nchini Uinngreza ambako alitunukiwa shahada ya kwanza ya Hisabati. Baada ya kumaliza masomo na kutunukiwa shahada ya kwanza ya hisabati nchini Uingereza, alienda jijini Washington DC nchini Marekani na baadae alitunukiwa shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha George Washington katika uhandisi wa ubaharia na mazingira (Ocean & Marine Engineering and Ecology) na baadae alitunukiwa shahada ya pili tena ya uzamili katika chuo kikuu cha Maryland katika Hisabati Tumizi (Applied Mathematics). Aliajiriwa na mamlaka ya ardhi mjini Wyoming kama mhandisi.
Emeagwali alitunukiwa shahada ya uzamivu katika chuo kikuu cha Michigan nchini Marekani katika masomo ya Sayansi ya kompyuta. Baadae chuo hicho kilificha taarifa zake kutokana na rangi yake nyeusi, maana yake ni kwamba lilikuwa ni jambo la kibaguzi. Alifungua kesi mahakamani kuhusiana na hujuma hiyo ya kufichwa taafifa zake kwamba isijulikane kama alisoma hapo lakini kesi yake ilifutiliwa mbali kwa vigezo vileveile vya kibaguzi. Hakukata tamaa, alijiamini ya kwamba amesoma Michigan.

Kwa elimu yake ya mazingira (Ecology) alifanya uchunguzi wa kina jinsi nyuki wanavyotengeneza asali kwa haraka na kwa ufanisi. Baada ya kumalisha uchunguzi wake huo kwa siku nyingi alichapisha matokeo yake ambayo aliyaongezea nguvu kwa elimu ya sayansi ya kompyuta. Lengo lake lilikuwa ni kuunda kompyuta yenye kasi zaidi. Alifanikisha jambo hilo ambapo alitumia vifaa vidogo vidogo 65,000 vya kielektroniki kuunda kompyuta hiyo ambayo ndiyo yenye uweza wa kasi kubwa duniani na ndiyo inayofanikisha intaneti iwe ya kasi zaidi. Kompyuta hii (Supercomputer) yeye ndiye mbunifu wa kwanza. Ina uwezo wa kukokotoa toni bilioni 3.1 kwa sekunde moja.

Ni ngumu kueleza ni wanasayansi wangapi na wanahisabti wangapi walichangia kupatikana kwa intaneti. Hakika walikuwa wengi. Lakini nguvu ya kasi ya intaneti imeletwa na kuasisiwa na mwanasayansi huyu Philip Emeagwali. Philip ndiye aliyebuni kanuni (formula) inayoruhusu kompyuta nyingi kufanya kazi kwa wakati mmoja zinapotumia intaneti.

Alifanikisha pia kuunganisha kompyuta 8 kubwa na kupata kile tunachoita KOMPYUTA MAHSUSI (SUPER COMPUTER). Hii alifanikisha katika maabara ya sayansi ya kompyuta jijini Los Alamos ambapo wanasayansi waliomtangulia walikata yamaa kutokana na ukweli kwamba kompyuta walizokuwa wakitumia hazikuwa na kasi sana kwa kuwa walitaka kuunda kompyuta itakayoweza kulisisimua bomu la nyuklia lilipuke haraka endapo mitambo itasetiwa mbali na bomu lilipo. Philip alifanikisha jambo hilo kwa kuunda “SUPER COMPUTER” ambayo iliongeza kasi ya nguvu ya utendaji wa intaneti na hivyo leo hii zipo kompyuta za aina hiyo nyingi na ambazo zina uwezo wa kusisimua mabomu yalipuke. Uvumbuzi huu ulimfanya apate tuzo ya nishani ya taasisi ya elimu ya elektroniki ya Gordon Bell mwaka 1989.

Anakili kwamba familia yake ilikuwa masikini wa kutupwa duniani kati ya familia masikini zilizokuwepo duniani. Philip ndiye mwanzilishi na mboreshaji wa sekta ya mafuta nchini Marekani, ushauri wake wa kitaalamu kwa sayansi ya kompyuta ulifanyiwa majaribio na kuona ya kwamba unafaa na mpaka sasa ndio unatumika na unaiingizia serikali ya Marekani mabilioni ya dola.

Milinganyo amabayo aliiasisi kutokana na kipawa chake cha hisabati na ambayo inatumika katika mashine za kuchimba mafuta inapofanyiwa kazi huweza kukupa mwelekeo wa kiasi cha mafuta unachoweza kuchimba na kama unaweza kuongeza uzalishaji au kama uzalishaji unaweza kupungua basi milinganyo hii inakupatia majibu. Ni wakati wa wanafunzi wetu vyuoni kudadisi mambo na si kusoma tu kwa lengo la kushinda GPA ya juu! Tunao wanafunzi wengi wenye uwezo huu lakini mazingira yanawafunika au wanajifunika vichwa!

Philip anasifika sana kwa kuwa gwiji wa hisabati na mwenye bidii ya kujifunza bila kukata tamaa. Mara nyingi yeye hakupenda kuitwa gwiji kwani alidai gwiji ni baba yake aliyeuhamishia ugwiji kwake yeye. Philip anasema “wakati fulani silipendi jina hilo, yaani sipendi kuitwa gwiji kwa sababu watu wengi hudhani ugwiji upo kwenye hisbati tu, si kweli. Sidhani kama kila mmoja kati yetu anayo nguvu ya kujipa ugwiji yeye mweyewe, mimi sikuzaliwa nikiwa gwiji na sikufahamu kama itakuwa hivyo. Ugwiji ulipandwa na baba yangu ndani yangu, hivyo, baba yangu ndiye gwiji” aslisema akiwa katika mkutanao wa wazazi nchini Nigeria mwaka 1999.

Philip anaongeza na kusema “watu huniita mimi gwiji wa hisabati, lakini mimi nawaambia kuwa yeyote anaweza kuwa gwiji kama akikokotoa maswali 100 kwa muda wa saa moja”. Philip aliwasisitiza wazazi katika mkutano huo kuwa mtoto akipewa kazi kutoka shuleni akaifanya nyumbani waichukulie kwa uzito kwa kuwa kazi za nyumbani (home work) zina umuhimu kwa mwanafunzi yeyote duniani.

Wazazi na welezi, fuateni mfano huu wa Philip. Leo inaweza kuonekana ajabu sana mtu kujisomea nyumbani na kuweza kimasomo, unaweza kukumbana na falsafa za kwamba umefoji vyeti lakini hakika jambo hili la kujielimisha nyumbani linawezekana. Mnapaswa kuwaamini watoto wenu katika kujifunza. Igeni mfano wa baba yake Philip alipoamua kumfundisha Philip nyumbani na kuweza kusonga mbele. Hamishia kipawa kwa mtoto wako ili asonge nacho mbele.

Philip kwa sasa ana uraia wa Marekani na ana taasisi yake inayoshughulikia masuala ya mawasilianao. Mpaka sasa ametunukiwa tunzo zaidi ya 80.

URUSI, CHINA KUTAWALA BIASHARA DUNIANI

$
0
0


 
MOSCOW, URUSI

MIKAKATI ya serikali ya Urusi kuifanya China kama mshirika thabiti na muhimu kiuchumi umechochea kukuza sekta ya biashara na kufikisha asilimia 22 katika mapato yake.

Gazeti la The Moscow Times limesema kuwa ushirikiana wa karibu baina ya Urusi na China umechangia kuimarisha mapato katika biashara na kufikia kiasi cha dola bilioni 80 mwaka huu huku matarajio yakiwa ni kufikiwa dola bilioni 200. 

Taarifa zinasema kuwa ili kuongeza mapato zaidi China imepanga kuweka mfumo mpya wa sheria za fedha wenye lengo la kurahisisha mikataba ya kibiashara kati yake na Urusi pamoja na kuongeza umuhimu wa matumizi ya Yuan duniani. 

Takwimu zilizotolewa na serikali ya China Oktoba 13 mwaka huu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu biashara kati yake na  Urusi imeongezeka kwa asilimia 22.4  ambayo ni kiasi cha fedha cha dola za kimarekani bilioni 61.4. Katika kipindi hicho hicho, usafirishaji wa bidhaa za Chinja kwenda Urusi umeongezeka kwa asilimia 17 ambacho ni kiasi cha fedha cha dola za kimarekani bilioni 31.4, wakati bidhaa za kutoka Urusi kwenda China zimeongezeka kwa asilimia 28.5 ambayo ni kiasi cha fedha cha dola za kimarekani bilioni 30 katika kipindi hicho hicho.

Aidha, imeelezwa kuwa katika kipindi cha mwezi Septemba biashara kati ya nchi hizo mbili zilifikisha dola za kimarekani bilioni 7.6, ambapo thamani ya bidhaa za China zilizopelekwa Urusi ni dola za kimarekani bilioni 3.79, wakati bidhaa za Urusi zilizopelekwa nchini China zimefikisha thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.81.

Kiwango cha ushirikiano wa kibiashara kati ya China Urusi kwa mwaka 2016 kilipanda kutoka asilimia 2.2 sawa na dola za kimarekani bilioni 69.5. nchi hizo zimetajwa pia kuwa washirika wazuri wa masuala ya kijeshi na diplomasia.

Biashara kati ya China na Urusi ilifikisha kiasi cha dola za kimarekani bilioni 5 na bilioni 8 miaka 1990, lakini kumekuwa na ongezeko kuanzia wakati huo.
Malengo ya awali ya nchi hizo mbili yalikuwa ni kufikisha kiasi cha dola za kimarekani bilioni 100 kabla ya kukumbwa na mdororo wa uchumi mwaka 2008.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa malengo ya Urusi yapo mbali sana ukilinganisha nay ale ya Umoja wa Ulaya ambako biashara imekuwa ikiyumba miongoni mwa wanachama. Wakati ushirikiano wa kibiashara kati ya Urusi na China ukizidi kuimarika, hali imekuwa mbaya kwa nchi zilizopo kwenye Umoja wa Ulaya (EU).Biashara kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya imeshuka kutoka Euro bilioni 330 mwaka 2014 hadi Euro bilioni 228 kwa mwaka 2016, huku wataalamu wa uchumi watabiri kuporomoka zaidi. 

Hilo lina maana kukua kwa biashara kati ya Urusi na China kumesababisha kuporomoka kwa biashara ya EU na Urusi. China inatarajiwa kuchukua nafasi ya EU kuwa mshirika muhimu wa kibiashara kati yake na Urusi ifikapo mwaka 2020.

MWALIKO; WOTE MNAKARIBISHWA KWENYE MJADALA HUU

FELA ANIKULAPO KUTI: MWANAMUZIKI ALIYEASISI MTINDO WA PIJINI KATIKA MUZIKI NCHINI NIGERIA NA KUOA WANAWAKE 27.

$
0
0
NA KIZITO MPANGALA

TUNASIKILIZAmuziki wa Nigeria mara kwa mara na pengine huenda uliwahi kujihoji aina lugha wanayotumia kuimba na hata katika mazungumzo ya kwaida ya wananchi wa Nigeria. Mtindo huo umejaa pijini kwa kiasi kikubwa hali iliyopelekea kuitwa NIGERIAN ENGLISH.

Fela Anikulapo Kuti alizaliwa  mjini Abeokuta nchini Nigeria mwaka 1938. Alipewa majina OLUFELA OLUSEGUN OLUDOTUM RANSOME ANIKULAPO KUTI lakini alifupisha na kuwa FELA ANIKULAPO KUTI. Mama yake alikuwa ni mwanaharakati wa haki za wanawake katika utawala wa kikoloni wakati huo, na baba yake alikuwa ni mwalimu na vilevile alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza mweusi wa chama cha walimu nchini Nigeria. Fela ni binamu ya Akimwande Oluwole Babatubde Soyinka maarufu kama Wole Soyinka.

Fela alisoma nchini Nigeria na baadae mwaka 1958 alikwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kusoma Udakitari wa Dawa lakini alipofika huko alivutiwa na masomo ya muziki hivyo akasoma masomo hayo ya muziki katika chuo cha Trinity. Fela alikuwa mjuzi wa kupiga tarumbeta na Saxophone.

Alianzisha bendi yake iliyoitwa Koola Labitos ambayo ilipiga muziki aina ya jazz.  Huko alimuoa mwanamke aliyeitwa Remilekun Taylor na wakawa na watoto watatu. Mwaka 1963alirudi nchini Nigeria na kuendelea na bendi yake aliyoianzisha na pia utangazaji katika shirika la utangazaji redioni la Nigeria.
Mwaka 1967alihamia nchini Ghana na kuanzisha mtindo mpya wa muziki ambao uliitwa Afrobeat. Mwaka 1979 alisafiri kwenda Marekani na alikaa kwa muda wa miezi 10 jijini Los Angels, huko alibadili jina la bendi yake na kuitwa NIGERIA 70. Baadae alitimuliwa nchini humo pamoja na waimbaji wenzake kwa kutokuwa na kibali cha kufanya kazi nchini humo.

Aliporudi Nigeria alibadili tena jina la bendi na akaiita AFRIKA 70 na akajikita na nyimbo zilizohusu masuala ya kijamii. Alianzisha studio yake aliyoiita KALAKUTA REPUBLIC. Jina Anikulapo alijipachika yeye mwenyewe likiwa na maana ya “msimamizi wa maisha na shighuli zake”, aliamua kujipachika jina hilo baada ya kuachana na jina Ransome ambalo alidai lilikuwa ni la kitumwa, hivyo alihitaji jina lake liwe na asili ya Afrika tu.

Katika bendi yake alikuwa maarufu hasa katika uamuzi wake wa kuimba kwa Pijini, ndio maana hadi sasa wasanii wengi wa Nigeria na hata mazungumzo ya kawaida ya raia wa Nigeria yana kiingereza chenye mchanganyiko na lugha zao za asili.

Mwaka 1977 alirekodi na kuachia ngoma iliyoitwa Zombie, ambayo alikuwa ikieleza jinsi wanajeshi wa Nigeria walivyokuwa wakivamia studio yake kutokana na nyimbo zake zilizodhaniwa kuwa zinaichefua serikali ya Nigeria. Fela alipigwa vibaya sana pamoja na mama yake ambaye alirushwa nje kupitia dirishani na akaumia. Waliichoma moto studio hiyo na vifaa vyake vya muziki pamoja na rekodi ambazo bado alidai hakuziimba.

Baada ya uvamizi huo uliosababisha maumivu makali mwilini mwake aliamua kutengeneza sanduku ambalo lilikuwa kama la kuwekea maiti na akaenda nalo katika kambi ya jeshi ya Dodan jijini Lagos ambako alikuwa akiishi Rais Jenerali Olusegun Abasanjo wakati huo na kuliweka getini kisha akaanza kuachia vibao viwili hapohapo getini. Vibao hivyo viliitwa SANDUKU LA MKUU WA NCHI na MWANAJESHI ASIYEJULIKANA. Aliimba kwa majuto ya stdio yake.

Fela Anikulapo Kuti akiugua baada ya kupigwa na wanajeshi
Fela aliooa wanawake 27 wengi wao wakiwa ni wanenguaji wake katika bendi yake. Lengo lake lilikuwa ni kutosambaratika kwa bendi yake na kuonyesha kuwa ana upendo wa dhati na washirika wake, hivyo akaamua kuwaoa. Mwaka mmoja baadae alipokuwa jijini Accra nchini Ghana akitumbuiza jukwaani na ibao chake cha Zombie alitangaza kuwaacha wanawake 15 na kubaki na wanawake 12. Hilo lilizua ugomvi jukwaani na serikali ya Ghana ikampiga marufuku kuingia tena nchini humo.

Alianzisha chama chake cha siasa alichokiita MOP (Movement Of the People), mwenyewe alidai anataka kuisafisha jamii ya Nigeria hasa katika ufisadi. Chama hicho kilikuwa kinafuata falsafa za Kwame Nkrumah. Na mwaka 1979 aliingia kwenye orodha ya wagombea Uraisi nchini Nigeria lakini baadae jina lake liliondolea katika orodha ya wagombea. Alikemea mapinduzi ya ovyo ya kijeshi nchini humo. Alikuunda bendi mpya iliyoitwa EGYPY 80 ambapo alikuwa akiimba na kutukuza ustaarabu wa Misri, historia yake, maarifa yake, falsafa zake, dini zake, na utaalamu wa hisabati katika Misri ya kale.

Jenerali Muhammadu Buhari alipoingia madarakani, alimsweka jela mwanamuziki huyo kwa kuwa harakati zake zilikuwa zinaichefua serikali ya Nigeria wakati huo. Pia alituhumiwa kutakatisha fedha. Pia ni kutokana na wimbo wake ulioitwa BEAST OF NO NATION uliokuwa ukimkosoa Rais Buhari kuwa ni mnyama aliye na kiwiliwili cha binadamu kadiri alivyoona utawala wake wa kijeshi. Katika wimbo huo alioimba kwa Pijini, anasema;

“No be outside Buhari dey yee,
na krase man be dat,
animal in krase man skin ii”

fela aliamni sana mtindo wa maisha wa Afrika na nyimbo zake nyingi zlikuwa zikikosoa utawala wa kibabe katika serikali za Afrika hasa utawala wa kijeshi nchini Nigeria wakati ule. Hivy0, likaa jela kwa muda wa miezi 20 ambapo alitolewa na jenerali Ibrahim Babangida. Kisha aliamua kuwataliki wanawake 12aliobaki nao.

Haifahamiki wazi sababu kuu ya kifo chake kutokana na hali yake kuwa dhaifu ambapo laikuwa anakonda mithili ya mtu aliyeathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI ingawa wengi husema aliathirika na ugonjwa huo kwa kuwa alisumbuliwa na kansa ya ngozi inayoambatana na ugonjwa huo.

0692 555 874.

WAAMUZI WA SOKA KATIKA JICHO LA JAMII.

$
0
0
NA HONORIUS MPANGALA
 
WAAMUZI wa soka wamekuwa wakitazamwa tofauti kulingana na wao wenyewe wanavyojiweka katika jamii ya wapenda soka. Wako ambao wameifanya fani hiyo kuwa moja ya vitu ambavyo vinaweza kuwapatia nafasi ya kucheza matangazo. Pia wapo ambao jamii imewachukulia tofauti kutokana na mitazamo yao.
Jonasia Rukyaa.
Kuna mitazamo hasi kwa baadhi ya wapenda soka waonapo waamuzi wa kike wakichezesha mchezo. Mitazamo hiyo inatokana na asili ya mchezo wenyewe unavyochukuliwa kama ni wa wanaume. Licha ya wanawake kuucheza lakini bado mitazamo hiyo imekuwa ngumu kuwatoka baadhi ya wapenda soka. Ndo maana hata wale wanawake wanaocheza soka ukiwatazama utafikiri wanaume Kwa baadhi yao.

Tanzania ina Mwamuzi wa kati maarufu Jonasia Rukyaa ambaye anafanya vizuri sana. Alikuwepo katika mashindano ya Afcon ya wanawake ikiyofanyika Kameruni. Pia baada ya kushiriki katika kliniki ya waamuzi Kule Ureno mwaka huu amekuwa na mwaliko 'appointment' ya uwepo katika kombe la dunia. Na yupo katika mshindano ya kombe la dunia la vijana wa chini ya miaka 17 Iliyofanyika India. 

Wako waamuzi wengi wa kati wanawake dunia kama ilivyo Kwa Bibiana Steinhaus (Ujerumani), Amy Fear(Uingereza), Sian Massey-Ellis, Lucy Oliver (Uingereza) Fernanda Colombo Uliana (Brazil). Na hata hapa kwetu Tanzania wapo wasaidizi kama Helen Mduma, Janet Balama, Grace Wamara.
Fernanda Colombo Uliana
Kwa namna fulani waamuzi wetu wanawake wameshindwa kujipambanua katika kujiweka huru na kazi kutokana na mitazamo ya jamii. Mitazamo hiyo inatokana ni kiini cha mitazamo ya kikabila iliyopo na jinsi inavyomchukulia Mwanamke mbele ya mwanaume kama sio mtu wa kutoa maamuzi Kwa mwanaume.

Sasa nataka niwaeleze waamuzi wetu wanawake Kwa wale wa kati na wale wasaidizi. Inawezekana mtu asijue namna ya kuipata fursa lakini baada ya kuipata unaweza kujiweka katika hali ya kutazamika tofauti katika kazi yako.
Nianze na kusema jambo moja toka Kwa Mwamuzi msaidizi mwanamke ambaye inasemekana ni Mwamuzi mwenye mvuto kuliko wote Brazil. Anaitwa Fernanda Colombo Uliana. Huyu baada ya kuifikia fursa ya kuwa Mwamuzi akaamua kujitengenezea mazingira ya upekee kujitambulisha kwa wapenzi wa soka. Utambulisho huo ulitokana na mwonekano wake mbele ya mashabiki na timu pia. Baada ya kuonekana tofauti akaanza kunyatiwa na makampuni ya utengenezaji wa vifaa vya Michezo na kufanya matangazo.

Waamuzi wa Brazil wanavaa sare za 'penalty' zinazotengenezwa na kampuni ya vifaa vya Michezo vya Malharia Cambuci S.A. kampuni hiyo iliwahi kuivalisha pia Klabu ya Sao Paulo na Gremio za huko. Iliingia mkataba pia na golikipa wa zamani wa Fc Barcelona Victor Valdes mwaka 2010 kama mtu anayetangaza vifaa vya Penalty.

Ujio wa Fernanda Colombo Uliana Kwa wabrazil katika uamuzi wa soka ilikuwa kama kachori kwenye mhogo uliokaangwa na mafuta. Namaanisha waliupokea vizuri kwasababu ya mvuto wake awapo kwenye mstari wa uwanja. Katika kulifanyia kazi hilo Mwamuzi hiyo alikuwa akipangwa kama 'line one'.

Kama ujuavyo 'Line one' husimama karibu na moja mabechi ya timu zinazocheza. Ikawa kama ni burudani nyingine kumwona Mwamuzi hiyo katika vazi lake huku umbo lake likiwa burudani ya macho Kwa wachezaji wa akiba na hata watazamaji wengine. Si unajua macho ya wanaume yalivyo kosa ustahimilivu mbele ya maumbo muswano ya wanawake.

Baada ya kuonekana kuvutia watu kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya Michezo ya Malharia Cambuci S.A kupitia vazi lake la penalty wakamua kumfanyia maboresho vazi la Fernanda. Hiyo ilikuwa kutokana na yeye jinsi anavyo jipambanua awapo kazini. Hadi kufikia hapo kampuni ililazimila kuingia nae mkataba wa kutangaza vazi hilo Kwa waamuzi wa kike na kuonekana mtu wa kwanza kuvaa ni Fernanda.

Fernanda Colombo Uliana
Umaridadi ule wa vazi mpya lilolokuwa kaptura ambayo mbele imefunikwa na kitambaa kingine na kuonekama mithiri ya sketi fupi ulinogesha umbo la Fernanda. 

Fifa wamefikia hatua kukubali vazi la Fernanda kutumika katika mashindano yake na huenda likaanza kutumika mwakani Kwa waamuzi wa kike kwenye fainali za kombe dunia. Fernanda alikuwa maarufu Kwa vazi lile dunia kote kwasababu fursa aliyoipata ameitumia Kwa mitazamo chanya na kufikia hatua ya kujipambanua.

Kwa jamii yetu ya kiafrika hususani Kwa taifa letu la Tanzania mitazamo ndo kitu kinacho wafanya pengine wasizifikie zile fursa ambazo walizihitaji kuzifikia. 

Nilimtazama Mwamuzi msaidizi katika mechi ya Simba na Mtibwa Dada kutokana Iringa Janet Balama nikajisemea moyoni yawezekana mitazamo inaweza mfanya asijipambanue na kuwa huru zaidi ya nimwonavyo kwenye mstari wa uwanja.

Mwili wa mwanamke umekuwa usiogusika kirahisi na wanaume katika jamii zetu. Halo hiyo inafanya hata watu kuchukuria tofauti pale Mwamuzi wa kike atakapoguswa sehemu yoyote ya mwili wake itatafsiriwa vibaya. Na hata watu jinsi na ustawi wa jamii utawasikia wakija na tamko kuwa ni udhalilishaji.

Ni Mara ngapi tunaona Mwamuzi wa kike kavaa kaptura fupi na kuchezesha mchezo. Huwa haitamkwi kama vazi lake halina staha licha kuonyesha mapaja wanasubili mchezaji akimpa mkono wa ishara ya uungwana Mwamuzi Kwa kugusa popote katika mwili wake. Wachezaji wamekuwa na mazoea ya kugusana popote iwe katika kalio au bega au kifua au ubavuni. 

Tatizo huja Kwa wapenzi wa soka wenye mitazamo tofauti na uhalisia wa tukio. Uhuru wa mwili na akili ndio ambao humpa uwajibikaji ulio bora Mwamuzi wa jinsi yoyote. Hivyo hata Dada zangu hawa wanapaswa kuwa huru na kuachana na mitazamo ya mashabiki. Kwasababu inaweza kutokea makampuni ya vifaa vya Michezo wakaja na mtindo mwingine wa sare za waamuzi wa kike. Hii ilitokea Kwa vilabu vya ulaya baada ya kuona wana mashabiki wanaume na wanawake wakaamua kuunda jezi za kuziuza kwa mwonekano wa jezi ya kuvaa mwanaume na kuvaa mwanamke. 

Natamani kuona mitazamo ya wale zi wa soka ikabadilika nikaona uhalisia wa Uhuru wa mwili mahala pa kazi kwa dadangu Mwanahamis Matiku, Jonasia Rukyaa na wenzao Helen Mduma,Janet Balama,Grace Wamara, Dalila kutokana Zanzibar na Frolentina kutokana Dodoma.

Ziko kampuni za mavazi ambazo Leo hii zinafanya kazi makocha,wachezaji na hata waamuzi kulingana na aina ya vazi ambalo anaweza kulifanyia matangazo.
Uliwahi kujiuliza umuhimu wa mashindano ya Umiss au kujiuliza kwanini katika mapambano ya ngumi kila raundi Dada mrembo anapita na bango akionyesha raundi inayofuata. 

Kwanini iwe kwao na sio wanaume. Vitabu vitakatifu vimeandika mwanamke ni pambo la nyumba sasa kushindwa kwetu kuwatengenezea mazingira ya kuwafanya watu wakahamasika na uwepo mahali Fulani ambapo mwanamke atakuwa mwendesha shughuli hizo ni akili zetu za tuliopo ulimwengu wa tatu.
Mitazamo yetu ikibadilika dhidi yao hata soka lao litakuwa na mashabiki wengi kwasababubya kutumia vyema fursa.

0628994409

NIYONZIMA SIO MSAADA MBELE YA MASHUTI YA NDEMLA

$
0
0

NA. HONORIUS MPANGALA
 
SAID NDEMLA

ILIKUWA ni Oktoba 20, 2013 ambapo mechi ya watani hawa wa jadi ilikuwa na matokeo ya kushangaza mashabiki. Mchezo ulimalizika kwa sare ya bao tatu kwa tatu. Hadi wanaenda mapumziko ilikuwa tayari Yanga anaongoza goli tatu zilizofungwa na Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza aliyerudi nyavuni Mara mbili. Kila kitu kwa Simba kilienda vibaya ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Wale waliokuwa na ushabiki uliopitiliza waliamua kuondoka uwanjani kwa kujua dhahama ya kichapo iko upande wao. Ikumbukwe ni msimu mmoja nyuma yaani 2011/12 Simba alitoka kuwafunga Yanga bao tano bila. Hivyo wengi waliamini zinarejeshwa ile oktoba 20. 

Ilikuwa Simba iliyoongozwa na Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kihwelo. Maamuzi ya kuusoma mchezo na kufanya maamuzo ambayo mashabiki walifikia hatua ya kulaumu kwa nini yanafanyika kwa wachezaji wale kiliwazidishia wasiwasi mashabiki. Bechi la Simba liliwainua William Lucian na Said Hamis Ndemla kuchukua nafasi za Abduhalim Humud na Haruna Chanongo.
Ilikuwa ni wasaa wa vijana hawa waliotoka katika kikosi cha vijana cha Simba kuwadhihirishia wapenzi na mashabiki wao kuwa walimu hawajakosea kuwaingiza mchezoni baada ya kubaini mapungufu yaliyokuwepo kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza. 

Ndemla alilishika dimba vyema kwa kukaba na kupiga pasi ndefu na fupi. Mambo yalibadilika ndani ya muda mfupi alioingia kwa eneo la kiungo. Aliwapoteza viungo wa Yanga akiwemo Haruna Niyonzima aliyesumbua kwa dakika 45 za awali. 


Hakutakuwa na la kustaajabisha kama utamsikia Ajibu akisema namkubali sana Ndemla na wakati huohuo Ndemla akisema anamkubali sana Ajibu. Hawa vijana ni vipaji tofauti na tunavyo watathimini katika mzani mwepesi kiasi hicho.

Ndemla alimfanya kocha wa Yanga wakati huo Erne Brandts ajikune kichwa pasipo kuwasha na nywele zake. Dakika ya 53 Bertram Mwombeki aliwainua mashabiki wa Simba kwa kupachika bao safi akipokea pasi toka kwa Amiss Tambwe. Wakati goli linapatikana ilikuwa Yanga wameendeleza kosakosa nyingi langoni mwa Simba.

Mabadiliko ya kiakili kwa sehemu ya ulinzi wa kati kwa Simba kulileta matunda kwani mrundi Gilbert Kaze na Mganda Joseph Owino walisimama vyema. Umakini wao ulifanya Ndemla ulifanya kazi kubwa ya kuunganisha timu kwa kusaidiana na Jonas Mkude akiwa ni kijana mwenzake toka timu ya vijana ya Simba ambayo ilichukua ubingwa wa Uhai na kuinyanyasa Mtibwa kwenye mashindano ya BancABC.

Yanga walipotezwa na Ndemla hakukuwa cha Niyonzima wala Mbuyu Twite katika eneo la kiungo,wote wakabaki wanafukuza kivuli cha kijana yule mwenye wajihi wa upole ambao kwa Ndemla kulikuwa na tafsiri ya tofauti katika miguu yake. Anapiga mashuti akiwa nje ya eneo la kumi na nane anatawanya vyema mipira kwa wakati.
'Show' ilikuja kushangaza zaidi baada ya goli la pili kwa Simba dakika ya 57 lililofungwa Joseph Owino. Kila kitu kilibadilika. Kila mchezaji aliamini inawezekana kushinda mchezo. Kona ya Ramadhani Singano ilitua katika kichwa cha Kaze na kuandika bao la tatu dakika ya 84. Ndani ya dakika zilizobaki ilikuwa Yanga ndo walitamani mchezo umalizike.
Kila mpenzi wa Soka kumbukumbu yake kwa Ndemla inaanzia katika mchezo ule. Kwa kipindi chote kiungo Huyo amekuwa na kiwango bora na kile kile kila anapopewa nafasi huonyesha kile alicho nacho. Unaweza kusema kama hana bahati na Makocha wanaoinoa Simba kwani makocha walio onyesha kumuamini na kumpa muda mwingi wa kucheza alikuwa ni Patrick Lewig na Goran Kopunovic ambao waliamini sana vijana katika kikosi cha Simba.

Licha ya kuwa kipenzi cha mashabiki ka ilivyo kwa Jonas Mkude lakini bado Kocha Omog hajampa muda mwingi wa kucheza huku nafasi yake ikionekana ikichezwa sana na James Kotei,Mzamiru yassin na Haruna Niyonzima. 

Katika kutazama jicho la kiufundi ingefaa sana kama Omog akaamua kumwanzisha Ndemla badala ya Niyonzima kama inavyokuwa. Haruna ni mchezaji mkubwa na mwenye uwezo mkubwa sana lakini kwenye mechi kubwa amekuwa akipania sana mchezo husika. 

Rejea katika mechi za Yanga dhidi Azam ambapo aliwahi kupata kadi nyekundu katika moja ya mechi dhidi ya timu hiyo. Pia alikuwa anapata wakati mgumu sana katika pambano la Simba na Yanga hadi kufikia hatua ya kutuhumiwa kutumika na klabu aliyoko sasa. Lakini kumbe kiufundi ilikuwa ni kuzidiwa au wapinzani kumfahamu soka lake na kumdhibiti barabara. 

Mechi ya ngao ya jamii ni moja ya mechi ambazo niliona Haruna akiendela kukamia 'kupaniki' kwenye mchezo akihitaji kufanya kitu dhidi ya Yanga lakini akawa anashindwa kwasababu ya kukosa utulivu wa akili. Katika Michezo sita aliyocheza Haruna hajawa nachango mkubwa sana katika matokeo ya Simba kutokana aina yake ya kiuchezaji kufahamika sana na wapinzani wake. Soka la shoka hapo ndipo unapoweza msababishia kadi Haruna kwasababu ya kutawaliwa na hasira.

Ulikuwa ni wakati wa Ndemla tena kupewa jukumu la kusimama mbele ya Mkude au Kotei ili awaongoze wenzake namna ya kucheza zilipendwa ya wasafi.Kwanza ni mtulivu wa akili pili ana uwezo wa kumudu hasira tatu ni mchezaji asiye na mambo mengi dimbani mtazamo wake unakuwa katika kulitafuta goli liliko.

Nyakati zote ninazo tazama mechi za Simba anapoingia Ndemla mashabiki hufurahia sana tofauti na zile hali zinazoweza jitokeza za kulaumu mabadiliko. Sababu kubwa mashabiki ni kwamba Ndemla anauwezo mkubwa wa kupiga mshuti kuelekea kwenye lango la wapinzani. 

Hilo halina ubishi awapo uwanjani anabadilisha mchezo toka falsafa ya Simba iliyozoeleka ya kupiga pasi nyingi na badala yake wanakimbia kwa kasi kuelekea lango wapinzani. Apatapo nafasi ya mpira nje eneo la goli hupiga mashuti makali kitu ambacho washambuliaji na viungo wengine hawafanyi hivyo.
Rejea mabadiliko ya Ndemla dhidi ya Mbao,Mtibwa na Azam alikuwa mtu kujaribu kupiga na ndio kawaida yake ya soka analolihusudu. Kila kiungo anakuwa na utambulisho wake awapo uwanjani. Nakumbuka sana alipoingia akitokea bechi kawenye mchezo wa Tanzania dhidi ya Malawi katika uwanja wa Taifa. Alipokonya mpira toka kwa mchezaji wa Malawi huku akiwa karibu na Himid Mao. Akadanganya kama anauruka ule mpira kumwachia Himid halafu akaukanya na kusonga nao huku akiwaacha wachezaji wa malawi wakitaka kumkaba Himidi. Mashabiki walilipuka kwa Shangwe na wakisema "huyu mtoto Fundi".

Licha ya kocha kuwa na uamuzi wake kwa kuwa na 'game plan' Fulani anapoikabili timu pinzani. Suala la kutazama mchezo upi unamfaa mchezaji yupi ni jema pia. Uchu alionao Ndemla katika kuendelea kuwaaminisha mashabiki wa Simba kwa yeye ni yuleyule wa Oktoba 20, 2013 anatamani sana kuudhihirisha katika mechi kubwa kama dhidi ya Yanga. 

Sura yake na kazi yake dimbani hukupa wasaa wa kuliona soka lote aheli wangecheza wachezaji wenye sura kama yeye. Maamuzi yatabaki kwa Mwalimu katika kutazama kikosi chake na kuamua ni yupi acheze. Hakuna ubishi kuhusu eneo ambalo kocha Omog anapata kigugumizi kupanga kikosi chake kama eneo la kiungo.

0628994409

KWANINI WILAYA YA NYASA IMESHIKA MKIA KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA?

$
0
0


RAYMOND NDOMBA, SONGEA
WILAYA ya Nyasa iliyopo mkoa wa Ruvuma imekuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu 2017 kimkoa. Swali la kujiuliza ni kwanini hali hiyo imetokea. 

Mawazo yangu ni haya; Pamoja na sababu nyingi zilizosababisha matokeo hayo ya aibu kubwa. Wazazi wanapaswa kubeba lawama kubwa. Wengi wao hawafuatilii maendeleo ya watoto wao, pia makuzi na malezi mabaya.

Miaka ya hivi karibuni (kuanzia mwaka 2000), Wazazi wengi katika wilaya ya Nyasa hawajali elimu, hawajigusi katika ufuatiliaji wa watoto wao kielimu na hata kitabia (Angalia matokeo ya mitihani ya Taifa ya shule za msingi na sekondari kunzia miaka hiyo ya 2000 kwa shule kongwe ndani ya wilaya). 

Wazazi wanapenda tu kuona mtoto anakwenda shule ila sio kufuatilia ili afahamu mtoto huyo anafanya nini huko shuleni. Hawajigusi hata kujua kama mtoto kalala ndani au yuko wapi nyakati za usiku (saa 1 adi 6 usiku). Binafsi katika janga hili, asilimia 75 za lawama zangu nazielekeza kwa wazazi. 

Mwezi wa 8 na 9, 2017 nimekaa sana Nyasa. Nimetembelea Tingi, Chimate, Kwambe, Likwilu/Kilosa, Mango, hadi Lituhi; katika maeneyo yote niliyopita wazee kwa vijana wako sambamba na wanzuki (Mabobo). Muda wote na siku zote za wiki wao ni mitungi tu. 

Sehemu kama Kwambe, Matenje, Mtipwili, Ruhekei, Kilosa, Maporomoko Liuli, Lundu, Mbaha, Lituhi nk; nimeshuhudia wazee kwa vijana wakiwa wanakunywa komoni/wazuki (Mabobo) kuanzia saa 2 asubuhi. Wazazi wengi wamejiweka mbali kabisa na mambo yanayo husu taaluma. 

Kwao kazi ya malezi, makuzi na maendeleo ya watoto wao kitaaluma ni jukumu la mwalimu. Kitu ambacho si sahihi. Kila mwana Nyasa aliangalie tatizo hili kwa jicho la pekee. Tukawaelimishe wazazi wetu, ndugu zetu na watoto wetu juu ya umuhimu wa ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya kitaaluma na kitabia ya watoto wetu waliopo shuleni.

Katika hili, binafsi napingana na wale wanaoelekeza lawama zao kwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Stella Manyanya. Tatizo hapa lipo kwetu wenyewe (wana Nyasa). Ili tuitatua changamoto hii, yatupasa tuanze kuangalia upya makuzi na malezi ya vijana wetu kuanzia ngazi ya familia pamoja na kufuatilia mienendo yao kitabia wakiwa nyumbani na hata shuleni. 

Hatuwezi pata matokeo chanya kwa watoto wenye tabia hasi, hatuwezi pata vijana wenye mitizamo ya kimaendeleo toka kwa familia isiyo fuatilia malezi, makuzi na mienendo ya mtoto wao kitabia na kitaaluma na hatuwezi pata matokeo chanya toka kwa viongozi wa elimu wenye uwezo mdogo kitaaluma. 

Baadhi ya wakuu wa shule na maafisa walishindwa kwenda kujiendeleza kitaaluma kwa nia ya kulinda vyeo vyao. Na baadhi yao walichangia sana kushuka kwa kiwango cha elimu kwa vile walikuwa wanashindwa kusimamia majukumu yako ipasavyo na wengine kushindwa kuwawajibisha walimu wengine walio wazidi kitaaluma.
Baadhi ya Majengo ya Mbamba Bay High School yakiendelea kujengwa.
Tukiacha kubadilika na kuchukua hatua mapema hata hiyo “Mbamba Bay High School” ambayo inajengwa kwa kasi na majengo ya kisasa, itakuwa ni jiko la kuwapika vijana toka nje ya wilaya ya Nyasa.
Mwaka 2016 vijana wa kidato cha nne Lundo Sekondari waligoma kufanya mitihani ya muhula kwa madai eti itawapotezea muda wa kujisomea kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa. Nini chanzo cha tabia kama hii na wanafunzi wale walitoa wapi ujasiri wa kuwagomea walimu wao? TABIA TABIA TABIA.

SEBASTIAN KURZ; Kiongozi mbichi anayeugusa ulimwengu

$
0
0


NA MWANDISHI WETU

“ULIKUWA unafanya nini ulipokuwa na umri wa miaka 31? Hiyo ni sentensi ya kwanza iliyoandikwa na Mwanahabari wa Televisheni ya CNN, James Masters, kwenye tovuti ya CNN. Sentensi hiyo ilinivutia zaidi, ingawa aliendelea na mengine, lakini staili pekee haikuwa kivutio, bali mtu aliyekuwa akizungumzwa alivutia zaidi. 

Mwandishi James Masters alikuwa anamzungumzia kijana mmoja aitwaye Sebastian Kurz kutoka Austria. Ni kijana ambaye anazidi kuvutia duniani kutokana na siasa zake ambazo kwa namna moja au nyingine ziliibua nchi hiyo kwenye ramani ya kidiplomasia. 

Baada ya hapo nililazimika kufuatilia habari zaidi za Sebastian Kurz. Niliyokutana nayo ni somo, ingawa kwa Tanzania lilianza muda mrefu.
Nimekuandalia makala haya msomaji ili kujifunza jambo katika malezi ya familia na taifa kwa ujumla. Austria ipo tayari kwa kiongozi kijana? Fuatilia.

Sebastian Kurz ni nani?
Kijana huyu alizaliwaAgosti 27, mwaka 1986. Kwa sasa ana umri wa miaka 31 tu. Yeye ni mwenyekiti wa chama cha Austrian People’s Party (OVP) tangu Mei, mwaka huu. Baba yake ni Josef Kurz, ambaye alikuwa injinia. Mama yake ni Elizabeth Kurz, ambaye kitaaluma alikuwa mwalimu. Amekulia katika jiji la Vienna, ambalo ndilo makao makuu ya serikali na mji wa kibiashara nchini humo. Sebastian ni muumini wa Kanisa Katoliki. Anatajwa kuwa ni Mkatoliki mhafidhina. 

Miaka ‘mitatu mitatu’ ya dhahabu
Baaadhi ya wazungu wanahusudu sana mchezo wa namba. Katika mchezo wa soka namba 13 inatajwa kuwa yenye mkosi. Mifano mbalimbali inatolewa, lakini hali hiyo ni tofauti kwa miaka mitatu mitatu ya dhahabu kwa Sebastian. Iko hivi, mwaka 2009, akiwa na miaka 23, alichaguliwa kuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa chama cha OVP. 

Aidha, Sebastian alipokuwa na miaka 24 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Austria. Miaka mitatu baadaye alipotimiza miaka 27, yaani mwaka 2013, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Katika kipindi hiki aliwahi kuitisha mkutano wa mawaziri 30 wa Mambo ya Nje wa nchi za Umoja wa Ulaya uliofanyika nchini Austria. Mnamo mwaka 2014, alichaguliwa kuwa mbunge kupitia chama cha OVP. 

Kutoka umri wa miaka 24 hadi 27, tofauti ni miaka mitatu. Kutoka umri wa miaka 27 hadi 31, tofauti yake ni miaka mitatu na nusu. Hii ina maana wakati mwaka huu ukiwa wa tatu tangu akabidhiwe cheo cha uwaziri wa mambo ya nje, amechaguliwa tena kuwa Kansela wa Austria. 

Kwanini amekuwa Kansela?
Katika umri wa miaka 31, Sebastian Kurz anakabidhiwa majukumu makubwa ya kuiongoza Austria, baada ya rais wa nchi hiyo, Alexander Van der Bellen, kumuomba aunde serikali ya kitaifa na chama kingine cha Freedom Party. Uchaguzi uliofanyika mwaka huu ulikipatia chama chake cha OVP asilimia 31.4 ya kura zote. Vyama vingine vilipata alama zifuatazo; Freedom Party (27.4%) na Social Democrats (26.7%). Kutokana na ushindi huo,  haukumwezesha kuunda serikali, hivyo kulazimika kuungana na chama cha Freedom Party kuunda serikali. 

Ni mtaalamu wa nini?
Sebastian ana shahada ya sheria aliyopata kutoka Chuo Kikuu cha Vienna mara baada ya kumaliza mafunzo ya lazima ya Jeshi la Kujenga Taifa la Austria.

Mdogo kama Kim, Macron
Nchini Ufaransa walijivunia kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, Emmanuel Macron (39). Nchini Korea Kaskazini pia wanajivunia kiongozi mdogo zaidi, Kim Jong-Un, mwenye umri wa miaka 33. Pamoja na Canada ambao walimpa waziri mkuu mdogo kuliko wote, Justin Trundeau mwenye umri wa miaka 45.  Pia ni kama Leo Vardarkar mwenye umri wa miaka 38 na raia wa Ireland, ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa Usafirishaji, Utalii na Michezo mwaka 2011.
Naam, wananchi wa Austria wanamwona Sebastian Kurz kama Emmanuel Macron, Justin Trudeau, Leo Vardarkar, Kim Jong-Un kutokana na umri mdogo, lakini wamebeba matumaini makubwa ya uongozi wa nchi zao. 

Nyerere, Salim na Kabila
Katika suala la uongozi hapa nchini pia zipo rekodi za viongozi vijana. Mwalimu Julius Nyerere alikabidhiwa urais akiwa na miaka 40. Salim Ahmed Salim alikabidhiwa ubalozi wa Misri akiwa na miaka 22. Naye rais wa sasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, aliukwaa urais akiwa na miaka 29 tu. Kwa namna fulani utaona kuwa, dunia imekuwa na mabadiliko ya hapa na pale kwa viongozi wengi vijana kukabidhiwa majukumu makubwa. Sababu kubwa ni kwamba, wanakuwa na vitu vya ziada kuliko wengine pamoja na kuaminiwa au kuwa sehemu ya mtandao wa wanasiasa wenye kukabidhiana madaraka. 

Makala haya yameandaliwa kwa msaada wa mashirika ya habari.

TAARIFA YA KUNG’ATUKA LAZARO NYALANDU, MBUNGE WA SINGIDA KASKAZINI

$
0
0


NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.

HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. 

AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo. 

VILEVILE, nimemua kujiuzulu KITI Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. 

Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na nchi yenye ADILI.
#MunguIbarikiTanzania.
Lazaro S. Nyalandu.


FURSA: MAFUNZO YA JESHI JKT 2017

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo anawatangazia vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2017.
 
Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo, unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa mikoa na wilaya ambapo muombaji anaishi.

Zoezi la kuchagua vijana litaanza Mwezi Novemba 2017 na vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 04 mpaka 09 Desemba 2017.

Jeshi la Kujenga Taifa linaendelea kusisitiza kuwa nafasi za vijana kujiunga na mafunzo ya JKT haziuzwi, aidha yeyote atakaye husika na utapeli wa kuuza au kununua nafasi hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Sifa za mwombaji ni kama ifuatavyo:
1. Awe raia wa Tanzania.
2. Kwa vijana wenye elimu ya Darasa la Saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.
3. Vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne ni kuanzia miaka 18 hadi 20.
4. Vijana wenye elimu ya Kidato cha Sita ni kuanzia miaka 20 hadi 22.
5. Vijana wenye elimu ya Stashahada na Shahada ni kuanzia miaka 23 hadi 25.
6. Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamili ni kuanzia miaka 26 hadi 27.
7. Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamivu ni kuanzia miaka 28 hadi 35.
8. Awe na afya njema, akili timamu na asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo).
9. Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.
10. Kwa vijana waliomaliza elimu ya sekondari kidato cha nne, wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2015, 2016 na 2017 wenye ufaulu wa alama (Points) zisizopungua 32.
11. Awe na cheti cha elimu ya msingi aliyehitimu Darasa la Saba.
12. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).
13. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving Certificate).
14. Awe na cheti halisi cha matokeo (Original Academic Certificate) na kwa wale waliomaliza shule mwaka 2017 wawe na Transcript au Statement of Result.
15. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.
16. Asiwe amepitia mafunzo ya JKT Operesheni za nyuma.
17. Asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo.
18. Aidha, Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kujigharamia nauli za kwenda na kurudi kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa na pia kuwa na vifaa vifuatavyo:
19. Bukta ya rangi ya Dark blue yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu. Aidha bukta za wanawake zinatakiwa kuwa na lastic magotini.
20. Raba za michezo zenye rangi ya kijani.
21. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
22. Soksi ndefu za rangi nyeusi.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 30 Oct 2017

WAZIRI KAZINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, Hamis Kigwangallah, akiwa kwenye ziara ya mojawapo ya Mbuga za wanyama

CCM WALIPANGA KUMFUKUZA LAZARO NYALANDU AU AMEITEMA CCM? SOMA BARUA YA SPIKA WA BUNGE

UCHAGUZI KATA 43 KUFANYIKA NOVEMBA 26 MWAKA HUU

$
0
0

Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi. Uchaguzi wa udiwani Novemba 26.
1.      CCM-wagombea 43 katika kaata 43
2.    Chadema-wagombea 42 katika kata 43
3.    ACT-Wazalendo-wagombea 18 katika kata 43
4.    ADA-Tadea-mgombea mmoja katika kata 43
5.     ADC-wagombea wanne katika kaata 43
6.    NCCR-Mageuzi-wagombea 6 katika kata 43
7.     NRA-wagombea wawili katika kata 43
8.    SAU-wagombea wawili katika kata43
9.    TLP-mgombea mmoja katika kata 43
10.                        UDP-wagombea wawili katika kata 43
11.  CHAUMA-mgombea mmoja katika kata 43
12.CUF-wagombea 30 katika kata 43
13.DP-wagombea watatu katika kata 43

SOMO LA LEO

$
0
0
“Nitashangaa sana kama patakuwepo wanafunzi waliopo kwenye orodha ya kupata mikopo na wawe hawajapata, nitashangaa sama lwa sababu mimi najua nimeshaidhinisha fedha hizo na zimeshatoka,”
 
RAIS JOHN MAGUFULI
Viewing all 535 articles
Browse latest View live