Quantcast
Channel: KARIBUNI NYASA
Viewing all 535 articles
Browse latest View live

KAMERA YETU NORWAY

$
0
0


Furahisha macho kwa vipawa walivyo navyo wenzetu. Hapo ni Norway kwenye bahari ya Atlantic ambapo walijenga barabara kukatiza bahari kuunganisha miji iliyoko visiwani kwenye eneo la bahari. Kwa kuisoma zaidi tafuta Google. Atlantic way in Norway utaiona. Ila nilipata bahati ya kuzuru eneo hili wiki chache zilizopita nikiwa kwenye mkutano huku mwezi uliopita.

PICHA KWA HISANI YA BENJAMIN MBEZI

KITAI NI ENEO ZURI KWA UWEKEZAJI

$
0
0
Pichani ni sehemu ya mji wa KITAI. Mahali hapo ni makutano ya barabara za Songea-Mbinga, Mbinga-Lituhi, Songea-Lituhi, mkoani Ruvuma ambapo kunajengwa Kituo cha usambazaji wa umeme vijijini (REA). Hilo eneo kushoto, na upande wa kusini ni tambarare na ambalo halikumbwi na mafurikio. Panafaa sana kufungua mradi wa uwekezaji hapa ni kiunganishi cha wilaya tatu za Mbinga, Songea na Nyasa. Sifa yake kubwa ni kuzikutanisha wilaya hizo na kuwa eneo la katikati katika kupata huduma za kibiashara n.k

MAISHA

$
0
0
Maisha ni furaha na huzuni,
Yakupasa kuyafikiri akilini,
Ongeza na maarifa ubongoni,
Usisahau na akiba kibindoni.

Ni huzuni na furaha maishani,
Ni furaha zaidi kupata amani,
Ya maisha kuitunza duniani,
Aliye mjini hata kijijini.

Maisha ni huzuni na furaha,
Wengine raha waona karaha,
Wapo wanaoupenda mzaha,
Wenigne wajigamba kwa madaha.

Ingawa ni furaha na huzuni,
Nyumbani kwetu nako mamtoni,
Jitahidi kuweka akiba kibindoni,
Ikufae uishipo hapa duniani.

Kweli ipo huzuni na furaha,
Tuichapeni kazi tuache mzaha,
Raha yetu isije kuwa karaha,
Unisikilize kwa makini Twaha.

Hakuna atafutaye huzuni,
Kwani yapiku furaha maishani,
Ikiingia  kukuvamia akilini,
Tadhani huna thamani duniani.

Furaha na amani sote tunataka,
Kuishi vema bila mashaka,
Tuchape kazi tusiogope viraka,
Tuongeze juhudi kakakaka.

Kalamu wino umejiishia,
Nami hapa basi nakomea,
Nakutaka uwe na furaha,
Usisahau akiba kujiwekea.


Na Kizito Mpangala

NINAONDOKA

$
0
0
Ndugu zangu sikieni, mimi hapa naondoka,
Ninahitaji amani, mirindimo nimechoka,
Ninakwenda kwa jirani, hata kama akifoka,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Mitaani kuna mambo, twakimbizana daima,
Yapo mengi machafuko, yananitisha daima,
Yatokea milipuko, inanipatia homa,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Risasi zinasambaa, mirindimo inazidi,
Naishia kutambaa, ninapigwa na baridi,
Ninawasha mishumaa, kufukuza ukaidi,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Waasi nao watisha, siwezi kuvumilia,
Mikutano waitisha, mapigano kutulia,
Wakirudi wanawasha, bomu kutufyatulia,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Jirani niwie radhi, hali yangu waiona,
Unigawie ardhi, na wanangu nitapona,
Yaone yangu maradhi, nisaidie kupona,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Siwezi kuishi hapa, na milio ya risasi,
Mabomu yanalipuka, jirani kabisa nasi,
Wanangu hawana raha, wanalala kwenye nyasi,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Ndoto yangu kuwa hai, kila siku nilalapo,
Ninahitaji uhai, na wanangu waliopo,
Hatupuganii chai, amani hapa tulipo,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Ninataka hewa safi, siyo kama iliyopo,
Inanuka tu baruti, inakuwa na uvundo,
Vumbi limetamalaki, mchakato wa mapigano,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Ninataka maji safi, si haya niliyonayo,
Yamechafuliwa maji, ninaumia kwa moyo,
Maji kweli ni uhai, hapa kwetu ni uchoyo,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Nitakuwa mkimbizi, niipate tu amani,
Sihitaji kuwa mwizi, kuna nini duniani,
Hatuna pia mavazi, ni haya tu ya mwilini,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Ninakwenda kwa jirani, nikaipate hifadhi,
Kuitafuta amani, na kipande cha ardhi,
Nipokeeni jamani, niyaondoe maradhi,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Mashamba yangu hakika, yana hali mbaya sana,
Yamegeuzwa uwanja, wa vita kupigana,
Na mimi sina hatia, moyoni ninaumia,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Siasa za kupigana, hazitazaa matunda,
Waasi wanazaliwa, watazidisha ununda,
Mimi sitaishi hapa, moyo wangu unadunda,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Vikao vingi vyafanywa, kukomesha mapigano,
Haionekani dawa, kuponyesha mirindimo,
Nabaki nimeduwaa, naumia kwenye moyo,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Bunduki zinarindima, zimekuwa kama bao,
Siwezi kuishi hapa, penye sauti za ndumo,
Uhai ninautaka, sipendi kuwa na ndweo,
Nianondoka jamani, amani naitafuta.

Kwa herini waungwana, mimi sasa mkimbizi,
Tutakuja kuonana, hadi iachwe bunduki,
Ninahitaji kupona, makovu haya kichwani,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.

Wasalamu natamka, ninakwenda kwa jirani,
Hapa mimi nimechoka, nianatafuta amani,
Nalazimika kutoka, nikaishi ugenini,
Ninaondoka jamani, amani naitafuta.


Na Kizito Mpanagala

PAMBO LA NDOA

$
0
0
Ndoa ni kitu johari, thamani yake nyumbani,
Ndoa usiikahiri, utakuwa matatani,
Ndoa yahitaji siri, zihifadhiwe chumbani,
Pambo la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.

Kuvumiliana nako, ni muhimu kwenye ndoa,
Usiupende unoko, utakutia madoa,
Nawirisha ndoa yako, isinuke fondogoa,
Pambo la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.

Pambo la ndoa si pesa, ni mapenzi nakwambia,
Hata pesa ukikosa, mapenzi yatafidia,
Ninakuambia sasa, kwa masikio sikia,
Pambo la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.


Penzi halina mwalimu, wanandoa mfahamu,
Mlidumishe lidumu, sizungumzi fonimu,
Nisikilize ghulamu, lisikufikie ghamu,
Pambo la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.

Mapenzi pambo la ndoa, wanandoa nawambia,
Yaepukeni madoa, ndoa kuwaharibia,
Hamwezi kukokotoa, kwa hisabati na bia,
Pambo la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.

Msikilizane vema, jeuri ya fedha noma,
Zungumzeni daima, kwa wema nayo hekima,
Mapenzi yape heshima, mnapoishi daima,
Pambo la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.

Migogoro itupeni, mbali isionekane,
Yadumisheni mapenzi, tena mvumiliane,
Msifanye unajisi, na wala msizozane,
Pambo la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.

Wasalamu kutamka, sio kauli kukata,
Sasa muda wa uraka, na ulimi unanata,
Ndoa kuwa na viraka, inaongeza utata,
Pambo la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.

Na Kizito Mpangala

FUKWE ZA NYASA KATIKA PICHA

DAR ES SALAAM TANZANIA

TUZO YA NOBEL: NGUGI WA THIONG’O HOI TENA!!!!

$
0
0
Kazuo Ishiguro (pichani) raia wa Uingereza ameshinda tuzo ya Nobel katika fasihi kwa mwaka 2017. Amepata ushindi huo baada ya kuwabwaga washindani wake Margaret Atwood, Ngugi Wa Thiong’o na Haruki Murakami.Vitabu vyake ni kama ifuatavyo:-

RIWAYA
1.The Remains of the Day(1989)
2.Never Let Me Go(2005)
3.The Unconsoled (1995)
4.An Artist of the Floating World(1986), 
5.The Buried Giant(2015)
6.A Pale View of Hills (1982),
7.When We Were Orphans (2000).

TAMTHILIYA
1.A Profile of Arthur J. Mason (1984)
2.The Gourmet (1987)
3.The Saddest Music in the World (2003)
4.The White Countess (2005).

HADITHI FUPI
1.Introduction 7: Stories by New Writers (1981)
2.The Summer After the War(1983)
3. A Family Supper (1983)
4. A Village After Dark (2001)
5. Nocturnes: Five Stories of Music and Nightfall (2009).


SOMO LA LEO; SHERIA

$
0
0
Kifungu cha 6(1)(h) cha Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Nam 7/2001 kinaipa mamlaka na uwezo Tume kukagua Magereza (pamoja na Vyuo vya Mafunzo) na sehemu ambazo watu wanazuiliwa kwa mujibu wa sheria ili kufanya tathmini na kukagua hali ya haki za watu wanaozuiliwa humo na hatimae kutoa mapendekezo yatakayotatua au kuondoa matatizo yatakayoonekana.

WAKOLONI WALITUPOTOSHA KWA ELIMU YAO

$
0
0
NA HONORIUS MPANGALA, 0628 994409

MIONGONI mwa mambo ambayo waafrika hatutakiwi kujiuliza kuhusu wakoloni na wawekezaji kwanini wanapenda kukimbilia kuwekeza au kama walivyokuja kutawala afrika,jibu ni jepesi tu, utajiri wetu. Utajiri wa bara la afrika unatokana na uwepo wa rasilimali alizotuzawadia mwenyezi mungu Tangu anaiumba hii dunia.

Wako wengi wanaoshangaa wanapoambiwa kuwa katika karne ya 15 maendeleo kati ya afrika na ulaya yalikuwa sawa. Ni miongoni wa maswali yaliyopendwa sana kuulizwa katika mitihani ya somo la historia kwa masomo kidato cha tano na sita, kuwa inasadikika katika karne ya 15 maendeleo kati ya Afrika na Ulaya yalikuwa sawa. 

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akiwa na baadhi ya watanzania wanaoishi nchini Marekani.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya makatibu mbalimbali
 Hapo ndipo uliweza kuona watu wakitumia mifano mbalimbali ya kirejea kutoka kwa misafara kama ya mabaharia kina Bartholomew Diaz,Vasco Da Gama na Hata Christopher Columbus. Kitu pekee kilichosababisha kuliacha bara la afrika likawa na utofauti kuanzia karne ya 15 hadi sasa na kuonekana hakuna ulinganishi wowote utakaoweza kujionyesha uwiano wa kimaendeleo kati yao na sisi waafrika.

Ziko sababu lukuki zilizochangia tuendelee kupiga ‘mark time’ kama gwaride la mgambo wa jiji la Lubumbashi kule Kongo.  Sehemu kubwa ambayo wazungu walifanikisha ni kushika akili zetu na kutuaminisha katika mambo yasiyokuwa na msaada wa kutufanya tupige hatua ya kimaendeleo.

Upelelezi wa wazungu kabla ya kuja kututawala ulikuwa wa vitu vingi japo kuwa wanahistoria wetu wanaeleza tuu wapelelezi walitafiti maeneo yenye rutuba na hali nzuri ya hewa ili walowezi na wakoloni wanaweza kuishi na kufanya Kazi zao na kujiona wakiwa katika mazingira yanayofanana na wao kwa hali ya hewa.

Kitu ambacho naamini hakikuwekwa wazi ni upelelezi juu ya uwezo wetu wa kiakili katika utendaji wa Kazi na kuchanganua mambo. Hapo ndipo mzungu alipoona umahiri wetu wa matumizi mazuri ya akili lakini tulilwamishwa na mazingira yaliyotunzunguka tu.
Baada ya kugundua hilo waliona kuwa endapo tutawapa ujuzi ka upatikanao kwetu (ulaya) basi waafrika wangeweza kupiga hatua Kali zaidi katika maendele ya bara kiujumla. Labda tu niwaambie mwenyezi Mungu aliwaumba wanadamu na kuwaweka duniani kutazama mambo kadhaa ikiwapo ni wapi akae kutokana na uwezo wake wa kuhimili hali ya hewa ya maeneo husika. Ndio maana ni nadra kusikia seruji imedondoka Afrika, au kusikia Magonjwa ya Mafua ya ndege au Mafua ya nguruwe na mengineyo.

Uwepo wetu barani afrika ni kutokana na tabia ya nchi na hali ya hewa kiujumla ambayo watu wa ngozi nyeusi wamudu vyema kuwepo katika mazingira haya. Tukija katika suala la magonjwa kama Ebola ,malaria ni rahisi sana kusambaa ktk bara letu kutokana na hali ya hewa ya bara letu kwa ujumla.

Bara letu lina hali zote zinazopatikana katika Tabia ya nchi yaani Tabia ya kiikweta,kitropiki na kijangwa. Sababu ya elimu ndiyo pekee iliyokuwa chenga kubwa waliyotupiga wazungu kwa kutuchagulia aina hii ya elimu ambayo imeendelea kufuatwa karibia na mataifa mengi ya afrika.

Mfumo wa elimu waliotuanzishia tumekuwa tukipambana sana kuubadili katika maeneo tofauti lakini tumeshindwa kuwaondoa watu katika dhana ya kuajiriwa na kupata maarifa ya kuweza kujiajiri na kusaidia kuondoa tatizo la ajira katika bara letu kwa sababu tu ya aina ya elimu tuliyoipata.

Wazungu baada ya kuona babu zetu wana uwezo mkubwa wa kutumia akili na mikono yao katika kuunda vitu mbalimbali hivyo laiti kama wangekuwa na viwanda basi akili za vizazi na vizazi zingeegemea huko tofauti na walichokifanya cha kuvunja viwanda vyetu vya asili na kutuelekeza katika elimu ya kuelekea kuajiriwa katika serikali ya mkoloni tena kwa ngazi za chini sifa ikiwa tu anafanya kwenye serikali ya mkoloni.

Elimu ya ufundi ndiyo pekee iliyokuwa na msingi wa maendeleo ya viwanda kwa kuanzia chini hadi kufikia mambo ya teknolojia. Na hii ndiyo ambayo ingekuwa na msaada mkubwa kwa Afrika kwa sababu ingesaidia kuinua maendeleo ya bara la afrika.

Kunyimwa kwetu elimu ya ufundi ambayo Leo hii imeweza kudhihirika duniani kuwa sayansi na teknolojia imetokana na masuala ya ufundi ambayo yamekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo. Akili ya woga wa waafrika kupenda kufanya Kazi maofisini kwa kutumia kalamu ilikuwa ni heshima sana na kuwafanya wajione wana mazingira ya kizungu na kuona washika spana ni watu ambao hawana elimu yeyote.

Akili ya kujiona ni hadhi sana na kuthaminiwa kufanya kazi maofisini kwa kutegemea kalamu kulifanya akili za waafrika kuwa 'dormant' na kudhani aliyeko kiwandani ni mjinga na hajapata elimu. Tulijengwa katika mazingira ambayo leo hii babu zetu waliishia kutusimulia nilifanya kazi na wakoloni pasipo kuelezea faida iliyopatikana kimaarifa baada ya kuachana na wakoloni.

Laiti kama elimu ambayo wangetoa ingekuwa ya ufundi wa mambo mbalimbali ungetengeneza msingi bora wa kuwaandaa watu kuiljiajiri na kusaidia kuinua maendeleo ya nchi au bara letu. Ni dhahiri usemi wa asemaye kuajiriwa ni woga wa maisha unaweza kuwa kweli kutokana na mazingira yaliyopo kwa kuhusisha elimu tupatayo na ongezeko la wanaohitaji kuajiriwa na sio kujiajiri.

Akili tuliyonayo ukiona mtu kujiajiri tunaamini hakubahatika kusoma na aliyeajiriwa kabahatika kusoma jambo ambalo ni kinyume kabisa na linalotengeneza utegemezi wa akili katika kuishi. Hakuna tajiri duniani aliyeajiriwa ila tajiri anaajiajiri kwa kutenda mambo yake kwa elimu aliyoipata.
Nimetazama video moja ya mtoto wa kichina ambaye kwa mwonekano hajafikisha umri miaka 12 lakini elimu ya ufundi na teknolojia aliyoipata itamfanya apende zaidi na zaidi kitu anachokuwa nacho kwa sababu amejifunza angali mdogo na anakipenda.

Mtoto anaendesha Katapila na kunifanya nifikirie mbali zaidi juu ya msingi wa elimu yetu tuliyoachiwa na wakoloni nikatazama elimu yao,mwisho wa siku najipa majibu kuwa wakoloni kuna walichokigundua toka kwetu endapo tungepata elimu ya ufundi na teknolojia ambayo leo hii imekuwa msaada mkubwa katika maendeleo dunia kwa sasa.

Kuna watu kadhaa waliwahi kuniambia kuwa ukitaka kutazama utofauti wa elimu ya ufundi na ile ya kutumia kalamu basi wachukue watu waliosoma masuala ya mabomba (plumbing)' yule aliyeko vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) na yule aliyeko Chuo Kikuu kwa kozi hiyo hiyo na wakufanyie matendo ya namna ya kutengeneza ‘Intake’ ya maji.

Utakacho kipata ni mambo mawili tofauti yule wa VETA atakuwa mzuri sana katika elimu ya matendo wakati yule wa Chuo kikuu anaweza kuwa bora katika maelezo lakini kutenda ikawa tofauti, nafikiri unaweza kuwa shahidi wa maeneo yako.
Unakutana na injinia yeye ni injinia wa makaratasi tu na sio wa kufika eneo la kazi na kutenda. Hii yote ni kutokana na akili zetu za kuamini kazi ya matumizi ya kalamu na sio nyundo, koleo, au spana. Tunatakiwa kubadilika kiakili na kutambua kuwa elimu ya ufundi na teknolojia ndiyo ambayo ingekuwa msaada mkubwa sana kwa vizazi na vizazi.

Hatuwezi kutamani kuwa na nchi ya viwanda wakati akili za wanafunzi na wananchi kwa ujumla hazibadilika na kuona kuna kila sababu ya kuvitumia vyuo vyetu vya ufundi na teknolojia pamoja na mashule yetu ya ufundi kuwa ndiyo msaada pekee wa kutoa mazao ya hao watakaokuja kuwabadilisha wengine na kuhamasisha umuhimu wa elimu hii ya ufundi na teknolojia.

Kama tukawaanda watu wakasoma kozi mbalimbali na baadaye tukawajenga katika kutambua ujenzi wa nchi au bara unafanywa na wenyeji kwa kuwa na elimu nzuri ya ufundi na teknolojia kwa sababu tuko katika karne inayotumia teknolojia zaidi kuliko nguvuwatu. Hebu fikiria kama itatokea watoto wakapata maarifa kwa kutumia teknolojia huko madarasani unajiuliza Mwalimu amayetegemea kalamu ama nguvu yake kufundisha atakuwa na kazi gani.

Kila mmoja atathimini elimu tupatayo na mchango wake katika maendelo ya nchi hii. Tukumbuke neno maendeleo linatoa taswira ya uchumi wa nchi au mahali fulani. Ulaya tunao waona wanamaendelo ni kutokana na kujikita katika teknolojia na ufundi.

Ifike mahali tutambue nini tunataka , tuna watu gani wanaoweza kutupatia hicho tunachokitaka. Unaposema viwanda lazima uandae akili ya watu wako kimtazamo kujielekeza katika viwanda kwa kuvipa hadhi vyuo vya ufundi ambayo ndiyo kichocheo cha maendeleo ya viwanda.

ALFRED NOBEL: MHANDISI MWANZILISHI WA TUZO YA NISHANI YA AMANI YA NOBEL.

$
0
0

NA KIZITO MPANGALA, 0682 555 874

ALFRED NOBEL ni mtu aliye wazi masikioni mwa wengi lakini akifahamika zaidi kwa jina lake la mwisho yaani Nobel kutokana na tuzo aliyoianzisha katika amani, lakini kwa sasa tuzo hiyo imepanuliwa zaidi, haipo katika amani tu, bali ipo katika uga mwingi duniani na washindi wanapatikana kila mwaka kulingana na uga husika ambayo hubebwa na jina lake la mwisho yaani Nobel. 

Nobel alizaliwa Oktoba 21, 1833 jijini Stockholm nchini Sweden. Alikuwa ni mvumbuzi, mtaalamu wa Kemia, mfanyabiashara, mwanaphilanthropia na mhandisi katika viwanda mbalimbali ambavyo kati ya hivyo vipo vilivyomiliki yeye mwenyewe kikiwemo kiwanda cha Bofors ambacho kilikuwa kinajishughulisha na kufua vyuma na vyuma vya pua.
Alfred Nobel.
Alizaliwa katika familia ya kipato cha chini ambapo baba yake Mzee Emmanuel Nobel alikuwa mhandisi pia. Katika malezi yao Alfred Nobel na wadogo zake watatu walisalimika kuishi miaka mingi zaidi wakati wenzao waanne wakipoteza uhai kwa sababu mbalimbali. Hivyo kati ya watoto nane wa Mzee Immanuel Bernhard Nobel, bwana Alfred alijihusisha na kazi ya baba yake. Alijiunga katika mafunzo ya uhandisi katika himaya ya Mwanasayansi wa Sweden bwana Olaus Rudbeck ambapo alipendelea zaidi masuala ya milipiko (explosives) jambo ambalo alianza kulipenda kwa kujifunza misingi yake alipokuwa na baba yake nyumbani.

Baadae alilazimika kufuatana na baba yake huko Urusi na kuishi katika jiji la St. Petersburg na kufanya kazi ya uundaji wa mashine mbalimbali na baruti za kiwango cha kawaida. Hii  ni baada ya baba yake kushindwa katika harakati kadhaa za biashara ndipo alipoamua kwenda Urusi ambako kipawa cha Alfred Nobel kiliongezeka zaidi.  

Katikati ya mwaka 1867 na 1887 alifanya ugunduzi wa baruti kali ambayo inatumika katika silaha za kivita hasa milipuko, lakini lengo lake kuu lilikuwa itumike katika upasuaji wa miamba migodini, na katika kutobolea sehemu za milima ambazo zilihitajika kupitishwa reli. Alifanikiwa katika hilo na lilimuongzea kipato zaidi. Kutokana na utaalamu huo, leo hii katika Kemia kuna elementi ambayo inaitwa Nobelium ambayo ni elementi iliyo katika kundi la elementi za kisasa (Synthetic Elements) 

Hapo wazazi wake walipopata morali ya kumuendeleza zaidi Alfred. Walimpeleka katika shule mbalimbali ikiwemo Ufaransa, Marekani, na nyumbani kwao Sweden. Baada ya mafunzo ya miaka kadhaa, yeye na wazazi wake walirejea kwao Sweden kutoka Urusi na wakaanzisha kiwanda cha kisayansi kwa mara nyingine baada ya kiwanda cha kwanza kilichoanzishwa na baba yake kufilisika na kukumbwa na mlipuko ambao ulisababisha kifo cha mdogo wake wa mwisho, jambo hilo lilipelekea magazeti mengi kuchapisha taarifa inayofanana kimakosa ikimtuhumu Alfred Nobel kumfanyia mdogo wake majaribio ya kulipua baruti aliyoivumbua na ikasemwa na yeye mwenyewe amefariki. Magazeti mengi yalichapisha habari hiyo yenye kichwa cha “LE MERCHAND DE LA MORT ES MORT” ikiwa na maana ya “BEPARIWA KIFO AMEFARIKI” yaani “THE MERCHANT OF DEATH IS DEAD”. 

Alifaulu kuanzisha kampuni zake za masuala ya kisayansi ambazo ziliendelezwa na wengine baada ya kifo chake, na hivi sasa bado zipo. Kampuni hizo ni pamoja na AkzoNobel na Dynamite Nobel. Baruti alizozivumbua kwa ujumla ziligawanyika katika makundi matatu ambayo ni GELIGNITE, BALLISTITE, na CORDITE.

Licha ya kutopata elimu ya sekondari na chuo kikuu, aliweza kuzimudu     lugha sita ambazo ni Kijerumani, Kiswidishi, Kiitaliano, Kirusi, Kiingereza, na Kifaransa. Pia aijifunza fasihi na kuwa mwanafasihi hasa katika ushairi kutokana na kumbukumbu aliyoiacha katika kitabu chake cha ushairi (diwani) kilichoitwa NEMESIS, na tamthiliya katika kitabu cha ESPERANTO.
Mwanzilishi wa tuzo ya nishani ya Nobel Bw. Alfred Nobel akitafakari jambo.

Alfred Nobel alifikwa na wasiwasi mwingi katika ugunduzi wake wa baruti kali baada ya kuona matumizi yake katika silaha za kivita yamekuwa ni ya kuangamiza uhai wa wengine wengi duniani. Hakukata tamaa, alitafuta mbimu itakayoweza kusaidia kupunguza matumizi ya baruti hiyo katika mauaji mbalimbali yafanywayo kwa milipuko. Hapo ndipo alipata wazo kuu la AMANI. Baruti yake ilisifika na bado inasifika kwa kuwa na uwezo wa kuua watu wengi zaidi kwa wakati mmoja. Hii ni ile inayotumika katika mauaji ya kimbari. 

Aliiheshimu sana amani katika ulimwengu huu hasa zama alizokuwepo ambapo mbio za mapinduzi ya kisayansi katika viwanda zilishika kasi sana, hivyo alihofia sana suala la matumizi holela ya baruti aliyoivumbua ambayo inatumiwa katika silaha kama ilivyokwishasemwa awali. Hivyo basi, katika hati yake ya wosia alianzisha TUZO YA NOBEL kwa ajili ya mafanikio ya kisayansi lakini pia kwa ajili ya amani duniani ambalo ndilo jambo lililomsukuma sana. Baruti hiyo kwa sasa imekuwa msingi mkuu wa uundaji wa mabomu yanayotegwa chini ya ardhi. 

Mwaka 2001, mtoto wa mdogo wake Alfred Nobel  bwana Peter Nobel aliiomba Benki kuu ya Sweden kuanzisha nishani nyingine ya masuala ya uchumi ambayo itabebwa na jina la Nobel jambo ambalo limefanikishwa. Na zaidi ya hilo, nishani hii ya Nobel sasa imekuwa nishani kubwa zaidi duniani ambapo imejikita katika uga mbalimbali ikiwemo Sayansi, Hisabati, Uchumi, Fasihi, Amani na kadhalika. 
Mojawapo ya medali za tuzo ya nishani ya Nobel.


Mwaka huu 2017 kikundi kinachopinga matumizi ya silaha za nyuklia ndio kilichoshinda tuzo hii ya Nobe. Hatupaswi kumlaumu Alfred Nobel, yeye tayari alishaona dosari ya matumizi ya baruti hiyo ndipo alipobuni mbinu ya kuepuka matumizi holela ya baruti hiyo kwa utoaji wa tuzo kwa aneyekuwa mstari wa mbele kuhimiza amani duniani. Alifariki miaka minne kabla ya kuingia karne ya 20, yaani mwaka 1896, 10 Disemba.

Baadhi ya watu ambao wamewahi kutunukiwa nishani hii katika uga mbalimbali ni Nelson Mandela, Kalamcnand Mahatma Gandhi, Mama Teresa wa Kalkuta, Kazuo Ishiguro, Albert Einstein na kadhalika.

© Kizito Mpangala        

SOMO LA LEO

$
0
0
"Sitaki kulieleza zaidi jambo hili. Lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa. Vitu vingi sana vimepanda bei; na kila mtu kaumia; wenye kipato kidogo waliumia zaidi kuliko wenye kipato kikubwa. Tumetangaza bei zaidi kwa mazao ya wakulima na tumepandisha mishahara ya wafanyakazi wote. Najua sasa hivi kuna kushangilia kwingi kila mahali. Wakulima wanashangilia na wafanyakazi mnashangilia. Mnayo haki ya kushangilia, kwa sababu vitendo hivyo vya Serikali vinaweza kuinua hali ya maisha ya Watanzania. Nasema, vinaweza. Sikusema lazima vitainua maisha ya watanzania"

Mwalimu Julius Nyerere; Mei 1974.

MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI.

$
0
0

NA MWANDISHI WETU

WIZARA  zimeongezeka kutoka 19 hadi 21, Mawaziri kutoka 19 hadi 21, Manaibu Waziri kutoka 16 hadi 21. Wataapishwa ni Jumatatu tarehe 9/10/2017 asubuhi kwenye saa tatu au saa tatu na nusu.

Rais Magufuli: Pia tumeongeza Mawaziri 2 na Manaibu Waziri 5
Rais Magufuli: Waziri wa Mazingira amebaki kuwa January Makamba, Naibu atakuwa Mh. Kangi Lugola.


Rais Magufuli: Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi tumeigawa na kuwa Wizara 2 za Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Selemani Jaffo amepandishwa na kuwa Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, kabla alikuwa Naibu kwenye Wizara hiyo.Mbunge George Mkuchika ameteuliwa kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora.

Rais Magufuli: Mbunge Luhaga Mpina ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Abdallah Ulega ameteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo. Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuwa chini ya Waiziri Dr Philip Mpango na Naibu Waziri Dr Ashatu Kijaji

Wizara ya Kilimo Waziri ni Charles John Tzeba, na Naibu Waziri ni Marry Mwanjelwa. Wizara ya Habari utamaduni wasanii na Michezo, Waziri ni Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri ni Juliana Shonza

Wizara ya Madini, Waziri ni Angela Kairuki na Naibu Waziri Harun S Nyongo. Wizara ya Nishati, Waziri atakuwa Medadi Kalemani, Naibu Waziri atakuwa Subira Hamisi.

Katibu wa bunge atakuwa Steven Kagaigai na Dkt. Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine.







LUTENI JENERALI MIKHAIL KALASHINKOV: MWASISI WA BUNDUKI YA AK – 47

$
0
0
Na Kizito Mpangala

Alizaliwa tarehe 10 Novemba mwaka 1919 nchini Urusi. Alikuwa ni mtoto wa wazazi Timofey Aleksandrovich Kalashinkov (baba) na Aleksandra Frolovna Kalashinkova (mama) akiwa ni mtoto wa 17 kati ya watoto 19 katika familia waliozaliwa katika familia hiyo ya wakulima. Baba yake aliweza kusoma na kuandika lakini mama yake katika maisha yake yote hakuweza kusoma wala kuandika. Jenerali Mikhail Kalashinkov alikuwa ni mhandisi wa jeshi la Urusi hasa katika masuala ya silaha ambapo aliiboresha bunduki aina ya AK-47 na kuwa AKM, AK-74, PK Machine Gun, na LMG (Light Machine Gun).

Alinusurika kifo baada ya kugua mara kwa mara alipokuwa mdogo. Alivutiwa na aina mbalimbali za mashine lakini pia alikuwa mtaalamu wa kuandika mashairi akiwa na tumaini la kuwa mshairi mahiri katika fasihi ya Urusi. Aliendelea na morali hiyo na kuweza kuandika vitabu sita  na kuendelea kuandika mashairi muda wote wa maisha yake.


Alipokuwa akiishi na wazazi wake katika kijiji cha Kurya nchini Urusi alijishughulisha na uwindaji pamoja na kilimo, hiyvo alikuwa akiitumia mara kwa mara bunduki ya baba yake katika shughuli hiyo ya uwindaji ili kupata kitoweo. Hakupata elimu katika chuo chochote lakini alijifunza umakenika. Shughuli ya kuwinda aliendelea nayo mpaka alipotimiza miaka 90 mwaka 2009.

Alichukuliwa na jeshi na kufundishwa shughuli za umakanika baadae akawa askari kamili huku akiendelea na uundaji wa silaha ndogo ndogo. Mwaka 1941 aliumizwa vibaya katika moja ya pambano aliloshiriki hivyo akalazimika kulazwa katika hospitalai ya jeshi la Urusi tangu mwezi Oktoba 1941 hadi mwezi April 1942, ni zaidi ya miezi minne.

Alipokuwa wodini askari wenzake walikuwa wakija kumjulia hali na katika mazunguzmo aliwasikia baadhi wakilaumu silaha duni za jeshi lao. Yeye hakutia kauli yoyote katika jambo hilo katika mazungumzo yale lakini alilitunza kichwani lalamiko lao na baada ya kupata ahueni akaanza kazi ya kubuni bunduki mpya ambayo itataondoa kero ya askari wenzake waliokuwa wakilalamika, ndipo alipoanza na Ak-47.






Bunduki aina ya AK - 47

Mwaka 1947 aliunda silaha ambayo mwanzo aliipa jina la MIKHTIM ambalo lilitokana na herufi tatu za mwanzo za jina lake na herufi mbili za mwazno za jina la baba yake yaani MIKHail TIMofeyevich, lakini baadae ikapewa jina rasmi ambalo ni AUTOMAT KALASHNIKOVA MODEL 1947 hapo ndipo ikafupishwa na kuitwa AK – 47 na ikaanza kutumika huko Urusi lakini baadae ziliundwa nyingi na kuuzwa nchi zingine.

Mwaka 1949 aliunda bunduki nyingine ambayo ilipewa jina la ufupisho AKM (AßTOMaT KaлáШHиKOßa MoдepHизиpoßaHHbIŇ). Baada ya kuafanikisha utengenezaji wa AKM aliweka wazo jipya la kutengeneza bunduki nyingine ambayo ni ya gaharama ya chini. Alifanikisha zoezi hilo na kuipa jina la RPK likiwa ni kifupi cha maneno “Russian PyЧHOŇпyлeMeT KaπáШHиKOßa” ambayo kwa sasa ni jina maarufu ni LMG yaani Light Machine Gun.Aliunda silaha nyingine nyingi kwa manufaa ya jeshi la nchi yake ingawa baada ya kuwaongezea utaalamu wenzake, waliunda silaha nyingi zaidi na kuziuza kwa mataifa mengine.

Sifa kuu anuai kwa silaha zote alizounda ni urahisi wa jinsi ya kuunda, na ubora wake wa kufanya kazi katika hali yoyote ya pamabano, iwe kiangazi, mazika, kipupwe na kadhalika, zinafanya kazi kwa uhakika.

Kalashikov mwenyewe alisema kwamba juhudi zote hizo ni kwa manufaa ya nchi yake katika suala la ulinzi na usalam lakini siyo kwaajili ya kufanya biashara ya silaha kama ilivyokuwa imezoeleka miaka kadhaa baada ya kuwazoesha utaalamu askari wenzake ambapo walitengeneza silaha nyingi zaidi na kuziuza kwa matifa mengine. Hii ni kutokana na utaalamu wake ma uzoezfu wake.

Alimiliki asilimia 30 ya kampuni aliyoianzisha huko Ujerumani ambayo aliiacha chini ya usimamizi wa mjukuu wake bwana Igor Kalashinkov. Kampuni hiyo ina lebo ya neno VODKA, ambayo hujishughulisha na utengenezaji wa pombe aina ya Vodka, visu vyenye lebo ya Vodka, na miamvuli yenye lebo hiyo pia. Pombe ya Vodka unaypiona sasa ndiyo inatoka kwenye kampuni yake.

Luteni Jenerali Mikhail Kalashinkov enzi za uhai wake

Rais wa Urusi Mh. Vladmir Putin akiwa na maafisa wa jeshi walipokuwa wakizindua toleo jipya la AK - 47

Bunduki aina ya AK – 47 imekuwa katika matumizi rasmi katika zaidi ya mataifa 55 duniani kama sehemu ya michoro ya bendera zao kama vile Msumbiji, Zimbabwe, pia na baadhi ya vikundi kama vile kikundi cha wanamgambo cha Hezbollah.  Katika maisha yake yote ametunukiwa nishani mbalimbali ambazo kwa ujumla zote ni 53. Alikuwa mwanajeshi wa kutumainiwa nchini Urusi katika masuala ya utengenezaji wa silaha. Hii ni kutokana na morali yake alipoona kuwa askari watatu au wane wanatumia silaha moja kwa kupokezana.  

Baadhi ya matamko yake katika maisha yake ya kijeshi ambapo aliamini kuwa Mungu ndiye msimamizi wa kipawa chake cha ufundi, aliwahi kesema

“Walaumuni Wanazi wa Adolf Hitler kwa kuwa wamenichochea niunde silaha nyingi zaidi. Mimi nilitaka kutengena mashine za kilimo lakini Wanazi wamenigeuzia kibao”

“Nilipokuwa mdogo nilisoma mahali pameandikwa kuwa Mungu anasema chochote ambacho lina utata achana nacho ila kilichorahisi kwako basi kiendee, basi mimi kicho rahisi ni ufundi wa silaha ili kulinda nchi ya mababu zangu”

“Nina furaha sana kwa ugunduzi na ubunifu wangu katika silaha kwa lengo la kuilinda Urusi, lakini ninasikitika sana kwa kuwa zinatumika kigaidi. Nilipenda kuunda mashine za kilimo ziwasaidie wakulima”

“nilitengeneza silaha kwaajili ya ulinzi wa nchi yangu, kwa hiyo, siyo kosa langu jinsi inavyotumika mahali ambapo hapastahili. Wanasiasa ndio walaumiwe kwa hili”

Kalashinkov alimwandikia barua padre wa kanisa alilokuwa akisali. Barua hiyo aliiandika miezi sita kabla ya kifo chake mwaka Disemaba, 2013. Barua hiyo iliruhusiwa kuchapishwa magazetini, na aya mohawapo aliandika hivi

“Ninaumwa maumivu ya kiroho. Ninapaswa kuwajibishwa kutokana na uvumbuzi wangu wa silaha kwa kuwa vifo ni vingi mno vinavyosababishwa na silaha zangu ingawa sikuwa na matarajio hayo”

Alisifiwa sana kwa uzalendo wake katika taifa lake la Urusi mapaka kifo kilipomkuta mnamo mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 94.

© KizitoMpangala
     0692 555 874


NIMEWASILI

$
0
0
Salama nimewasili, jirani kanipokea,
Mekaa kwenye kivuli, upepo unapepea,
Nimekuwa mdhalili, mengi yamenipotea,
Nimewasili salama, jirani kanipokea.

Nilikotoka najuta, watu wengi wamekufa,
Mazingira ya utata, yamejaa nyingi nyufa,
Maadui masalata, ni kama vile malofa,
Nimewasili salama, jirani kanipokea.

Kwetu kweli kunatisha, mirindimo ya bunduki,
Maisha inakatisha, na matatizo lukuki,
Hali ile inachosha, waasi hawabanduki,
Nimewasili salama, jirani kanipokea.

Kuupata usalama, hapa kwa jirani yangu,
Ni mimi wa kusimama, kufata kanuni humu,
Nimefika hapa jana, mambo yasiwe magumu,
Nimewasili salama, jirani kanipokea.

Nimekuja mikono wazi, uninusuru jirani,
Siwezi kusema wezi, ndio hali ya nyumbani,
Kurudi sasa siwezi,  tajiweka matatani,
Nimewasili salam, jirani kanipokea.

Nilipokuwa nyumbani, ndoto nyingi niliota,
Moja kubwa maishani, uhai kuutafuta,
Nilikuwa mashakani, uhai kuupata,
Nimewasilio salama, jirani kanipokea.

Ndoto zingine jamani, mazingira yaliukata,
Nashukuru kwa uhai, ndoto niliyoitunza,
Uhandisi nilitamani, sikuweza kuupata,
Nimwasili salama, jirani kanipokea.

Bora huku ugenini, vema niishi salama,
Sijiweke matatani, nisionewe  mashaka,
Nakushukuru jirani, tuhurumie fukara,
Nimewasili salama, jirani kanipokea.

Kwetu hali si salama, hatari ndani kukaa,
Hali ilivyo mbaya, bunduki twafyatuliwa,
Waume na kina mama, na watoto twaumia,
Nimewasili salama, jirani kanipokea.

Asante kwa mapokezi, nitaishi kwa amani,
Sitakuwa mchokozi, nakushukuru jirani,
Bora ninyime andazi, uniachie amani,
Nimewasili salama,  jirani kanipokea.

Na Kizito Mpangala

PENZI LA TAIFA; MKASA WA CATALONIA (BARCELONA) KUJITOA HISPANIA

$
0
0
Mfalme Ramon Berenguer wa IV wa Barcelona alimuoa Malkia Petronilla kutoka ufalme wa Aragon. Ndoa hiyo ilichochea muungano kati ya ufalme wa Aragon na Catalonia(Barcelona). 

Mwaka 1469 ulishuhudia ndoa nyingine ya kifalme. Ilikuwa ndoa kati ya Mfalme Ferdinand wa II (Antequera) wa ufalme wa Aragon na Malkia Isabella wa I wa Castila (Madrid). Ndoa hiyo ilichochea muungano Castila na Aragon.
Baada ya ndoa hiyo ndipo nguvu ya mamlaka na siasa ilihama kutoka Aragon kwenda Castila (ambako iko serikali kuu kwa sasa yaani jijini Madrid). Kuanzia hapo serikali kuu ilitoka Madrid, na Catalonia kuwa na serikali ya jimbo. 

Tayari tumeona ufalme wa Aragon umeungana na Catalonia (Barcelona), kisha Castila (Madrid) ikaungana na Aragon. Maana yake falme zote nne ziliunda nchi moja. Hispania. Baadaye ikaongezeka Sevilla, Granada na kadhalika.  
Hakika lilikuwa la taifa. Lakini sasa WANATAKA KUACHANA.

Malkia Isabella wa I

KUMBUKUMBU YA ERNESTO CHE GUEVARA

$
0
0
LEO imetimu miaka 50 tangu mwanamapinduzi wa Argentina Enersto Che Guevara alipouliwa huko Bolivia. Che anafahamika kwa harakati zake za kupigania uhuru wa nchi kama DRC/Cuba na nyingine nyingi. Aliwahi fika Tanzania miaka ya 1960 Kupitia Ujiji-Kigoma na kukaa miezi saba kabla hajaondoka kuelekea Cuba. 
 
Che Guevara alikuwa ni Mwanaharakati/Mwanadiplomasia/Mjamaa na Mwanamapinduzi katika Karne ya ishirini. Mchango wake unakumbukwa na wengi Duniani, alikuwa ni swahiba Mkubwa wa Rais wa Cuba hayati Alejandro Fidel Castro #Socialism.


ZENZILE MIRIAM MAKEBA: MWANAMUZIKI ANAYEKUMBUKWA NA WENGI BARANI AFRIKA.

$
0
0
Na Kizito Mpangala

Zenzile Miriam Makeba alizaliwa mwaka 1932 jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Alizaliwa kwa wazazi wenye asili tofauti kikabila, baba yake ni Mxhosa, na mama yake ni Mswazi. Bibi yake alikuwa mkunga wa jadi na ndiye aliye fanikisha z0ezi la kumsaidia mama yake kujifungua salama. Bibi yake huyo alimuasa mama yake Miriam kwamba asione taabu na asijisikie upweka kumlea mtoto (Miriam) katika hali duni ya maisha kwani ndiye aliyemleta ulimwenguni. Alikuwa akimwambia “Uzenzile” kwa lugha ya Xhosa, likimaaniasha “Umemleta wewe mwenyewe”, hivyo akaamua kumpa mtoto huyo jina la ZENZILE MIRIAM MAKEBA.

ZENZILE MIRIAM MAKEBA

Licha ya baba yake kuwa mwalimu, lakini walikabiliwa na ukata ambapo alipotimiza siku
18 tu tangu azaliwe alilazimika kwenda kuishi gerezani na mama yake ili apate kunyonya. Aliishi gerezani na mama yake kwa muda wa miezi sita, hii ni kutokana na Makaburu walioshinikizwa na  falsafa ya Apartheid walimhukumu mama yake Miriam kifungo cha miezi sita gerezani licha ya kuwaeleza kuwa ana mtoto mchanga na hajamaliza hata mwezi tangu azaliwe. Lakini hakusikilizwa. Sababu ya kuhukumiwa kifungo hicho ni baada ya kukutwa (mama yake Miriam) akiuza pombe ya kienyeji maarufu sana nchini Afrika Kusini ambayo inaitwa umqombot. Ndugu, jamaa na marfikia walishindwa kumlipia faini kutokana na ukata wa uchumi, hivyo ilibidi akaishi gerezani.

Alipokuwa na umri mdogo, Miriam alikuwa mwanakwaya katika kanisa lao la Methodisti. Baada ya kifo cha baba yake alilazimika kufanya kazi mbalimbali ili kupata ridhiki, hapo akachukuliwa na tajiri mmoja ili akahudumu kama “house girl” katika nyumba yake, huku mama yake akipewa kazi za kufanya usafi katika nyumba za Makaburu jijini Johannesburg, na baadae wakahamia katika mkoa wa Transvaal.

Alipokuwa mkoani Transvaal, mwaka 1949 akiwa na miaka 17, Miriam alilazimishwa kuolewa na polisi aliyekuwa mafunzoni na mwaka 1950 walibahatika kupata mtoto mmoja, Bongi Makeba. Baadae Miriam aligundulika kuwa na kansa ya titi ndipo mume wake akampiga na kisha kumtelekeza moja kwa moja baada ya miaka miwili tu ya kuishi ya ndoa yao.

Zenzile Miriam Makeba akitumbuiza
Miriam Makeba alianza kuwekeza rasmi katika muziki alipokaribishwa na kujinga katika bendi ya watu wa Cuba iliyoweka makazi yake nchini Afrika Kusini, bendi hiyo iliitwa Manhattan Brothersambapo alikuwa mwanamke peke yake katika bendi hiyo. Akiwa na bendi hiyo mwaka 1953aliatoa wimbo wake wa kwanza kwa lugha ya Xhosa ulioitwa “Laku Tshoni Ilanga” na akatambuliwa rasmi kitaifa kama mwanamuziki.

Akiwa bado na bendi hiyo, licha ya kushirki katika bendi zingine za wenyeji, mwaka 1955alionana na kijana mmoja mwanasheria ambaye alijitambulisha kwake kwa jina la Nelson Mandela. Nelson Mandela alijieleza kwake kuwa amemfuata ili kumpa hamasa zaidi ya kukosoa falsafa za Apartheid kupitia muziki. Kisha akamwambia si lazima aimbe kuhusu Apartheid tu, bali yapo mengine anaweza kuyaimba. Akazungumza naye maneno ya kumuongezea morali na mwisho akamwambaia “Miriam, usikate tama, utakuja kuwa mtu muhimu kwenye taifa letu hili

Mwaka 1956 alitoa wimbo mwingine ambao aliuimba kwa lugha ya Xhosa lakini baadae ukatafsiriwa kwa Kiingereza na ukaingia katika chati ya nyimbo 100 bora duniani kwenye rekodi ya Marekani iliyoitwa “US Billboard Top 100 na picha yake ikatumiwa katika ukurasa wa mbelewa jarida la Drum.

Mwaka 1959, Miriam alijizolea sifa na pongezi kemekem baada ya kuigiza kwenye filamu iliyoitwa “Come Back Afica” ambayo ilikuwa na maudhui ya yaliyokuwa yakikosoa falsafa za Apartheid nchini humo. Ni filamu ambayo ilirekodiwa kwa siri kubwa ili kuepuka pingamizi la serikali ya Makaburu kwa kuwa ilikuwa na uhalisia wa hali ya juu sana. Baadae mwongozaji wa filamu hiyo alimlipia viza Miriam na kumuambia aende nchini Italia kuhudhuria tamasha la filamu la kitaifa nchini humo. Uhodari wa Miriam katika filamu hiyo ulitambuliwa kimataifa na alipaswa kusafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani ili kucheza mubashara jukwaani.

Miriam alipata huzuni kubwa kutokana na kifo cha mama yake ambaye aliuawa katika shambulio la mauaji ya kimbari ya Sharpeville yaani Sharpeville massacre mwaka 1960 wakati yeye akiwa uhamishoni nchini Marekani. Alipotaka kusafiri kurudi nyumbani ili kuhudhuria mazishi alifanyiwa hujuma ya kufutiwa passport yake ya kusafiria. Katika mauaji ya kimbari ya Sharpeville alipoteza ndugu zake wengine wawili.

Miriam Makeba alikwenda nchini Kenya mwaka 1962 katika harakati zake za muziki akiwa na lengo la kuishawishi serikali ya Walowezi iiache Kenya iwe huru, yaani aliongeza hamasa ya kupigania uhuru wa Kenya. Alimchangia Mh. Jomo Kenyatta fedha za matumizi katika harakati zake kama kiongozi wa kudai uhuru nchini humo.

Mwaka huo huo, Miriam Makeba alinyang’anywa uraia wa afrika Kusini na Makaburu waliokuwa wakitawala nchini humo na kupigwa marufuku ya nyimbo zake nchini humo na hata studio yke binafsi ilifungwa. Akafikia hatua ya kuwa mtu asiye na taifa (stateless person). Lakini alisaidiwa na serikali ya Algeria, Ubelgiji, Guinea, na Ghana akapatapassport ya kusafiria, na aliweza kuishi katika nchi hizo tajwa. Katika maisha yake alikuwa na passport9 za kimataifa na alipewa uraia wa heshima katika nchi 10 duniani.

Baada ya misukosuko hiyo, Miriam Makeba alialikwa na Mh. Haile Selassie nchini Ethiopia akatumbuize katika sherehe za kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika. Na katika misukosuko ya ndoa yake ya pili, alifanywa kuwa mtu wa kuangaliwa sana kutokana na ujasiri wake katika kupinga falsafa za Apartheid, hivyo Makaburu wa afrika Kusini waliwasiliana na serkali ya Marekani ambako alikuwa anaishi imchunguze kwani Makaburu walihisi kuwa Miriam ana mafunzo ya kijeshi. Hivyo, shirika la ujasusi la CIA liliweka kamera kwa kificho katika nyumba yake aliyokuwa akiishi huko Marekani. Baadae FBI nalo likajiunga katika mchakato wa kumchunguza Miriam Makeba.

Hii ni baada ya kuolewa na mwanaume mweusi wa Marekani ambaye naye aliwekewa mashaka. Miriam na mumewe waliposafiri kwenda Bahamas walizuiliwa na serikali ya Marekani wasirudi tena. Mumewe alikuwa akiitwa Stokely Carmichael. Baada ya kuzuiliwa kurudi Marekani ndipo Miriam alipotumia passportaliyoipata kutoka serikali ya Guinea na akaenda huko  na mumewe. Wakati wakiwa Guinea mumewe alilazimika kubadili jina na kuitwa Kwame Toure. Waliishi Guinea kwa zaidi ya miaka 10, wakawa watu wa karibu sana wa rais wa nchi hiyo Mh. Ahmed Sekou Toure  ambaye alisifika sana kuheshimu kazi za wasanii wa muziki kutokana na kuvutiwa na muziki wa Miriam Makeba. Tangu mwaka 1968 Makeba  hakurudi tena Marekani hadi mwaka 1987.

Mume wa Miriam Makeba, bw. Stokely Carmichael. Baadae alibadili jina na aliitwa Kwame Toure

Makeba alipokuwa Guinea alikuwa akiandika nyimbo mbalimbali na kuimba kuhusu utwala wa kibaguzi wa Marekani huku akisifu juhudi za Malcolm X, na pia alisifu juhudi za Patrice Lumumba nchini Congo kupitia muziki. Amewahi kualikwa kutumbuiza katika nchi mbalimbali barani Afrika zilipokuwa zikiachiwa madaraka na wakaloni. Amewahi kutumbuiza nchini Tanganyika (Tanzania ya sasa), Kenya, Angola, Zambia, Msumbiji, Liberia na kadhalika. Akateuliwa kuwa mhusika wa shirika la umoja wa mataifa nchini Guinea mwaka 1975.   

Binti yake, Bongi Makeba naye alikuwa mwanamuziki akiwa anaishi nchini Ubelgiji. Kwa bahati mbaya binti yake huyo lalifariki mwaka 1985 alipokuwa anajifungua ambapo mtoto alipona, hivyo Miriam alipaswa kuwalea wajukuu wake wawili, akahama nchini Guinea na kwenda kuishi Brussels Ubelgiji. Mwaka 1987alikwenda nchini Zimbabwe kutumbuiza katika wimbo wake ulioitwa “Sangoma” ukimaanisha “mponyaji”

Mwaka 1990, rais wa Afrika Kusini Mh. Frederick de Clerk alifuta zuio la Miriam Makeba kuishi nchini Afrika Kusini, hivyo aliruhusiwa kurudi nyumbani sambamba na kuachiliwa huru Mzee Nelson Mandela kutoka gerezani. Mwezi June ikiwa ni mienzi minne baada ya kuachiliwa huru Mzee Nelson Mandela, Miriam Makeba alirudi nchini Afrika Kusini kwa kutumia passport ya Ufaransa aliyokuwa amepewa bure, hii ni baada ya kuishi umaishoni zaidi ya miaka 10.

Mwaka 1992aliigiza katika filamu ya Sarafina ambayo inaeleza mambo ya  Afrika Kusini hasa katika matukio ya kinyama yaliyokuwa yakifanyika katika mji wa Southern West Town maarufu kama SOWETO. Na mwaka 1999aliteuliwa kuwa balozi wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia kilimo na chakula, FAO.

Alifanya kazi kwa ukaribu na Mh. Graca Machel-Mandela, kisha alianzisha kituo cha MakebaCenter Of Girls cha watoto yatima. Mwaka 2002 alishiriki katika filamu fupi iliyokuwa ikieleza jinsi watu weusi wa Afrika Kusini walivyokuwa wakipambana dhidi ya  Apartheid nchini humo. Filamu hiyo inaitwa Amandla. Ameandika vitabu viwili vya wasifu wake. Kitabu cha kwanza kinaitwa Makeba: My story na kitabu cha pili kinaitwa Makeba: The Miriam Makeba Story.

Mwaka 2008aliugua ghafla kutokana na maumivu katika moyo wake alipokuwa jukwaani akitumbuiza nchini Italia. Alialikwa nchini humo katika tamasha lililoandaliwa ili kumsaidia mwandishi wa vitabu bwana Roberto Saviano ambaye alikuwa anataka kuchapisha kitabu chake kilichokuwa kikieleza maovu yanayofanywa na kikundi cha uhalifu cha Camorra. Ndipo alipofariki.

Miriam Makeba anasifiwa kwa kuchukia kuweka nakshi katika uso wake hasa make up. Alikuwa hapendi kabisa urembo wa aina hiyo na kudai anataka kuwa na mwonekano wa asili. Pia hakupenda kutia nywele zake dawa ya aina yoyote ili ziwe ndefu. Alipenda kuchana nywele zake zikiwa zimesimama vizuri na akazipa jina Afro look yaani mwanekano wa Kiafrika, hapo ndipo neno ‘Afro” lilipozaliwa.

Miriam Makeba alikuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini na hata Marekani. Makaburu walisi kwamba nyimbo zake zinalenga siasa zao lakini yeye mwenyewe alikana jambo hilo na kusema haimbi siasa bali anachokiimba ndio ukweli ulivyo nchini humo. Hapo nyimbo zake nyingi zikapigwa marufuku.

Yapo mengi aliyoyafanya na kuyapa kipaumbele katika harakati za maisha yake hasa katika harakati za kudai uhuru. Mzee Nelson Mandela alikuwa akimuita Miriam Makeba kwamba ni mama wa taifa la Afrika Kusini katika muziki. Miriam Makeba ni mmojawapo wa washawishi wa kuwepo kwa muziki pekee nchini Afrika Kusini maarufu kama Kwaito. Mpaka alipofariki, Miriam Makeba alikuwa na mtoto mmoja tu.


© Kizito Mpangala  (0692 555 874,  0743 369 108

RUVUMA: WANANCHI WAKERWA KUUZIWA KONDOMU

$
0
0
Wanawake wa kijiji cha Lumecha wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuweka ratiba ya kudumu ya utoaji huduma za uzazi wa mpango bure kwenye vijiji vya pembezoni ili kuwasaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi usio salama.

Wananchi hao wamekerwa na kitendo cha kutozwa fedha mbalimbali za vipimo ikiwamo kuuziwa mipira ya kiume, kuweka vipandikizi, kuchoma sindano na kupima watoto kliniki.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na wanawake hao wakati wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili ambapo walionyesha uhitaji zaidi wa kupatiwa elimu na huduma za uzazi wa mpango.

Mmoja wa wanawake hao, Neema Komba alisema huduma hiyo imekuwa ikitolewa kwa zamu ambapo wakienda wataalamu wa afya kutoka taasisi ya Marie Stopes wamekuwa hawatozwi fedha, lakini siku za kawaida kuweka vipandikizi wanalipia Sh10,000, mipira ya kiume wanauziwa Sh1,000, kuchoma sindano za kujikinga na mimba Sh2000 na kupima watoto kliniki Sh200.

Alisema wanawake wengi hawana uwezo wa kulipia huduma hizo, hivyo hujikuta wakitumia njia za kienyeji na wengine huzaa mara bila mpango kutokana na kukosa elimu sahihi ya uzazi salama.

Neema alisema kijijini hapo idadi kubwa ya watoto wanajilea wenyewe kutokana na wazazi wao kuelemewa na idadi kubwa ya watoto waliozaa bila mpango hivyo kushindwa kuwahudumia kwa kuwaendeleza kielimu.


Kwa upande wake, Agnela Hyella alisema bado tatizo la upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango katika kijiji hicho ni kubwa na limechangia wanawake wengi kuzaa idadi kubwa ya watoto ambao hawana uwezo wa kuwatunza.

Mganga wa zahanati ya kijiji cha Kingerikiti ambayo pia inahudumia wananchi wa Lumecha, Linda Sanga alikana wanawake kutozwa fedha akisema huduma hiyo inatolewa bure na kuahidi kufuatilia iwapo kuna baadhi ya wahudumu ambao wanafanya vitendo hivyo.

Muuguzi wa zahanati hiyo, Emelita Mapunda alisema tatizo kubwa wananchi ni imani potofu kwamba huduma hizo zina matatizo, lakini kila baada ya miezi mitatu Marie Stopes hufika kwenye zahanati hiyo na kutoa huduma bure.

Aliwataka wananchi hao kujitokeza ili waweze kusaidiwa kwa kuwa vipandikizi vipo vingi na kondomu za kutosha.

Mganga mfawidhi hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Magafu Majura alisema ili kuondokana na tatizo la utoaji mimba usio salama elimu juu ya kuepuka mimba zisizotarajiwa kwa akinamama wote walioolewa, wasioolewa pamoja na wanafunzi wa kike inapaswa kutolewa mara kwa mara.

Kwa mujibu wa taasisi ya Children Choice ya Marekani, wanawake saba kati ya 100 hupata mimba bila kutarajia kila mwaka huku mwanamke mmoja kati ya sita hakuwa amepanga kupata ujauzito nchini Uingereza mwaka jana, lakini aliupata bila kutarajia na hivyo kulazimika kujifungua.


Chanzo: Gazeti la MWANANCHI, Toleo la leo Oktoba 9/2017


MIAKA 50 TANGU CHE GUEVARA AUAWE, BADO ANAISHI

$
0
0
NA ZITTO KABWE
 
MIAKA 50 imetimia tangu Komredi Che Guevara auwawe huko Bolivia mnamo tarehe 9/10/1967. Che, mwanamapinduzi mzaliwa wa Argentina na mkombozi wa Cuba ni mmoja wa wanadamu waliojitoa mhanga kupambana dhidi ya ubeberu kote duniani. Katika maisha yake aliwahi kupita Tanzania na kushiriki kwenye vikao na vyama vya ukombozi kusini Mwa Afrika. 

Tanzania iliunganishwa na Che kupitia Zanzibar. Vijana wa Zanzibar walipelekwa mafunzoni Cuba Kwa ajili ya ukombozi. Mwaka 1962 wakati wa mgogoro wa Oktoba 1962, vijana wa kizanzibari waliokuwa mafunzoni Cuba walijitolea kupigana bega Kwa bega na waCuba dhidi ya Marekani. Jambo hili liliwafungua macho wacuba kuhusu Afrika na Kwa hakika Afrika yao ilikuwa Zanzibar.

Vijana hao baadhi yao wapo hai wakiwa ni wazee Sasa. Mmoja ni Mzee Ali Sultan Issa na Komred Shaaban ( pichani nikiwa naye nyumbani Kwa balozi wa Cuba ). Pia Dkt. Salim Ahmed Salim akiwa Mkuu wa Ofisi ya Zanzibar kule Havana, Cuba. Mzee Ali Sultan Issa ndiye alikuwa mwenyeji wa Che huko Zanzibar mwaka 1965. Prof. AbdulRahman Mohamed Babu, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Zanzibar na baadaye Waziri wa zamani wa Uchumi wa Tanzania alikuwa mtu wa karibu wa Che Guevara. Pichani walipokuwa kwenye mkutano huko Geneva, Uswiss. 

Kwa sisi watu wa Kigoma Ujiji Che Guevara ana historia kubwa. Che alikwenda Congo mwaka 1965 kupigana dhidi ya mabeberu waliomwua Patrice Lumumba. Alikaa huko miezi 7. Alipokwenda Congo alipitia Kigoma na kulala nyumbani Kwa Mkuu wa Mkoa wakati huo akiitwa Semvua Msangi ( mtoto wa Semvua alikuwa Mwalimu wangu Shule ya Sekondari Kibohehe Moshi, akiitwa Zidikheri Semvua Msangi). 

Che alipanda Boti kutokea kijiji cha Bangwe kwenda Congo. Hata alipokuwa akifanya mikutano walifanyia Kigoma mjini akiwa pamoja na kina Mzee Laurent Kabila ambaye baadaye alikuja kuwa Rais wa DRC.
Che Guevara katika nyakati hizi aliitwa Tatu huku mwenzake Dreke akiitwa Moja ili kuficha majina yao ya asili. 

Moja bado yupo hai na Kwa kushirikiana na ubalozi wa Cuba tumemwalika kuja nchini na yeye pamoja na aliyekuwa Myeka wa Che wataambatana na baadhi ya Watanzania kwenda Kigoma Kwa kufuata njia aliyopita Che.
Manispaa ya Kigoma Ujiji imeamua kutunza historia Hii Kwa kuiita Che Guevara Barabara inayoanzia Stesheni ya Reli mpaka mji wa Bangwe. Pia mazungumzo yanaendelea na Meya wa Mji wa Cadiz katika Nchi ya Spain ili kujenga jengo la makumbusho mjini Kigoma Kwa ajili ya kuenzi nafasi ya Kigoma katika juhudi za ukombozi dhidi ya ubeberu barani Afrika. 

Che Guevara ni alama halisi ya mwanamapinduzi wa kimataifa aliyepinga dhuluma kokote duniani. Maneno yake ya mwisho Kwa mkewe na wanawe yalidhihirisha hilo. Aliwaambia uzuri wa uanamapinduzi ni kuchukia dhuluma inayofanyika dhidi ya yeyote popote duniani. Kwa kimombo alisema;
"Above all, always be capable of feeling deeply any injustice committed against anyone, anywhere in the world. This is the most beautiful quality in a revolutionary.”
Che bado anaishi.

Zitto Kabwe Ni mbunge wa Kigoma Mjini

Viewing all 535 articles
Browse latest View live