Quantcast
Channel: KARIBUNI NYASA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 535

MFADHILI WA DHIKI

$
0
0
Nikiwa katika ufukwe wa forodha ya Lundu, Nyasa.
Nilitamani nguo kupiga pasi,
Hakika hilo tena siwezi,
Kwetu umeme wa manati,
TANESCO hisani nifanyieni,

Umeme wahakika nipatieni.

Mimi ni muuza Juisi
Kama yule fundi Kinyozi,
Jenereta kwetu hatuwezi,
mitaji yetu kama mkwezi,
Umeme wahakika nipatieni.


TANESCO vyenu visingizio
Daima vimejaa kwenye makolido
Ianzapo mawio hadi machweo
Lini mtakuwa bwana Kipoozeo
Umeme wahakika nipatieni.


Mimi ni fundi wa nyayo
Umeme wanipiga bao
Mashine yakosa mishono
Wateja wasovumilia porojo
Umeme wahakika nipatieni.


Mimi ni fundi nguo,
Nashona kila mtindo
Kiwanda kuibua mitindo
Njaa si rafiki wa tumbo
Umeme wahakika nipatieni.


©Markus Mpangala.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 535

Trending Articles