Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mazoezi ya siku 14 ya pamoja ya makamanda wa kijeshi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki yanakayojikita katika kupambana na matukio ya ugaidi. Mazoezi yatafanyika katika kituo cha ulinzi wa amani cha jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ Kunduchi jijini Dar es Salaam.
↧